Serikali: Jeshi la Polisi kurejesha mfumo wa zamani wa vidhibiti mwendo kwenye mabasi ili kupunguza ajali

"Chuma masaa sana"
"Acha iende"
"Tembea baba"
"Mwaga moto"
.
.
.
.
.
Mwisho wake huwa ni kula mbanga na watu kudanja
 
Kwanini walivitoa vizibiti mwendo walivyoviweka awali? Tukisema mambo yanaenda kwa mihemko, tunaonekana wachonganishi.

Danadana na chenga nyingiii hakuna magoli.
Tatizo la hii nchi ni upigaji tu ndio unaosababisha yote hayo,mkubwa mmoja akiamua kuja na dili la kihuni ili apige hela tayali inakuwa Sheria,kiufupi ni dili za wakubwa ndio zinazoangaliwa na si vinginevyo
 
Jeshi la polisi nchini limesema linafikiria kurejesha mfumo wa zamani wa kufunga Vidhibiti mwendo kwenye mabasi ya abiria ili kupunguza ajali.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani afande Mutafungwa amesema wanakwenda kukutana na wamiliki wa mabasi ili kujadili na kukubaliana juu ya jambo hilo.

Source: ITV habari
Mla rushwa wa kwanza ni polisi Yani wanarudisha ulaji kwa mhalifu namba moja, save this post mtaona kitakachofuata baada ya polisi kurudisha usimamizi wa ving'amuzi.

Kama polisi ndio anakuwa na power ya kukamata na kutoa ushahidi mahakamani then unatarajia hawataweza kula rushwa kupoteza ushahidi wa speed ingali wao ndio Wana final say kwenye upelelezi????

Suala la speed governors lingekuwa chini ya TANROADS wakishirikian na TARURA may be. Ila police HAPANA.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
  1. Huo ni mradi wa mtu, kwanini wasitumie takograph ambayo ni teknolojia ya kisasa inatumia satelite
  2. Kuna ajali wapi zimetokea?
Wakiweka hiyo ulaji utaisha. They did it at TRA walifungwa zile tracker za container wizi umeisha Ila wajanja wanahakikisha wanaizingua Ile system then ngoma inapigwa mkasi fasta then Mambo kama kawaida.
 
Hii serikali ina vichekesho sana, ukienda pale Latra au Sumatra zamani baada ya kazi ya basi lako jeshi la polisi wanakagua hicho kifaa kama umefunga, leo mnakuja na hadithi mpya eti mfumo wa zamani 😃😁😂🤣🤣
Wakati wengine wakienda TEHAMA sisi tunarudi enzi ya macho kwa macho,labda wanajua wanachokifanya! By
 
Wenzetu unaendesha lorry au Bus lina speed limiter ya mile 56 kwa saa

Na mwakani sheria ya kuzifunga gari zote inakuja ( serikali haijajadiliana na mwenye magari )


hapa 🇹🇿 hatutumii vipimo vya maili

na hatutumii sheria za 🇬🇧

diaspora, hebu jiongeze
 
Back
Top Bottom