Serikali kama imeshindwa industrial revolution tafadhali fanyeni agricultural revolution

Kwani kipindi cha jk pembejeo za kilimo tulikua tunapata wapi??

Sasa kwanini hakuna hayo Mapinduzi ya kilimo kama unaona JK alifanikiwa? kwa nini bado hatuna chakula cha kutosha? Kwa nini nchi ya Kenya inaangiza chakula nje ya Afrika na siyo kwetu kama JK alifanikiwa kufanya Mapinduzi ya Kilimo?
 
Mkuu nani kasema jk alifanikiwa?? Mbona unajitungia mada aloo?? Umeuliza pembejeo tutapata wapi mimk nikauliza kwani wakati wa jk zilipatikana wapi?? Jibu swali mkuu!
 
Mtoa mada uko sahihi kinachotakiwa ni serikali kuwekeza ktk miundombinu ya kilimo cha kisasa kama vile kujenga mifumo bora ya kilimo cha umwagiliaji, matractor, machine za kisasa kama vi havester(combine havesters), mowers na piler kwa ajili ya kukatia nyasi ba kupile nyasi za kulishia mifugo, kuwezesha wakulima pembejeo za kilimo kama vile mbegu bora, mbolea, na kutafuta masoko bora ya mazao ya kilimo/mifugo
 
Mkuu nani kasema jk alifanikiwa?? Mbona unajitungia mada aloo?? Umeuliza pembejeo tutapata wapi mimk nikauliza kwani wakati wa jk zilipatikana wapi?? Jibu swali mkuu!

Hilo swali wewe ndiyo ulijibu, kama unaona halikuathiri chochote ni kwa nini Kilimo kimeshindwa mpaka leo hii?
 
Wakati ss huku tunahangaika na vyeti feki, wenzenu wanacheza na makombola, wanaende mbele ss tunarudi nyuma
 
Hilo ni swala lingine, ila najaribu tu kuelezea uhalisia kwamba huwezi kutenganisha haya mambo 2 kama unataka kulima kisasa!
Tunatakiw tufanye moja linalowezekana sasa, hayo matamko ya majukwaani hayatusaidii kitu kwa sasa kutokana hali ya maisha ya sasa,
Wanasiasa wamezidi kuwahadaa wananchi, bora tuelekeze nguvu zetu katika kilimo.
 
Hapa ndipo ninaposhangaa sana, na mara zote nimekuwa sielewi moja kwa moja kuhusiana na swala la viwanda. Najiuliza ni viwanda vya aina gani ambayo tunakurupuka kuvianzisha? Je, tunaweza kujivunia viwanda hivyo vitakavyoanzishwa? Je vitakuwa ni viwanda shindani kama viwanda vya mataifa mengine? Je viwanda hivyo vitakuwa na maslahi mapama kiasi cha kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kuangalia maslahi mapana au vitanufaisha wachache kupitia jasho la wengi na hivyo kugeuza wafanyakazi kuwa watumwa ndani ya taifa letu.

Nitazamapo haya naona tunakimbia, tena tunakimbia ilihali tumeona wenzetu wanakimbia, kwa maana hiyo tunakimbia kwasababu tumeona wenzetu wanakimbia lakini tusiulize wanakimbia nini na je nasi tukimbie wanakokimbilia wao au tutembee. Kwa dhana hii huwa nasikitishwa na jinsi mambo yaendeshwavyo kisiasa, ni jamba la kushangaza kusikia eti mtu kuwa na mashine ya kusagisha nafaka mtaani basi nasi tunachukulia moja kwa moja ni kiwanda. Ni kweli ni kiwanda lakini je ni kiwanda cha namna gani? SIDO?
Mwalimu Nyerere alishindwa sera ya kuinua uchumi kupitia kilimo mwishoni mwa miaka ya 1960s na 1970s tatizo lilikuwa ni kushindwa kuweka mazingira ya uzalishaji wenye tija hii ni kwasababu aliwaachia kazi wakulima wadogowadogo na huku akitarajia matokeo makubwa hapo ndipo akashuhudia mporomoko katika kklimo hususani baada ya ukame. Nadhani Serikali hii inataka kutuambia kuwa inawekeza katika viwanda lakini mwisho wa siku wanaachiwa wenye mashine za kusaga na kukoboa huku wakitarajia tupate bidhaa bora na kuweza kushindana katika soko la kimataifa. Hizi ni ndoto za mchana kweupe pee. Viwanda vinavyotakiwa kuanzishwa na serikali ni kupoteza bajeti iliyotokana na pesa za walipa kodi. Mawazo yangu ni kuwa, serikali inatakiwa kukaa chini na kutafuta njia mbadala itakayowafanya wawekezaji kama Dangote waje kuwekeza viwanda huku yenyewe ikikaa chini kufanya tafiti na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maswala ya kilimo mfano SUA, kutafuta njia mbadala zitakazo watoa wakulima wadogowadogo ambao ndio wengi katika taifa hili na kuwafanya kuwa angalau wakulima wa kati ili kuendana sambamba na uwepo wa viwanda.

