Serikali kuahirisha Mechi ya Simba na Yanga ili kuwalazimisha wananchi wafuatilie tukio la Uzinduzi wa Kitabu cha Mzee Mwinyi ni kitendo cha aibu

Aisee. Inabidi hapa mtaani kwetu tuendelee tu kuvumilia kelele zao za vuvuzela....
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri, bali lazima itekelezwe, lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!

kiukweli walichofanya ni u***
 
TFF HAO wakaidi wakitoa timu uwanjani wapigwe faini.
mpira ule ule tofauti masaa Tu.
 
Hii game sidhani kama itachezwa tena, psychollogy za wachezaji na viongozi zimeshavurugika, hao wapiga kelele wataondoka muda sio mrefu, Yanga wameshaanza kuondoka uwanjani.
Hatakama ikichezwa haitakuwa na amsha amsha yeyote
 
Serikali inatakiwa iwe makini sana, hao wanaowaita wanyonge usiwaguse kuhusu yanga na simba wataandamana hadi vijijini zingua vyote lakin sio simba na yanga
 
Unajua kuna wakati unaweza ukajiuliza hivi tuna viongozi wa serikali wa namna gani.

Inafahamika wazi kuwa ratiba ya Ligi inapangwa muda mrefu na bila shaka kwa kuzingatia matukio mbalimbali makubwa ya Kitaifa na kwa kanuni za Ligi

Sasa inashangaza Leo, mchezo ukiwa umebakisha masaa mawili tu, Serikali inaiagiza TFF kubadili ratiba ya mchezo huu wakati kukiwa na maelfu ya wananchi Uwanjani. Hili ni kosa, Serikali imewakosea sana wananchi.

Kwanza ni lini serikali ikawa na mamlaka ya kupanga ratiba za ligi?

Pili, Serikali inataka Kuwachonganisha wananchi na Mzee wetu mzee Mwinyi, Mtu asiyependa makuu, Kwa nini mlifanye tukio lake kuwa ni adha kwa wengine?—Je mzee Mwinyi ndiye aliyewatuma kubadili ratiba ya mambo mengine ya kijamii kwa ajili yake binafsi?

Huu utaratibu wa kufanya mambo kwa zimamoto zimamoto ni dalili za serikali dhaifu, isiyojiamini inayokurupuka!

Tunataka yeyote aliyehusika kubadili ratiba hii ya mchezo, ambayo wananchi walishawekeza akili zao na muda wao achukuliwe hatua mara moja! . Hatuwezi kuvumilia mikurupuko kama hii.

Na isitokee mkasingizia kuhusu Mfungo wa Ramadhani, Suala la ramadhani lilishajulikana toka mfungo ulipoanza kwa hiyo msisingizie eti kuwapa Waislamu muda mzyri wa kufuturu, Kwanza hata huo muda wa saa moja jioni Waislamu watakuwa bado wanafuturu kwa hiyo Msituletee hoja hii!

Tunataka serikali isifanye mambo kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kutoa amri, bali lazima itekelezwe, lazima iheshimu timetable za wananchi.

Nimekereka sana na uamuzi huu wa Serikali kuingilia ratiba za Mpira, Ni mambo ya ajabuajabu kabisa haya!
1620486894458.png

Mkuu wewe ni mtu mzima acha uzushi-
 
Back
Top Bottom