Serikali kama haipo au haipo kabisa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kama haipo au haipo kabisa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 8, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  Na Mhariri
  MwanaHALISI


  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda anasema, "haraka haraka nayo haina baraka." Alikuwa akizungumzia suala la serikali kuchukua hatua pale jambo linalohusu jamii nzima linapotokea.

  Msemo huu ambao kwa asili hauna neno "nayo," unahimiza busara kuzingatiwa kabla ya mtu kutenda jambo.

  Je, ni kweli waziri mkuu amesahau kuna misemo mingine isemayo, kwa mfano, "Chelewa chelewa utakuta mtoto si wako;" "Asiyesikia la mkuu huvunjika guu," "Mficha uchi hazai" na "Mficha ugonjwa, kifo kitamuumbua?"

  Leo hii dunia nzima inaishangaa Tanzania na serikali yake. Inaona serikali ya nchi hii haina hata uwezo wa kujua lipi zuri na lipi baya, jambo ambalo watu hufunzwa au huiga tangu utotoni.

  Chukua mifano hii: Kulikuwa na mjadala juu ya nafasi ya Zanzibar katika Muungano – iwapo ni nchi au la. Ilichukua muda mrefu kusema lolote na bado suala hilo linatokota. Ni ngojangoja.

  Kuna mgogoro wa Zanzibar. Rais Kikwete aliuita "Mpasuko." Serikali haitafuti ufumbuzi. Bado ni ngojangoja.
  Ufisadi ni unyama. Ni ukwapuaji wa kinyama wa fedha na maliasili za nchi na kuzitumia kwa manufaa binafsi ya watu wa ndani au nje ya nchi.

  Leo hii bado serikali inaendeleza mijadala juu ya mafisadi, hadi wabunge wanagawanyika pande mbili: Hawa wanataka ufisadi na kuutetea na hawa wanapinga unyama huu. Ni ngojangoja ya Pinda.

  Wazazi wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu, kwa muda mrefu sasa, wamekuwa wakilia na kutaka serikali iweke utaratibu wa kugharimia elimu yao kwani, kwa raslimali zilizopo, hilo linawezekana.

  Serikali haisemi lolote la maana. Inajua jibu moja tu: Hakuna fedha. Inaacha walie na kusaga meno na ikiwezekana watawanyike na kuacha masomo. Ni ileile ngojangoja.

  Yapo masuala mengi ambayo serikali inapaswa kuchunguza na kuchukulia hatua kabla wananchi hawajachoka.

  Hata kwa ngazi ya familia, lazima awepo kiongozi wa kuchukua hatua msimamo kwa masuala na inakuwa vema kama kiongozi anashirikisha wadau wote.

  Tunahimiza siku zote serikali ichukue dhamana iliyopewa na wananchi ya kuongoza kwa kuonyesha njia. Haidhuru hata kama uamuzi wa kwanza utakuwa na kasoro.

  Afadhali kuwa na mwenye maamuzi yenye kasoro zinazosahihika kuliko asiyetoa uamuzi wowote.
  Serikali isiyo na uamuzi katika masuala makubwa, hata madogo, ni kama haipo; na kama hakuna serikali, basi kuna vurugu. Wananchi hawakuchagua vurugu.
   
 2. Baridijr

  Baridijr Member

  #2
  Aug 8, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa jinsi wananchi walivyo kosa imani na hii serikali ya JK nahisi watanzania watakuwa na furaha na amani ya kweli iwapo tu wataambiwa serikari imejiuzuru licha haipo
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wako wanakula taratibu na hwataki shida , ukitaka kujua kama wapo basi gusa maeneo yao ya kuingizia mlo kwenye matumbo yao hapo utaijua serikali .
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna rafiki yangu mmoja humu JF alikuwa anauliza kuwa `je serikali inaweza kurogwa`!
  Mimi nasema kuwa serikali yetu imerogwa!

  Mwalimu wangu mmoja alipata kunifundisha kwamba `life is a series of decision making`! Aliendelea kwa kusema hata mtoto mchanga wa siku 1 anafanya maamuzi kila sekunde, maana atatikisa mikono, atakunja ngumi, atalia nk!

  Sasa kitendawili kipo na hii serikali yetu, inaposhindwa kuamua hasa inapokuja kwenye masuala nyeti na yenye ulazima kwa kuinusuru nchi, na kuamua kuwa bubu!

  Matokeo yake, wanananchi wanaamua kusema kwa jazba, na kazi ya serikali inakuwa sasa ni kujibu hoja za wananchi, kitu ambacho kisingekuwepo kabisa!

  Serikali yetu ni MSUKULE!
   
 5. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hatuna haja ya kuhangaika sana kutambua kasoro inayokwamisha maendeleo ya nchi yetu hasa katika awamu hizi mbili. Tatizo kubwa ni kuwa taasisi inayoitwa Public Service(Utumishi wa Umma) imekaribia kufa. Migogoro mingi inayotokea sasa nchini ni matokeo ya utumishi dhaifu ambao umetokana na kufanya mageuzi/maboresho ya haraka yasiyo endana na hali halisi ya Tanzania. Ilani, Sera na Mipango mingi ya Serikali imeshindwa kushamiri kwasababu hiyo kubwa. Bahati mbaya sana. Nasema ni bahati mbaya utumishi wetu kwa miaka hii ya karibuni ulijengwa kwa misingi ya nani anamjua nani na si nani anajua nini. Hebu tazama ile miaka ya akina Paul Rupia, Timoth Apiyo, William Shelukindo, Bernard Mulokozi, na sasa wakati wa akina Philemon Luhanjo, Marten Lumbanga, George Yambesi, Ruth Mollel na Joseph Rugumyamheto. Kuna tofauti kubwa sana. Tukiendelea hivi, bila kujua matarajio ya wananchi ni nini kuna hatari tukaingia kwenye migogoro zaidi. Mliona wenyewe wakati wa bunge la bajeti baadh ya Mawaziri wakikosa majibu na kusingizia kuwa wakati maamuzi fulani yanatolewa walikuwa hawajazaliwa au wakati PM na timu yake wanawasilisha taarifa ya Richmond kusema kuwa Watumishi walitimiza wajibu wao na kwamba wamepewa maonyo Katibu Mkuu Kiongozi akaja na hoja kwamba walikuwa wanakamilisha masuala ya watumishi hao ili watoe adhabu. Hicho ni kielelezo tosha kuwa kuna matatizo makubwa. Rais kama Rais na kama Rais Mtendaji ataendelea kulaumiwa kwa makosa ambayo yangeweza kusahihishwa kama tungekuwa na utumishi makini ambao una reflect mahitaji halisi ya wananchi na si kuhangaika kushughulikia reforms zenye nia ya kuua kabisa utumishi wenyewe.

  Kwa nia njema kabisa ni vema Mhe Rais afahamu kwamba tatizo si sera wala Ilani ya Chama cha Mapinduzi na wala si wanasiasa ambao wana matatizo. Tatizo ni namna mtu alimyemkabidhi jukumu la kusimamia serikali kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma Na. 8 ya 2002 asivyojua nini anatakiwa kufanya. Concentration kubwa sasa imekuwa kamati za maadili, kuandika barua kali za maonyo, kufanya adhoc check ya ujazaji wa OPRAS na mambo madogo madogo badala ya kutazama kwa kina ni nini hasa kama nchi tunatakiwa kufanya katika kusimamia rasilimali na kuziendeleza. Ukienda Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa dakika chache sana, kama unaufahamu utawala utabaini kuwa sehemu ile sasa si chimbuko tena la mawazo ya kujenga utumishi uliotukuka bali ni sehemu ya kuvuruga kila kizuri kilichoanzishwa huko nyuma kwa manufaa ya taifa hili. sijui tunapelekwa wapi. Ushauri: tunaweza sana kumdharau au kudharau matamshi ya mzee John Malecela kuhusu masuala ya uendeshaji wa nchi lakini kwa watu tusioshabikia siasa kulikuwa na haja kwa Rais kuijenga upya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuteua Katibu Mkuu Kiongozi makini. Si vibaya pia hata kama kutakuwa na maelezo matamu kiasi gani kuifuta sheria hiyo mpya ya utumishi wa umma na kuanza upya kwa kutazama mazingira yetu na uhalisia wa Ilani na sera zetu.
   
  Last edited: Aug 8, 2009
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Duh! Mpoki .Tatizo si sera wala ilani ya CCM bali ni mtu aliwekewa na kupewa majukumu lakini mtu huyu kinga yake kubwa ya yeye kuzidi kufanya aendavyo si sheria bali ni CCM bado unasema ?
   
 7. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #7
  Aug 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  It's very easy to decode the time and season Cote d'Ivoire is in presently after the people chased sadist Guei out of office. It's quite easy too to translate the time and season Yugoslavia is in today after the fall of catastrophic Slobodan Milosevic. Unfortunately, it is enigmatic as it is cumbersome to even have a clue as to what phase or stage of development that we are currently going through as a nation. Agreed, so much was destroyed and is still being lost but that is no excuse for the dark ages to be prolonged. It's been forty wasted years and from the recent events that we are witnessing we are likely to waste many more years. Corruption is still transparently and hypocritically compromised. The basics of a developing or developed society are apparently epileptic in supply. The list goes on...
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Maneno mazito haya .Tangia nikujue hapa jamvini ndiyo leo umesema kitu cha maana .Naona mwaka 2010 unakaribia na changes kibao .NI kweli nimekubali usemayo .
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hararaka haraka aina baraka jibu hilo mi nadhani ni kwenye maswali yanao husu maendeleo ya wananchi bila ya kuongezea mengine uliyoyasema yanatosha.

  tatizo la uongozi wa tanzania bado ni mmbovu, wananchi sasa wamewazidi fikra viongozi wetu. hanachosema aki itaji haraka wengi wameshajua mbinu za kuzitatua mfano kwenye ishu za ufisadi, hata kama (najizungumzia mimi) hatujui full scandal na wahusika wenyewe hasa swala la kuwasimamisha kazi na ku-freeze assets za wahusika just as matter of precaution until the final investigation sidhani kama ni la kulichelewesha. swala la kuwapeleka wasimamizi wakuu au hata walete bungeni mikataba yenyewe na risiti zinazoshutumiwa si la kucheleweshwa huku uchunguzi mwingine ukiwa unaendelea.

  kitu kingine amna openness bado katika budget spending hiyo tu ni tosha kumfanya mtu afikrie kutakua na namna na mara nyingi penye usiri basi kuna namna. kama siri yenyewe ni utumiaji wa hela basi namna yenyewe itakua ya kifisdi tu.

  serikali alafu sidhani kama ina jua tanzania hipo wapi na umaskini wetu, na hina lengo gani ya kutatua matatizo hayo. Mimi kwakweli sijui kama mkukuta ni chombo cha kupunguza umaskini au cha kuomba msaada kutumia jina la umaskini. kwa sababu msisitizo mkubwa kwenye site yao ni kuwaelimisha watu. alafu je ukishawaelimisha inakuaje kwani wakulima watalima tu kama mazao haya nunuliwi elimu yako aina faida then regardless ya mbinu mpya ulio mpa. kwa inavyoonekana mbinu za kutatua umaskini hamna. katika mstari huu wa fikra serikali inaoneka aina measurement yakutaka mtanzania wa chini awe na maisha gani given a period of time, using a set of programmes that if forseen properly would improve the situation. Kwa mtaji huo basi umaskini au ku-improve situation ya mtanzania sidhani kama ni priority ya serikali.

  Raisi alaumiwe kwa mengi, yangekua machache ila mengi kwa kujitakia mwenyewe inavyoonekana kaweka marafiki wengi sana kwenye madaraka sasa kukemea uwajibikaji inakua vigumu na kufukuza kazi wanaomletea matatizo inakua vigumu kwa hivo salaba lote linabaki lake mwenyewe uko ni kujitakia nahodha. halafu naona wizara na mawaziri ni wengi mno kiasi kwamba sielewi sehemu zingine za kua na mkuu mmoja zimegawanywa kama mara tatu au hata nne na bado zitakua na manaibu sasa yupi alumiwe kwa lipi iwapo wizara ni nyingi mno, get the priorities right.

  halafu kuna wanaomshauri ki-uchumi hawa ndio nadhani wanaomletea matatizo makubwa na hufanya vitu vya haraka haraka kiasi uondoa hiyo baraka yenyewe na contract za kipuuzi either mwishowe tanzania uishia kulipa mishahara ya kuendeleza hizo sekta walizobinafisha au ku-loose valuable customers in term of bandari and TRC. yaani the whole thing is a joke, yaani hata africa ukitoa nchi kama ya kwetu, Uganda kwa uchoyo wa museveni, zambia na malawi hata viongozi wa frica nchi nyingi wameanza kugundua siku za wizi wa kijinga umeisha watu si wapumbavu vile tena. wengi sasa wako detered in improving the contracts with the west na ku-incourage maendeleo through wasomi wao sisi bado tunaishi in times of 90% favour yakufika sehemu kisa unamjua mtu si kwamba your qualified first. favour is there anywhere in the world but the output is great because a majority are qualified to do what they do and a few are in because of favour. then the situation favours maendeleo.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Baada ya haya maneno ndipo nazidi kujiuliza kwamba hivi JK alijua shida za watanzania ni kitu gani wakati anaomba kura zao ? Did he have a vision this man ?
   
Loading...