Serikali Katika Utatuzi wa Upungufu wa Umeme Nchini Tanzania

MasterGamaliel

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
642
1,000
Ni kweli kwa sasa kabla ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa Stieglers Gorge Power Project au Nyerere Hydropower Plant, Tanzania kuna upungufu wa umeme unaosababisha kukatwa katwa umeme kwa mikoa mingi inayotumia umeme wa Grid ya Taifa.

Sababu zaweza kuwa nyingi; uchakavu wa mitambo, miundombinu ya usafirishaji n.k

Moja ya mawazo yaliyopo ya jinsi ya kutatua tatizo ni kujenga kituo kipya Mwanza cha kufua umeme (au pengine kuiwasha tena mitambo iliyopo Kijereshi pale Mwanza).

Ni vema Serikali ifikirie kusafirisha umeme kwa miundombinu iliyopo kutokea kwenye mikoa ya karibu na vyanzo vya nishati inayotumiwa na hiyo mitambo ili kuzalisha umeme na kusambaza kuelekea kwenye mikoa ya pembezoni kuliko kusafirisha mafuta au nishati nyinginezo pamoja na vipuri, service and maintenance materials pamoja na human resources kwenda huko mikoani kwa gharama kubwa kwa nchi (ihamishiwayo kwa walaji wa mwisho wa huduma za umeme na kupitia kwenye bei za bidhaa za viwandani).

Serikali iwaze kutatua changamoto za nchi katika lengo nia ya kuhudumia wananchi bila serikali kutafuta faida wala kuwawezesha watu fulani kutengeneza milango ya faida upigaji.

Kuanza kuyapeleka malori ya mahitaji ya mitambo kwa umbali wa kilomita zaidi ya 1000 kwa bara bara ni kuichelewesha nchi.

Tufikirini kujenga nchi yenye uchumi wenye ukuaji jumuishi wa jamii pana.
 
Lubebenamawe

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,588
2,000

Mbona msemaji wa Serikali alisema kwa sasa umeme unaozalishwa nchini tuna ziada ya Mega 200? Sasa upungufu wa umeme umetoka wapi mpaka kuwe na uhitaji wa kujenga kituo kufua umeme kwa nishati ya mafuta.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom