Serikali iwe makini na makampuni ya kamari kuhusu usalama wa nchi

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Nimepata mashaka sana na mtandao mkubwa wa hadi vijijini wa hizi kampuni za kamari tena zikiwa ni kutoka nje ya nchi.

Makampuni mengi makubwa ya kutoka nje ya nchi hasa nchi zilizoendelea huongozwa na wanajeshi au watu wa usalama kutoka nchi husika. Hii ni kwasababu huwa na ajenda ya biashara lakini pia ajenda ya upelelezi kwa manufaa ya nchi zao.

Sasa hizi mashine za kamari hadi vijijini tena nchi nzima zikiwa na wageni tena wa kutoka nchi moja na magari yao na simu zao za smart phone mimi binafsi naona ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.

Nawaza tu kwa sauti.
 
Uko sahihi 100%.Serikali inapaswsa kuwa smart zaidi.
 
Huu utawala unachotaka ni kodi yao waagize ndege zaidi, usalama wako sio priority saana..
 
ili uendelee kuwa masikini wao wazidi kuwa matajir
C unajua haina maana kuwa na tajiri ikiwa masikini hawapo?
Nchi zote za dunia ya kwanza,zinaishi kwa kudra za masikini ww dunia ya tatu

Halafu acha kuwa na Mawazo Mgando!
Watu wametoka mataifa yaliyoendelea wana shida gani na wewe masikini?wakupeleleze kutaka nini?
 
Nimepata mashaka sana na mtandao mkubwa wa hadi vijijini wa hizi kampuni za kamari tena zikiwa ni kutoka nje ya nchi.

Makampuni mengi makubwa ya kutoka nje ya nchi hasa nchi zilizoendelea huongozwa na wanajeshi au watu wa usalama kutoka nchi husika. Hii ni kwasababu huwa na ajenda ya biashara lakini pia ajenda ya upelelezi kwa manufaa ya nchi zao.

Sasa hizi mashine za kamari hadi vijijini tena nchi nzima zikiwa na wageni tena wa kutoka nchi moja na magari yao na simu zao za smart phone mimi binafsi naona ni hatari kwa usalama wa nchi yetu.

Nawaza tu kwa sauti.
Hoja yako ni njema sana kwa taifa letu.
Unawaza mchina ana cluga anawasha mafuta kilometa 20 kwenda kukusanya elfu 40 maana zile mashine sidhsni zinachukua zaidi ya elfu 60 yani pesa anayoifuata na gharama za usafiri haviingii akilini kabisa
End of the thread.
 
Yale makolokolo yanabeba uchumi wa vijana wengi sana.
Huku TEMEKE vijana wengi hufanya kazi na pesa kuzipeleka kwa Wachina.
Usichukulie simple, machine moja kwa siku hukusanya mpaka laki tatu.
Akizungukia mitaa 3 tu ana million ya bure.
Niliwahi kuwa addicted na zile machines, naliwa mpaka laki mbili kwa siku, Namshukuru Mungu sasa nimeacha. Hata bure sichezi.
Wafukuzwe nchini kwa ustawi wa vijana kiakili na kimaendeleo
 
Dah hiyo laki mbili ungeweka single bet ya uhakika ungeenda hivyo mdogo mdogo ungekuta sasa ni tajiri. Hicho kimashine nakumbuka niliona watu wakicheza nikaona isiwe tabu na mimi acha nifurahie mchezo nikaweka coins tatu za 200 kila moja ile naweka start tu kitu kikaniletea coins 90 nakumbuka kilichofuata niliagiza niletewe mfuko mkubwa wa rambo.
 
Una bahati.
Mimi nimeliwa kama 1 million kwa hizi machine.
Nimewahi kula pesa ila negative kwangu nadhani inatimia M.
Kuna wakati nilikuwa napiga pesa sana kazini. Kutoka na laki tatu, moja au mbili per day ilikuwa normal.
Sasa nilikuwa natenga kiasi ili nichezee kamari.
Sasa hivi marupurupu yanakuja kwa mbinde sana ila ndo mda nafanya vimaendeleo
 
Unawaza mchina ana cluga anawasha mafuta kilometa 20 kwenda kukusanya elfu 40 maana zile mashine sidhsni zinachukua zaidi ya elfu 60 yani pesa anayoifuata na gharama za usafiri haviingii akilini kabisa
Sio kweli mkuu,kuhusu kluger it's ok,mchina hupakua tsh 400,000-800,000 (kete 2000-4000+ kete 1@200 tsh) kila baada ya 2days kwa slot machine/bonanza moja,jamaa wanaua nguvu kazi ya taifa katika kiwango cha 100% huku wao na mataifa yao wakineemeka.
Vijana now hawalimi,wamekua na rottery mind,wakifanya mishe za kutwa jioni wanaenda kukabizi pesa yote kwa kamari za mchina..too bad
 
Mpaka siku sisi Tanzania kama taifa tugundue china ni jini subiani la kutunyonya damu tutakuwa tumesha chelewa sana. Hata ulinzi wetu ni kama nusu rehani mchina.
 
Huwa siamini pamoja na umakini wa serikali yetu katika mambo mengi, imekuaje haioni kuwa mashine za kamali hadi vijijini huko ndani kabisa ni tatizo. Wenyeviti wa vijiji huko mliko, madiwani, wabunge mpo? Kamali haifanani na hapa kazi tu!
 
Back
Top Bottom