Huu ni mtazamo wangu ukiona haujauelewa pita kimya.
 
Sasa kwanini hakuna hayo Mapinduzi ya kilimo kama unaona JK alifanikiwa? kwa nini bado hatuna chakula cha kutosha? Kwa nini nchi ya Kenya inaangiza chakula nje ya Afrika na siyo kwetu kama JK alifanikiwa kufanya Mapinduzi ya Kilimo?
Ndo mana Hapo juu nkasema hivi kaka sasahivi tuweke siasa pembeni, wananchi na serikali tuungane tuwe kitu kimoja tuelekeze nguvu zetu, akili zetu na uwezo wetu wote katika kuleta mapinduzi ya kilimo.
 
Mkuu, umeongea yote, kwa sasa viwanda Ni ndoto, Ardhi ya kilimo Ni kubwa Sana, sasa tumeshindwa kilimo viwanda tutaviwezea wapi jamani?tufanye kile kinachowezekana kwa sasa.maisha yanakimbia Sana.
Hapa ndipo ninaposhangaa sana, na mara zote nimekuwa sielewi moja kwa moja kuhusiana na swala la viwanda. Najiuliza ni viwanda vya aina gani ambayo tunakurupuka kuvianzisha? Je, tunaweza kujivunia viwanda hivyo vitakavyoanzishwa? Je vitakuwa ni viwanda shindani kama viwanda vya mataifa mengine? Je viwanda hivyo vitakuwa na maslahi mapama kiasi cha kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kuangalia maslahi mapana au vitanufaisha wachache kupitia jasho la wengi na hivyo kugeuza wafanyakazi kuwa watumwa ndani ya taifa letu.

Nitazamapo haya naona tunakimbia, tena tunakimbia ilihali tumeona wenzetu wanakimbia, kwa maana hiyo tunakimbia kwasababu tumeona wenzetu wanakimbia lakini tusiulize wanakimbia nini na je nasi tukimbie wanakokimbilia wao au tutembee. Kwa dhana hii huwa nasikitishwa na jinsi mambo yaendeshwavyo kisiasa, ni jamba la kushangaza kusikia eti mtu kuwa na mashine ya kusagisha nafaka mtaani basi nasi tunachukulia moja kwa moja ni kiwanda. Ni kweli ni kiwanda lakini je ni kiwanda cha namna gani? SIDO?
Mwalimu Nyerere alishindwa sera ya kuinua uchumi kupitia kilimo mwishoni mwa miaka ya 1960s na 1970s tatizo lilikuwa ni kushindwa kuweka mazingira ya uzalishaji wenye tija hii ni kwasababu aliwaachia kazi wakulima wadogowadogo na huku akitarajia matokeo makubwa hapo ndipo akashuhudia mporomoko katika kklimo hususani baada ya ukame. Nadhani Serikali hii inataka kutuambia kuwa inawekeza katika viwanda lakini mwisho wa siku wanaachiwa wenye mashine za kusaga na kukoboa huku wakitarajia tupate bidhaa bora na kuweza kushindana katika soko la kimataifa. Hizi ni ndoto za mchana kweupe pee. Viwanda vinavyotakiwa kuanzishwa na serikali ni kupoteza bajeti iliyotokana na pesa za walipa kodi. Mawazo yangu ni kuwa, serikali inatakiwa kukaa chini na kutafuta njia mbadala itakayowafanya wawekezaji kama Dangote waje kuwekeza viwanda huku yenyewe ikikaa chini kufanya tafiti na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maswala ya kilimo mfano SUA, kutafuta njia mbadala zitakazo watoa wakulima wadogowadogo ambao ndio wengi katika taifa hili na kuwafanya kuwa angalau wakulima wa kati ili kuendana sambamba na uwepo wa viwanda.

