Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,215
- 3,587
Kufuatia ndege kubwa ya shehena ya mizigo kukaribia kukamilika kuundwa kiwandani, serikali imefanya uamuzi wa kubadili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa KIA kuwa kitovu cha kimkakati cha mizigo yaani Strategic Cargo Hub kwa shehena za mizigo ya safari za anga.
Pamoja na kwamba kimsingi uamuzi ni mzuri unaolenga kupunguza msongamano JNIA, Bandari na barabara za Dar pamoja na kuleta hamshahamsha kwenye uwanja wa KIA, lakini hofu yangu ni kuwa shehena hizo zitalazimika kusafirishwa kwa njia ya barabara kwenda sehemu mbalimbali za nchi ikiwemo Dar.
Nachelea barabara ya T2 na zingine kuwa hatarini kuharibika baada ya muda fulani wa hub hii kutingwa.
Mbadala wa KIA nashauri wazo hili zuri litekelezwe kwenye uwanja wa ndege wa hadhi ya kikanda wa Geita Chato (Regional Airport) kwa sifa moja kuu salama kwa barabara zetu; ya kuwa karibu na reli za SGR na MGR ambazo zitapokea shehena hizo toka uwanja wa ndege wa kikanda wa Geita Chato na kuziingiza kwenye mtandao wa reli nchini na kusalimisha barabara zetu zilizojengwa kwa gharama kubwa.