Serikali iweke utaratibu makampuni yaanzishe vilabu vya michezo-tanzania

mlimbwa1977

Member
Feb 7, 2011
24
0
Miaka kadhaa iliyopita taasisi binafsi na idara za serikali ziliweza kumiliki vilabu vya michezo na kuiwezesha nchi kuwa katika msisimko mzuri kimichezo kuliko ilivyo hivi sasa.Leo hii dunia imebadilika kila kitu kipo,matajiri wameongezeka,masikini pia wameongezeka sana,vijana wasio na ajira wameongezeka sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma.Sehemu iliyowazi na rahisi ya kutengeneza ajira kwa watu wetu ni kupitia michezo ya aina zote.Michezo kama riadha,mpira wa miguu,na mingine mingi pia fani za musiki,maigizo na filamu ndio sehemu pekee kwa sasa inayoweza angalau kupunguza makali ya maisha kwa vijana wetu.

Serikali iweke utaratibu kuhakikisha kuwa kila kampuni inayofanya kazi hapa nchini yenye mtaji kuanzia bilioni 5 hata chini baada ya tathmini kufanyika ni lazima ianzishe na kumiliki klabu/kikundi katika moja ya michezo/fani inayotambulika katika jamii na kushiriki kikamilifu katika mashindano mbalimbali.Mathalani angalia klabu ya Azam inamilikiwa na kampuni,tunataka makambuni kama TIGO,VODACOM,AIRTEL,ZANTEL,TTCL,NBC,CRDB,NMB,TCC,TBL,SERENGETI,MWADUI GOLD MINE,BUZWAGI NK. pamoja na kutoa udhamini, nao wanapaswa kurejeshe faida wanazopata kwa jamii kwa kutoa ajira za moja kwa moja kupitia michezo.Pia halmashauri zote lazima nazo zimiliki vilabu vya michezo na kuviendeleza kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Back
Top Bottom