Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,477
51,043
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri basi lazima itekelezwe, serikali lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!
 
Siasa na dini mpaka kwenye soka!

Yanga wapinga agizo hilo la TFF/Serikali

Hii ni tweet ya Maulid Kitenge:

Taarifa fupi ya Yanga kwa Vyombo vya habari imesema wao watapeleka timu kama ratiba inavyosema saa kumi na moja na kulitaka Shirikisho la soka la TFF, liheshimu kanuni ya 15 inayohusu taratibu za mchezo ambayo inasema mabadiliko yoyote ya muda wa mchezo yatajulishwa saa 24 kabla.
 
Athari na chembechembe zingine zilizobaki za utawala wa awamu ya tano kujitolea matamko.

Michezo ina mfumo wake maalum ambayo hupangwa kwa muda mrefu lakini mazoea ya awamu ya 5 yameharibu kabisa utawala wa sheria, mifumo, taratibu na kanuni.

Nchi inategemea zaidi tamko la waziri, wizara, mkuu serikali za mkoa au rais au rais wa TFF bila kuzingatia mambo mtambuka kisheria, kimichezo n.k

Utasikia hata humu JF mtu anaweka " Rais wa Kenya aruhusu waTanzania ..." huku ni kuonesha jinsi jamii ya Tanzania ilivyoathirika na kutegemea zaidi matamko, hisani za mtu / watu wenye mamlaka badala ya kufuata sheria, katiba, kanuni , taratibu labda tu pale panapotokea hali ya hatari kwa wananchi na hizo pia zimeainishwa katika sheria na katiba kwa wingi kabisa nini kifanyike.
 
Athari na chembechembe zingine zilizobaki za utawala wa awamu ya tano kujitolea matamko.

Michezo ina mfumo wake maalum ambayo hupangwa kwa muda mrefu lakini mazoea ya awamu ya 5 yameharibu kabisa utawala wa sheria, mifumo, taratibu na kanuni.

Nchi inategemea zaidi tamko la waziri, wizara, mkuu serikali za mkoa au rais. Utasikia hata humu JF mtu anaweka " Rais wa Kenya aruhusu waTanzania ..." huku ni kuonesha jinsi jamii ya Tanzania ilivyoathirika na kutegemea zaidi matamko, hisani za mtu / watu wenye mamlaka badala ya kufuata sheria, katiba, kanuni , taratibu labda tu pale panapotokea hali ya hatari kwa wananchi na hizo pia zimeainishwa katika sheria na katiba kwa wingi kabisa nini kifanyike.
Hapa tusimlaumu Jiwe!

Haya ni makosa ya serikali ya Samia Full stop!
 
Hapa tusimlaumu Jiwe!

Haya ni makosa ya serikali ya Samia Full stop!

Ni kweli kwa kiasi kikubwa, na ndiyo maana tunaainisha athari mbaya za awamu ya 5 ambazo awamu ya sita imeathirika kiakili na inabidi wazinduke kuondokana na ulemavu wa kifikra, kisaikolojia na kiuamuzi walioachiwa baada ya kuwa chini ya utawala wa awamu ya 5 kwa miaka 5 na miezi 5.
 
Back
Top Bottom