mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,060
- 4,046
Viti maalum vya wanawake ni utaratibu unaopatikana katika nchi mbalimbali unaolenga kuongeza idadi ya wanawake na makundi yao katika bunge na mabaraza. Kuna nchi nyingi za dunia zilizochukua hatua za kuongeza nafasi za wanawake serikalini kulingana na Mkataba kuhusu ufutaji wa ubaguzi wote wa wanawake (Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women) uliosainiwa na mataifa 189 tangu kuanzishwa mwaka 1981 na kuimarishwa na azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2011.
Kwa tafsiri rahisi kabisa ni mpango mahsudi ambao unalenga kuwajengea uwezo kundi maalumu katika kushika nafasi mbalimbali katika ngazi ya maamuzi na uongozi.
Mpango huo unalenga sana katika kupunguza na kutokomeza dhana za ukandamizaji wa kijinsia na makundi maalumu kwa kuwapa fursa ya kupata nafasi za usawia katika maamuzi mbalimbali na uongozi.
Cha ajabu sasa tunawaona baadhi ya wawakilishi wetu kupitia viti maalumu wanaonekana kama hawajaielewa falsafa ya viti maalumu vizuri, maana mbunge anapata fursa ya kuteuliwa zaidi ya mara mbili lakini bado anakuwa hajajiamini na kujijengea dhana ya ushindani wajimbo.
Nashauri Serilikali iweke muda maalumu na kusiwe na fursa ya kujirudia mara mbili, na muwakilishi atayepata fursa ya kuteuliwa viti maalum afanyiwe majaribio baada ya kumaliza huo muda maalumu ili tuone kama dhana ya kumjenga katika kipindi alichopewa imemkaa? Sina maana ya kuvipinga viti maalumu
Viti Maalumu ni chombo cha kutupa fursa na kujiandaa, sio tubaki hapo hapo. Mbunge kama Benadeta Mshashu amekomaa sasa kiasi kwamba anayeweza kuwania jimbo bila kutegemea viti maalum, hii itasaidia kutoa fursa kwa wanawake wengine mkoa wa Kagera kuwania viti maalum.
Pamoja na kuangalia yote hayo, watanzania tujitathmini tangu tumeanzisha viti maalumu,
Je, lile lengo letu tunafanikiwa?
Je, wawakilishi wa viti maalumu wanaelewa kwa nini wamepata fursa ya kuwawakilisha watu maalumu katika viti hivyo maalumu?