Serikali: Jumla ya viwanda 3000 vimejengwa tangu kuanza kwa sera ya viwanda 100 kila mkoa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,444
3,354
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amesema kufuatia agizo la Serikali juu ya ujenzi wa viwanda 100 katika kila Mkoa chini ya usimamizi wa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mpaka sasa jumla ya viwanda 3,000 vimejengwa.
====

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesema Tanzania kuna viwanda vipya 3,000 tangu kuanza kwa mkakati wa kujenga viwanda 100 kila Mkoa.

Waitara ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 12, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti maalum (CHADEMA), Sophia Mwakagenda aliyetaka kujua ni viwanda vingapi vimejengwa tangu kuelezwa mkakati wa ujenzi wa viwanda 100 kila Mkoa, akidai kuwa mkakati huo ni wa kisiasa.

“Tumeshatenga maeneo mbalimbali katika wilaya ya mikoa na mpaka sasa kuna viwanda vipya 3,000. Huu si mkakati wa kisiasa,” amesema Waitara.

Katika swali lake la msingi Mwakagenda alitaka kujua ni waraka gani wa Serikali ulioainisha Tamisemi kujenga viwanda 100 ili kuwapa wananchi rejea ya pamoja na kitaifa

Akijibu swali hilo Waitara amesema, “mkakati huu ni sehemu ya mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kujenga uchumi wa viwanda uliofungamanishwa na maendeleo ya watu.

TAMISEMI imeandaa mwongozo wa kubainisha majukumu ya mikoa na mamlaka za serikali za mitaa katika utekelezaji wa sera ya viwanda. Mkakati huo haupaswi kutenganishwa na mipango mingine ya Serikali inayohamasisha ujenzi wa viwanda nchini.”
 
Kwenye idadi hiyo ya fisiemu hata fundi cherehani naye ni mmiliki kiwanda.
 
Sawa maana ukiwa na kinu cha kutuangia mahindi nacho ni kiwanda
 
Takataka, kama kungelikuwa na viwanda 3000, hakuna kijana mwenye sifa ambaye angeliwa hana employment. Hivi "viwanda" in the real sense of viwanda definition, would have absolved all employable unemployed graduates
 
Mtaani kwetu vipo vitano.Vya cherahani 3 ,kuuza Juice 1 kunyonyoa kuku 1 maendeleo jamani.Unless definition ya kiwanda imebadilika
 
Unajua hawa jamaa huwa wanasema nadhani huwa hawaulizwi? Swali viwanda 3000 vimetoa ajira ngapi?
 
Kausha mshua
Haya Mambo mazuri kuyatamka tu midomoni, njoo kitaa uone tunavyotokwa jasho kwenye meno.

Bongo sikuhizi tunalazimishwa kuishi kwa matumaini tu really life is so hard
 
Back
Top Bottom