Jimmy George
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 1,733
- 1,648
Habari za asubuhi wana-JF
Ni muda umepita tangu serikali imeanza story ya kutoa ajira, mfano nakumbuka Mhe. Simbachawene akisoma bajeti yake mwezi wa 5 mwaka jana alisema wangetoa ajira kwa waalimu mwezi huo lakini baadae ndipo hadithi zikaanza mara walimu wasubiri bajeti ijayo,kabla bajeti haijaanza kutumika likaja suala la watumishi hewa na ahadi ikawa zoezi litakamilika baada ya miezi miwili. Miezi miwili ilipofika kukawa kimya mpaka pale lilipoletwa suala la vyeti feki ambapo mpaka leo kimya. Mara tukasikia madaktari na manesi wanahitajika wataajiriwa kwa haraka mpaka sasa hakuna kinachoendelea.
Ninachoishauri serikali wawe wawazi na wakweli waseme tu hawana uwezo wa kifedha za kuajiri watu ili tujue kuwa tumepoteza fedha za wazazi kulipa vyuo tulivyosoma,tujue tumepoteza muda kusubiri kitu ambacho hakipo na tujue sisi tumeshindwa kujiongeza kwa kutojiajiri.
Wakisema ukweli itasaidia watu kuwa huru maana kusubiri ajira imekuwa gonjwa la moyo kwa watu,itasaidia watu kubadili mawazo yao kutoka kusubiri ajira hadi kubuni shughuli za kufanya na pia itawasaidia wenyewe kutoulizwa maswali ya ajira yanayowasababishia wawe wanajiumauma maneno.