Forbes1990
JF-Expert Member
- Apr 14, 2018
- 513
- 989
Nani kakudanganya nauli ya kwenda posta unalipa 400 hata Kama hufiki postaAmandla..........
- Vyumba havitozwi kwa masaa 24. Ingekuwa hivi basi wangekuwa wanatoza kwa masaa. Wanafanya hivi ili kurahisisha hesabu zao maana basi mtu akichukua chumba saa 12 jioni halafu akaondoka saa 12 asubuhi basi angetakiwa kulipa nusu ya pango. Wao wana bei moja ambayo inaanzia muda wao wa kuingia ( kati ya earliest check in na latest check out), ukiingia muda wowote katikati utalipa bei nzima. Ni kama vile ukipanda daladala ya kwenda posta Mwenge hautapunguziwa nauli kwa vile unashuka Morocco. Au kwa vile wamekuambia bei ya chumba ni pamoja na kifungua kinywa basi mpishi awepo wa kukupikia wakati wowote utakapotoka au wakupunguzie bei kufidia mlo kifungua kinywa ambapo haukula.
- Wanafanya hivi ili wawe na muda maalum wa kusafisha vyumba vyote. Wahudumu wanajua kati ya muda fulani na muda fulani ni muda wao kusafisha vyumba, kubadilisha mashuka na mataulo na kuweka sabuni, shampoo na toilet paper mpya. Ikiwa kila mtu atatoka kulingana na muda anaoingia basi wahudumu itabidi wawe kazini kwa masaa 24 ili vyumba visafishwe mara mtu anapotoka. Hii ni ngumu kufanyika.
- Nchi nyingine, breakfast sio sehemu ya gharama ya chumba. Ukitaka kula asubuhi basi unalipa zaidi. Hapa kwetu kuna sehemu hawatoi sabuni ya kuogea, ukitaka kuoga kwa sabuni inabidi uje nayo.
- Nchi nyingine bei ya chumba inategemea siku ya wiki, msimu n.k. Usitegemee bei uliyolipia jumatatu ndio itakuwa hiyo hiyo ijumaa.
- Kwa kifupi upangaji wa bei na masharti ya upangaji wa chumba ni ya mwenye hoteli. Kama hauridhiki, una haki kutafuta sehemu nyingine ambayo itaendana na mahitaji yako au hata unaweza kulala stendi ambako hakuna check out time.
Sent using Jamii Forums mobile app