Serikali kuajiri watumishi 15,000 kuziba pengo la vyeti feki

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Chawene.jpg

Waziri wa TAMISEMI Mh George Simbachawene amesema kuna upungufu wa watumishi wa uma uliosababishwa na uhakiki wa vyeti feki. Hivyo serikali ina mpango wa kuajiri watumishi 15,0000 katika bajeti ya mwaka 2017/18 kuziba pengo hilo.

======

Dodoma. The government will employ 15,000 new workers in 2017/18 financial year to fill the gap created after employment of more than 12,000 public servants were terminated due to lack of guanine academic certificates.

Minister of State in the President's Office, Regional Administration and Local Government (RALG) George Simbachawene admitted that there are shortage of workers in some of public offices following the verification of academic certificates of Public Servants.

He was responding to a question by Busanda Member of Parliament, Loresia Bukwimba who sought to know the government plans to fill the vacancy created by public servants, who were sacked over fake certificates in Geita.

Mr Simbachawene said his office has already submitted evolution report on sectors, which were mostly affected to the ministry of State in President’s office (Public Service and Good Governance) for further employment procedures.

Source: The Citizen
 
Kwa pesa gani..endeleeni kusubiri mpka ajira za kisiasa 2020..serikali haina pesa inapumulia mashine..itawalipa nini ikiwaajiri.
 
Serikali ya Blah! Blah! semeni tu kuwa wale vyeti vyeki mlikuwa mnapunguza mzigo wa wafanayakazi kwani serikali haina pesa za kulipa mishahara.

Hata walimu wa sanaa mliwazungusha sana ila mwisho wa siku mlikuja kusema ukweli.

Hii ndio serikali ya wanyonge wa Chattle ila sio watanzania wote.

Serikali kutangaza ajira mpya 15000 ndani ya miezi miwili kabla ya mwaka wa fedha 2016/2017 kuisha

=====

Mpango huo ulitangazwa jana mjini hapa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Dk. Laurian Mdumbaro, kwa vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa Dk. Ndumbaro, kutokana na uamuzi huo, waajiri wanatakiwa kuhakiki vyeti vya watumishi walioomba ajira kabla ya kuwaajiri.

“Wanatakiwa kuhakiki kabla watumishi hawajaajiriwa, wanatakiwa kuhakikisha vyeti vya waliomba kazi au usahili viwe vimehakikiwa na mamlaka husika kama ni cheti cha kidato cha nne, sita au ualimu au vyovyote viwe vimehakikiwa na mamlaka husika,” alisema.

Dk. Ndumbaro alielekeza kuwa vyeti vihakikiwe na Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) au chuo chochote kile kiwe ni chuo kikuu au vya Mamlaka ya Ufundi Stadi (Veta), vihakikiwe kabla hawajapata ajira mpya.

ATHARI KUONDOA WENYE VYETI FEKI

Wakati huo huo, Dk. Ndumbaro alisema kutokana na kuwaondoa watumishi wenye vyeti feki, kuna maeneo yameathirika kihuduma na kuwaagiza waajiri kwenye maeneo hayo kuwaandikia barua au kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Utumishi ili kutoa kibali cha ajira cha dharura.

Alisema kibali hicho kitatolewa ili huduma zisiathirike.

“Waajiri wote kwenye serikali za mitaa na sekta za umma kwenye maeneo ambayo yameathirika sana na zoezi hili la vyeti feki watoe taarifa kwa Katibu Mkuu Utumishi mara moja ili kutoa vibali vya dharura waweze kuajiriwa watu wenye sifa kufanya kazi hizo,” alisema Dk. Ndumbaro.

Alipoulizwa kama ajira zilizotangazwa zinalenga kuziba pengo la watumishi walioondolewa kwa vyeti feki, alisema bado kuna watu wanakata rufani na nafasi zilizotangazwa ni zaidi ya idadi ya watumishi wenye vyeti feki.

“Tulikuwa na mpango wa kuajiri, mwanzoni tuliajiri watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, walimu wa sayansi, madaktari tulikuwa kwenye mwendelezo huo wa ajira hizo. Hii ikikamilika tutatoa ajira zingine,” alisema.

Kuhusu mchanganuo wa ajira, Katibu Mkuu huyo alisema mchanganuo wa ajira hizo utatolewa kwa kuainisha kada zote kulingana na idadi hiyo.

“Kuhusu ajira elfu 71 zilizotangazwa zilikuwa ni za mwaka 2015/16, lakini mwaka ule yalifanyika mambo mengi… kulikuwa na programu ya kuweka sawa mishahara ya walimu wa vyuo vikuu waliokuwa wakipata mishahara tofauti,” alisema.

Alisema sehemu ya fedha zilizotengwa kwa ajira hizo ilitumika kuweka sawa mishahara ya walimu hao wa vyuo vikuu na kuwapadisha vyeo watumishi ambao hawakupandishwa kwa muda mrefu.

“Fedha zilizobaki tumeendelea kutoa ajira awamu kwa awamu,” alisema Dk. Ndumbaro.

Chanzo: Nipashe

Back
Top Bottom