Serikali kuajiri Walimu wapya 7,000 ili kuendana na ongezeko la madarasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,869
Waziri wa elimu Prof Mkenda amesema kutokana na ongezeko la madarasa ya uviko pamejitokeza hitaji la walimu wapya hivyo Serikali itaajiri walimu 7000 kukata kiu hiyo.

Chanzo: ITV habari

1643357162667.png

 
Dah na ndio ajenda zao hizo...

Wanasiasa lolote wanalofanya huwa ni kujiandaa na uchaguzi ujao... Hakuna ajenda kama serikali ila ni matamko tu kila siku...
 
Waziri wa elimu Prof Mkenda amesema kutokana na ongezeko la madarasa ya uviko pamejitokeza hitaji la walimu wapya hivyo Serikali itaajiri walimu 7000 kukata kiu hiyo.

Chanzo: ITV habari

Kutokana na ongezeko la wanafunzi sio ongezeko la madarasa! zamani walikuwa wana shifts mbalimbali
 
Mwaka 2020 wakati wanainadi kwa mbwembwe nyingi ilani yao yenye kurasa 303, walitoa ahadi lukuki kuhusu ajira. Waliahidi kutengeneza idadi ya mamilioni ya ajira kwa kila mwaka mpaka ifikapo mwaka 2025.

Kwa kufanya mchanganuo wa kimuelekeo, kwa mwaka 2021 peke yake hawa mbwiga sijui hata kama wanaweza kutupa takwimu sahihi kuhusu jumla ya ajira walizokwisha kuzitengeneza katika utumishi wa umma.

Tumeingia sasa 2022, "employment creation" imeanza kwa kuangalia eneo moja la ajira kutokana na ongezeko la madarasa, sasa Je! Serikali imejiandaa vipi kisera kuwaingiza katika ajira iliyo rasmi na isiyo rasmi lundo la vijana waliohitimu elimu ya msingi ya kati na ile ya juu?

Serikali kupitia wizara ya kazi, ajira na maendeleo ya vijana ni lazima iumize kichwa. Isitafute visingizio ama kutoa majibu rahisi eti vijana wajiajiri wao wenyewe. Kama kisingizio ni idadi kubwa ya vijana, walete majibu mazuri imewezekanaje kwa mataifa makubwa yenye idadi kubwa sana ya watu kama vile China na India kuweza kumudu hali hiyo.
 
Kwenye bajeti walitenga kuajiri 10000 Leo Ni 7000
Hona hili theeenge nalo,limeweka na emoj eti vya kujichekesha,

Bichwa kubwa akili hauna,

Ebu tuambie msukuma mwenzio aliajili wangapi??? Hizo chuki zenu kwa Samia zitaondoka na roho zenu mbwa nyie
 
Madarasa yaliyoongezeka ni 15 000, iweje waajiriwe 7000 ambao ni kidogo kabisa?!! inastahili kuajiri mara tatu yake......yaani 45,000.
Nionyeshe waliposema kwamba baada ya hao elfu Saba,hawatoajili Tena,kwaiyo ulitaka kwa mkupuo mmoja ken&ge wewe
 
Back
Top Bottom