Serikali jengeni bwawa kubwa eneo kati ya Wilaya ya Chamwino, Kongwa na Mpwapwa

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
3,032
3,478
Kupitia Jukwaa Tukufu,

Nawasilisha ushauri na maoni yangu kupendekeza kwa serikali ya Jamhuri wa Tanzania kujenga bwawa/lambo kubwa linalotokana na uvunaji wa maji ya mvua (rainfall water catchment dam).

katika eneo lolote litakalobainishwa na wataalamu kati ya wilaya za Kongwa, Chamwino na Mpwawa ambako kuna utambarare unaozungukwa na vijilima na makorongo hatarishi pindi mvua inyeshapo.

Bwawa pendekezwa ligawanywe mara mbili kwa matumizi tofauti

1. Sehemu ya kwanza ya lambo hilo itahudumia Kilimo cha mboga mboga, zabibu, alizeti, karanga, korosho na ufugaji wa kisasa wa mifugo ya ng'ombe. mbuzi na kuku (matumizi bora ya maji kwa njia ya dripu yataelekezwa vizuri na watalaamu)

2. Sehemu ya pili itahudumia wananchi kwa ajili ya mapumziko, kuogelea na uvuvi mdogo wa ndoana (maji haya yatatengenezewa mfumo wa kutembea kupitia vyumba maalum ambavyo vitayafanya kujirejesha kwa usafi kama ilivyo kwenye mabwawa ya maji machafu

3. Eneo hilo la bwawa ambalo halitahitaji kuchimba chini ardhini badala yake eneo lenye uwezo wa kupokea maji kutoka pande zote kisha matuta makubwa yenye upana wa kupita gari juu yatajengwa kwa kuzingatia taratibu za ujenzi na uimara wa udongo.

4. Eneo hilo la bwawa linatakiwa kupandwa miti isiyotumia kiwango kikubwa cha maji na rafiki wa utunzaji mazingira.

5. Eneo la bwawa linatakiwa angalau liwe na ukubwa wa kilomita za mraba kati ya (20*25) sawa na 500 Km2 au (20*30) sawa na 600 Km2.

6. Mibuyu yote iliyotamalaki maeneo ya Chamwino, Kongwa na Mpwawa isikatwe ila itunzwe na tunda na magome yatumike kwa matumizi ya binadamu ya asili na ya viwandani kama utengezaji wa sabuni ya mbuyu, nk

Endapo serikali itaridhia na kuweka ksenye mpango iwa utekelezaji manufaa yatakayopatikana itakuwa ni kumbukumbu isiyofutika vizazi na vizazi kwa kuchochea utayari wa kila mtu kuishi na kuwekeza Dodoma maana palipo na maji kwa matumizi ya kibinadamu, mimea, shughuli za kiuchumi na kijamii migogoro hupungua.

Nawasilisha kwa mjadala kutoka kwenye tanuru la fikira chanya.
 
Nawasilisha kwa mjadala kutoka kwenye tanuru la fikira chanya.
Mkuu, na makamanda nao wamo kwenye hilo kundi la tanuru la fikira chanya? 🤔

Btw, 1. Wazo ni zuri. 2. Wasiliana na wawakilishi wa wananchi km wabunge au madiwani ili kupanua wigo wa kuwasilisha fikira yako chanya!
 
Kama itachukua miaka 10 the Blue Nile kujaza lile bwawa la Ethiopia; Dodoma ina mvua za kutosha kujaza bwawa unalopendekeza? Halitaishia kubaki na tope miaka yote bila maji yanayotarajwa? Utafiti makini unatakiwa kufanyika kabla ya kujaribu hii white elephant project.

It is far feasible kuvuta maji L. Tanganyika, the world's second largest fresh water repository, to Dodoma than such kind of trial and error projects.
 
Wazo zuri, nasikitika litabaki humu jamii forum kwa ajil ya kusomwa tu.
 
By the way kumekuwa na mabwawa kadhaa maeneo hayo ni kwa kiwango gani yamekidhi matarajoo? Mtera kwa mfano? Na mengine madogo madogo yapo, yemekidhi mahitaji?
 
Sijasikia mkuu wa kaya akiimiza upandaji wa miti kwa wingi katika mikoa ya kati Tanzania, Wala sijasikia mkuu wa kaya akiwezesha matumizi ya nishati mbadala badala ya kukata kuni.
 
Sijasikia mkuu wa kaya akiimiza upandaji wa miti kwa wingi katika mikoa ya kati Tanzania, Wala sijasikia mkuu wa kaya akiwezesha matumizi ya nishati mbadala badala ya kukata kuni.
Mh mkuu wa Kaya,why not you!
 
Mpango Kama huo ,inawezekana zaismdi njia ya kwenda Mvumi kupitia Ntyuka ,Kuna vilima na mspromoko mengi yanayopitisha maji kutoka maeneo ya Mtera ,Mlowa kwa ujumla Iringa Road .
 
Hiyo mipango yote imo kwenye makabrasha ya sirikali, hakuna jipya wala la ajabu wasilolijua.
 
ushauri mzuri, ila huu ushauri wako ungechukuliwa chapchap kama hii sehemu ingekuwa inapatikana maeneo ya CHATO, KATORO na BUSERESERE!!!.
 
Subiri miradi mikubwa ya kimkakati ikamilike. Vinginevyo tuone uwezekano baada ya 2025
 
Back
Top Bottom