Serikali kibogoyo, serikali ya hovyo hovyo na dhaifu.

Ni Mimi Msiogope

JF-Expert Member
May 28, 2012
352
200
Nandika hapa nitaandika na pengine kwa kirefu kwenye gazeti la The East African.
Serikali ilipoamua kuwa wezi wa fedha za EPA 'Wazirudishe yaishe' niliifananisha na kibongoyo au Simba wa Kuchongwa!.. Nilihoji mara nyingi pamoja na Watanzania wengine tukaambiwa 'Msitufundishe kazi'.
Serikali ikafanya matumizi ya hovyo hovyo kwa uchache ni kama zile 3.8billion zilizotumika kuileta timu ya Brazil Tanzania, 209Billion kuagiza magari ya Serikali kupitia dalali mmoja huko Japan, Hivi karibuni ikatumia 1.7billion kuwasomesha watendaji 7 wa TCRA nje ya nchi kwa miezi nane, 56milion kwa ajili ya kushona sare za marubani 7wa ATCL, Na mengineyo mengi ya hovyo hovyo (Ambayo yatakuwepo kwenye gazeti)
Serikali dhaifu ikashindwa kufufua viwanda-Huku ikiwahimiza vijana wafanye kazi
Serikali dhaifu ikashindwa kununua hata ndege moja-Baada ya zile saba zote kufa
Serikali dhaifu ikashindwa kukuza uchumi wa kaya-Watanzania na mfumuko wa bei
Serikali dhaifu ikashindwa kulinda hata rasilimali zetu-Wakauza Twiga na Tembo kwenye jiji la Karachi Pakistani!
Serikali dhaifu ikashindwa kuwashtaki mafisadi papa-Kwakuwa ni wana CCM
Na mengineyo mengi!

Dawa ya serikali ya aina hii ni kufanywaje?
Serikali imewatawala watanzania au inawaongoza?
 
hayo Maelezo yenye uzalendo kwa Taifa, wahuni waliyakataa jana Sigida, wakaharibu mazingira
 
hayo Maelezo yenye uzalendo kwa Taifa, wahuni waliyakataa jana Sigida, wakaharibu mazingira

kwa swala la defence, nawasifu wakazi wa singida ingawa wametumia silaha kubwa zaidi, naamini wametoa onyo!!!!!

"msikubali kuchezewa na wahuni wa ccm i.e Mwigulu and the like"
 
kwa swala la defence, nawasifu wakazi wa singida ingawa wametumia silaha kubwa zaidi, naamini wametoa onyo!!!!!

"msikubali kuchezewa na wahuni wa ccm i.e Mwigulu and the like"

Ninachokiona ni kwamba Serikali hii hii legelege itasababisha yenyewe kuondolewa madarakani kwa kuwa watanzania kwenye maeneo yao kila mkoa watakuwa kama Arusha na pengine kuliko!

Yangu mimacho kondo na mikono shavuni
 
Back
Top Bottom