Huu ni mtazamo wangu ukiona haujauelewa pita kimya.
 
Hiyo agricultural revolution ya Ulaya unayoiongelea ilikuwa kabla ya Viwanda ni kweli lkn hiyo ilikuwa ni hatua mwanzo, kwa sababu Ulaya wao ndiyo waliokuwa wa kwanza na hwakuwa na njia mbadala, ni kama vile usema unataka kujenga Kiwanda cha kutengeneza simu za viganjani leo hii basi uanzie na simu za mshindi kama za Nokia halafu baadaye ndiyo uanze kutengeza smart phone, hauwezi kufanikiwa ukitaka kuanza kuunda ni lazima uanzie pale teknolojia ilipo leo hii yaani smart phone

Hivyo leo hii huwezi kufanya mapinduzi ya Kilimo cha kisasa bila ya kwenda samba samba na viwanda kwani huwezi kushindana na nchi nyingine ambazo wanalima kwa kisasa labda kama unaogelea kilimo cha kutegemea mvua na kupata mahindi ya kula lkn siyo kuwa nchi inayo export mazao!

Ngoja nikuulize pembejeo za Kilimo utapata wapi? Mbolea na dawa za kuuwa wadudu utapata wapi?
Umeuliza swali zuri sana, kule mtwala kunaendelea kujengwa kiwanda cha mbolea, lakini kimeingiliwa na figisu figisu za kisiasa, hapa ndipo ninapopatwa na mashaka kuwa hata vitakapopatikana vingine vitakufa kifo cha mende tu. Rejea kabla ya kuvunjika kwa jumuiya ya afrika mashariki mwaka 1977, mbona tulikuwa tunategemeana viwanda, kwa mantiki hiyo, upande wa zana ka kilimo au pembejeo, tunaweza tu import toka mataifa mengine afu sisi tukajikita katika kuzalisha mazao na ku export.
 
Safi kabisa hicho ndicho nilichoona kwa sasa, bila kufanya hivo,
Hatufiki popote,
 
Ni mapema sana kusema kuwa tumeshindwa kufanya mapunduzi ya viwanda. Hata hivyo ni kama hatujui tufanye nini kufikia mapinduzi ya viwanda, kuna kiwanda kama General tyre, mafundi wapo na soko kubwa sana lipo, ila tunashindwa kuweka machine mpya na kuanza kuzalisha matairi, yaani General tyre wakianza tu kuzalisha matairi kama yale ya zamani, nina hakika magari yote ya kusafirisha watalii yatafunga General.

Vv
 
Umeona eeh, yani wanataka tucheze mziki ambao sio wetu. Na kwasababu wameona watanzania wengi tuna mihemko ya kisiasa wanaamua kugeuza kila kitu ni siasa.
 
Tatizo ubinafsi wa viongozi na kujilimbikizia mali na pili Hakuna inchi ya kidemokrasia chama kimoja kikaa miaka yote
 
Ni mapema sana kusema kuwa tumeshindwa kufanya mapunduzi ya viwanda. Hata hivyo ni kama hatujui tufanye nini kufikia mapinduzi ya viwanda, kuna kiwanda kama General tyre, mafundi wapo na soko kubwa sana lipo, ila tunashindwa kuweka machine mpya na kuanza kuzalisha matairi, yaani General tyre wakianza tu kuzalisha matairi kama yale ya zamani, nina hakika magari yote ya kusafirisha watalii yatafunga General.

Vv
Niliskia wametenga milioni 70 eti kukikarabati na huku kujenga vipya wametenga mabilioni ya pesa. Wamesahau ile nahau isemayo FIMBO YA MBALI HAIUI NYOKA. badala ya kufufua ambavyo vinajivuta wanataka kuwekeza vipya.
 
Sasa
Umeona eeh, yani wanataka tucheze mziki ambao sio wetu. Na kwasababu wameona watanzania wengi tuna mihemko ya kisiasa wanaamua kugeuza kila kitu ni siasa.
Hivi sotoahangaika na siasa kabisa, washinde wasishinde hamna lolote la maana kwa sasa naona tunarudi nyuma hatusongi mbele
 
Kilimo kwanza ilifanya vizuri sana chakula kikawa affordable changamoto ni soko la nje, mimi naona tungekomaa na kilimo na food processing factories tumezungukwa na nchi zenye vita na ukame means hawana chakula so why not selling them Food?
Sawa sawa, hapo ndugu umenena.
 
Back
Top Bottom