Serikali kama imeshindwa kuzuia biashara ya ngono basi iwatoze kodi wadada poa

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,934
Nilipita kipenyo kimoja Sudan Temeke niliona mabinti wameweka mapaja nje wanatangaza biashara saa nne asubuhi.

Nilijua ni hostel za wanafunzi kwa harakaharaka. Ila nilipounganisha nukta nikakumbuka na kufahamu kuwa wako pale kibiashara.

Serikali yenye vyombo vya ulinzi na usalama zaidi ya vinne imeshindwa kukomesha ushetani huu wa mabinti kujiuza na wanaume kununua?

Nilipita Sokota usiku saa nne niliona barabara wameenea wadada poa, dereva alipunguza mwendo wadada wakaanza kutukaribisha huduma.

Je, wahusika wakuu wa kuzuia huu uhuni nao ni wanufaika wa hii biashara Tanzania?

Wananufaika kwa kununua bidhaa zao au wameamua kupuuzia siku zipite?

Ningekuwa na mamlaka kubwa ningeikomesha hii biashara nchini ndani ya siku 3 tu.

Kama hamtaki au hamuwezi kudhibiti basi muwarasimishe ili serikali ipate kipato kidogo.
 
Ni kweli kabisa, kama madada poa kuuza nyuchi ni kosa kisheria lakini wapo na wanajulikana wanapopatikana na hakuna anaechukua hatua yoyote basi haina budi wakahalalishwa na kusajiliwa chama chao kinachotambulika ili waweze kuwa wanachama kwa maslahi ya kutetea haki zao na kulipa kodi serikalini.

Serikali haioni kuwa hiki ni chanzo kizuri cha mapato? Viongozi wanawaza kununua tu wapinzani. Kama umeshindwa kukemea angalau basi nufaika na hii biashara isiyolipiwa kodi.
 
Sasa hasira zako ni kwasababu serikali haipati kodi kutoka kwa hao wanaojiuza au ni nini? Kwa hiyo wakilipishwa kodi utaifurahia hiyo biashara yao na hautakua na shida nao tena?

Lakini ni dots gani hizo uliunganisha mpaka ukajiaminisha kua "wanauza"? Ulienda kuuliza bei? Waliweka matangazo? Au ulipoona wanawake wanaota jua ukapata hisia kua wanauza?
 
Changamoto ni kwamba,sasa hivi mwanamke anapewa sana nguvu na shetani mwenyewe.

Ukioa,wanasema. huna hela, una kibamia na kwa hiyo atatoka kutafuta mwanaume mwingine nje hata kwa kujilengesha sana.

Ukiwa na hela atasema uko busy na huna muda wa ku- care.Hivyo hata ukimnunulia gari,hausaidii ndo kwanza atakudharau.

Kwa hiyo wanaume wanaogopa kuoa ili kuepuka stress toka kwa mwanamke asiyeridhika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni rahisi sana, tengeneza ajira zisizo rasmi za kutosha ndani ya nchi uone kama wimbi la wanaojiuza halitapungua. Tazama bodaboda na bajaji zilivyogeuka kuwa fursa nchi nzima. Idadi ya vibaka imepungua kwa kiasi kikubwa.

Unapowaambia wanawake wakae vikundi ili watengeneze sabuni za maji, hakikisha umetengeneza uhaba wa sabuni mbadala kutoka nje ya nchi. Hapo utakuwa umepanua uhitaji katika soko la ndani na hivyo mwanamke ataona tija kuendelea kutengeneza sabuni hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom