Serikali iwe macho na matumizi ya fedha za Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

Jul 18, 2020
9
15
SERIKALI IWE MACHO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA

Nimekua nikifuatilia yanayoendelea katika mitandao ya kijamii, na vikao mbalimbali ya vyama vya wafanyakazi nchini, leo nitajikita kuongelea Chama cha Walimu Tanzania (CWT)

Chama cha walimu Tanzania ni chama wafanyakazi ambacho kina idadi kubwa ya walimu ,kina jumla ya wachangiaji Laki 240000 + kwa mujibu wa TAKWIMU ZAO kabla ya MEI mosi 2021

kina kadiliwa kinakusanya sio chini ya bilion tatu kila mwezi fedha za 2% kwa mujibu wa katiba yao, ni fedha nyingi sana

changamoto kubwa ipo katika matumizi ya fedha hizo, serikali muda wa kubadilisha sheria umefika MKAGUZI MKUU wa serikali awe anakagua fedha za vyama vya wafanyakazi kila mwaka kama wanavyofanya kwa vyama vya siasa ambavyo mapato yao hayafiki hata nusu ya chama cha walimu Tanzania.

Serikali ikiendelea kukaa kimya na kutoyafanyia kazi madai ya walimu juu ya matumizi ya fedha za chama chao ipo siku watakumbuka ukumbusho huu, ipo siku isio na jina atakuja mzalendo atalisimamia ili na wapo viongozi watafungwa, fedha ya UMMA lazima ilindwe, tumeona baadhi ya viongozi wa serikali wakiwasifia viongozi wa kitaifa CWT kuna muda tukiwa na akili timamu tunajiuliza anaujua ukweli au amepotoshwa.

SISI WANACHAMA HATUTAKI KUSEMA NANI ANAFANYA NINI CWT, NANI MWIZI TUNACHOITAKA SERIKALI NI KUPELEKA KIKOSI KAZI CHA WAADILIFU NA WAZUNGUKE WILAYA ZOTE WATAPATA UKWELI, MUDA NDIO MKWELI

Kuna wilaya mpaka sasa hawajapata tisheti baadhi ya vituo, kofia mpaka sasa hazijafika kwa idadi ya wanaochangia ,mkono wa kwa heri kwa wastahafu tokea mwaka 2018 bado walimu hawajapata.

Ushauri kwa viongozi wa serikali hata kama wale viongozi wa kitaifa top five(CWT) ni marafiki zao unafaidika nao kwa namna moja au nyingine usikurupuke kumtetea jukwaani utapata aibu huko mbele ya safari, wanachama wanajua yanayoendelea.

WANACHAMA WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA SIO WAJINGA
 
Mimi likifika suala la walimu. Kazi iendelee ni wanafiki sana.
 
Mkisha ruhusu serikali "kuingilia" trade union kwa namna hii, msije piga kelele pale pia itapongilia katika maswala mengine katika kikundi chenu kama kuteua viongozi!

Ni kikundi chenu, mnashindwaje kuwajibishana?
 
Ninyi walimu ni wanafiki na msiojielewa, Mkae mkijua kuwa serikali katika kufanya yote inachofanya ni kupandikiza mtu ambaye ana influence in such away kwamba wanufaika(Serikali) inapotaka kufanya jambo lake kuwarubuni walimu njia rahisi ni thru yule Pandikizi ambaye ndio kiongozi wenu.

Kwa kifupi ninyi huwa hamna kiongozi isipokuwa kiongozi wenu anakuwa planted na wanufaika (Serikali) kwa manufaa yake. msipong'amua hili hamtakaa mfanikiwe Ng'oooo!

Kwa kifupi Serikali ndiye Mchawi wenu
 
Kabisa, hivi wewe unaona ni sawa mwalimu mzima kuanzisha thread kwa ajili ya kofia na tshirt, ndio maana wakati wa uchaguzi mkipewa wali na viposho kidogo tu, mnasaidia kuiba kura.
Kwa akili yako ndogo umefikiria kirahisi,tishirt za chama cha walimu ni zaidi ya bilion tatu ,kofia ni milioni miatisa,mkono wa kwa heri zaidi ya bilion mbili kama hujui kaa ujifunze
 
Mkisha ruhusu serikali "kuingilia" trade union kwa namna hii, msije piga kelele pale pia itapongilia katika maswala mengine katika kikundi chenu kama kuteua viongozi!


Ni kikundi chenu, mnashindwaje kuwajibishana?
hakuna chombo kisichoingiliwa na serikali kwa manufaa ya UMMA ndio maana mpaka vyama vya siasa vinaingia hususani mambo yanayohusu fedha
 
Ninyi walimu ni wanafiki na msiojielewa, Mkae mkijua kuwa serikali katika kufanya yote inachofanya ni kupandikiza mtu ambaye ana influence in such away kwamba wanufaika(Serikali) inapotaka kufanya jambo lake kuwarubuni walimu njia rahisi ni thru yule Pandikizi ambaye ndio kiongozi wenu. Kwa kifupi ninyi huwa hamna kiongozi isipokuwa kiongozi wenu anakuwa planted na wanufaika (Serikali) kwa manufaa yake. msipong'amua hili hamtakaa mfanikiwe Ng'oooo!

Kwa kifupi Serikali ndiye Mchawi wenu
kupandikiza watu hata ma Rais wa nchi wanapandikizwa ilo halizuiriki ,cha msingi baada ya sheria zifuatwe
 
hakuna chombo kisichoingiliwa na serikali kwa manufaa ya UMMA ndio maana mpaka vyama vya siasa vinaingia hususani mambo yanayohusu fedha
Hiki ni tawi la chama cha siasa na ni wanufaika wa michango inayokatwa Kwa wafanyakazi... Najaribu kuwaza !!
 
Tukubaliane kwanza,

Hizo fedha ni za Serikali au siyo za Serikali........!
 
Kabisa, hivi wewe unaona ni sawa mwalimu mzima kuanzisha thread kwa ajili ya kofia na tshirt, ndio maana wakati wa uchaguzi mkipewa wali na viposho kidogo tu, mnasaidia kuiba kura.
Kagusia na mkono wa kwaheri kwa wastaafu, unapojenga hoja kuwa objective
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom