Serikali kuajiri walimu wapya wa masomo ya Sayansi na Hesabu kukabiliana na uhaba uliopo

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Serikali inatarajia kuajiri walimu wengine wapya hususani wa masomo ya sayansi na hisabati ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo katika shule za sekondari nchini.

Hayo yamesemwa na waziri wa nchi ofisi ya Rais-TAMISEMI, mheshimiwa Ummy Mwalimu(mb) akiwa ziarani katika mkoa wa Kigoma.

Katika hatua nyingine, waziri Ummy amezitaka shule zote za sekondari nchini zilizo na mapungufu ya walimu wa masomo ya sayansi kuainisha mahitaji yao ili serikali iweze kupeleka walimu wa masomo ya fizikia, kemia, biolojia pamoja na hesabu ili kuhakikisha kila shule ya sekondari inapata walimu wa masomo hayo.

OR-TAMISEMI
 
Ni kosa kubwa kubwa kudhani kuwa Sayansi inaweza kufundishwa bila sanaa.

Sanaa ndiyo iliyozalisha sayansi na haya masomo hayawezi kutenganishwa.
 
Kabla ya kuendelea kuajiri tu hao walimu wa masomo ya sayansi nashauri serikali ingefanya kwanza research kujua chanzo cha uhaba wa walimu wa sayansi miaka yote unatokana na nini wakati vyuo vyetu kila mwaka vimekuwa vikizalisha walimu hao?

Je wanakwenda wapi wakati hata kipindi ajira zilipo kauka , wao waliajiriwa japo kwa idadi ndogo?

Kwa utafiti mdogo nilioufanya mimi nimegundua ni serikali yenyewe ndio chanzo cha tatizo hilo, kwani walimu wengi wa sayansi wamekuwa ama wakiacha kazi serikalini na kwenda shule za binafs au kwenda kujiendeleza katika fani nyingine au kuajiriwa na makampuni binafsi yote ikiwa ni kufuata maslahi mazuri kutokana na serikali kupuuzia suala la maslahi yao huku wakibeba mzigo mkubwa wa vipindi tofauti na walimu wa sanaa.

Hivyo tatizo hili litabakia kuwa sugu hadi hapo serikali itakapoamua kuboresha maslahi yanayovutia walimu kuendelea kutumikia kazi hiyo!
 
Upo sahihi mkuu. Walimu wa sayansi wanafanya kazi kubwa ila malipo kiduchu. Ndio maana wengi wao wanakimbilia private ambapo wanajali kiasi fulani.
 
Walimu wa sanaa wanaajiriwa kwenda kufundisha shule za msingi mkuu
Serikali hii hii! By the, way nimejaribu kuangalia majina ya ajira yaliyotoka wiki chache zilizopita, nikagundua walimu wenye elimu ya chuo kikuu wa masomo ya sanaa walichaguliwa wachache sana!

Astashahada na Stashada ndiyo walikumbukwa zaidi! Na kwa hali hii, maana yake bado kuna kundi kubwa mtaani la walimu wa shahada wa masomo ya sanaa!
 
Serikali inapita njia ndefu kukabiliana na kiwango cha elimu kushuka.rekebisheni maslahi ya walimu walipwe mishahara mizuri ,wapewe posho alafu wapimwe kulingana na ufaulu wa wanafunzi kwenye masomo yao kwa ajili ya kupata promosheni au kupanda madaraja.
 
Serikali inatarajia kuajiri walimu wengine wapya hususani wa masomo ya sayansi na hisabati ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo katika shule za sekondari nchini.

Hayo yamesemwa na waziri wa nchi ofisi ya Rais-TAMISEMI, mheshimiwa Ummy Mwalimu(mb) akiwa ziarani katika mkoa wa Kigoma.

Katika hatua nyingine, waziri Ummy amezitaka shule zote za sekondari nchini zilizo na mapungufu ya walimu wa masomo ya sayansi kuainisha mahitaji yao ili serikali iweze kupeleka walimu wa masomo ya fizikia, kemia, biolojia pamoja na hesabu ili kuhakikisha kila shule ya sekondari inapata walimu wa masomo hayo.

OR-TAMISEMI
Elimu siyo kipaumbele kwa viongozi wetu,
 
Hizi ajira hazichukuliwi seriously kuwa there is a high demand of teachers, viongozi wanachukulia ni kama favour kwa mashule yenye uhitaji, wanafanya mambo kama zima moto, ina maana hawakujua uhitaji uliopo
 
Elimu siyo kipaumbele kwa viongozi wetu,
Eti Kipaumbele ni kujenga sanamu la milion 400 ndo unabaki unajiuliza hiki kiasi cha pesa kama kingewekwa kwenye elimu kingeweza kuajiri walimu wangapi??
 
Back
Top Bottom