Serikali izuie midahalo ya siasa shuleni, vyuoni’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali izuie midahalo ya siasa shuleni, vyuoni’

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 6, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  TAASISI ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA) imeishauri Serikali kupiga marufuku midahalo inayochangia kukosekana nidhamu na kusababisha uvunjifu wa amani shuleni na vyuoni.

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Thomas Ngawaiya aliliambia gazeti hili ofisini kwake kwamba vipo baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikiingiza siasa mashuleni, hali inayosababisha wanafunzi kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja na kuchangia kiwango cha elimu kushika.

  Alisema midahalo ya siasa ambayo imekuwa ikifanyika vyuoni, demokrasia imekuwa ikitumika vibaya kutokana baadhi ya wachangiaji mada na wasikilizaji kutoa kauli zisizostahili kwa viongozi wa nchi.

  “Wanafunzi wengi wamekuwa wakichanganywa na siasa ambayo imekuwa ikiingizwa mashuleni na baadhi ya vyama, mwanafunzi anatakiwa apate elimu na shule sio sehemu ya siasa, hali hii imechangia hata kiwango cha ufaulishaji kushuka,” alisema Ngawaiya.

  Ngawaiya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, alisema pia demokrasia imekuwa ikitumika vibaya, jambo alilodai kuwa nchi za Magharibi zimekuwa zikitumia fursa hiyo kuhakikisha nchi zenye amani zinaingia katika machafuko.

  Kauli ya Ngawaiya ililenga kongamano la kujadili katiba lililoandaliwa na Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) wiki iliyopita kujadili Katiba ambapo alisema baadhi ya wachangiaji walitumia vibaya demokrasia.
  HABARI LEO
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Sasa watafaulu vipi Civics and GS kwenye lessons za governance and democracy?
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Mimi nimefundishwa SIASA toka darasa la TATU..........no harm in it.....unless hiyo enjioo inataka watoto wetu wasijuwe nini kinafanywa na wajanja wa kisisasa
   
 4. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa kaingia CCM tu ameshafulia kifikra, vyuoni kuna watu wazima wanajua mambo mengi hata kabla ya Midahalo. Aende Uganda kuna mawaziri wanasoma masters na wahadhiri wanaponda serikali na wenyewe wakiwa ndani ya lecture room.
  Mseveni wakati mwingine anatukanwa akiwa anaojiwa kupitia redio na hasemi lolote sembuse bongo.
   
Loading...