‘Serikali iwataje watesaji wa Kibanda, Ulimboka’ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

‘Serikali iwataje watesaji wa Kibanda, Ulimboka’

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Mar 22, 2013.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2013
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,015
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  PAMOJA na vyombo vya dola kupiga chenga katika kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka na Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006), Absalom Kibanda, serikali imetakiwa iwataje wahusika na kuwachukulia hatua.

  Kauli hiyo imetolewa na baadhi ya maofisa wastaafu katika vyombo mbalimbali vya dola, waliozungumza na gazeti hili jana, wakidai kwa sasa vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa shinikizo la kisiasa.


  Maofisa hao ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walidai kuwa inashangaza kuona idara nyeti kama ya usalama wa taifa na jeshi la polisi watendaji wake wanatajwa kuhusika katika matukio hayo ya utesaji raia lakini hawakamatwi kuhojiwa na kuchukuliwa hatua.


  Walisema kuwa badala yake umegeuzwa kuwa mchezo wa kufifisha na kuwahamisha watu kwenye hoja hizo kwa kuibua matukio mengine ambayo yanavaliwa njuga kwa nguvu nyingi pasipo sababu.


  Afisa mmoja mstaaafu alitolea mfano suala la kutekwa, kuteswa kwa Dk. Ulimboka akisema kuwa alishangazwa na kauli ya Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, kudai kwamba suala hi siri ya taifa.


  “Ninashindwa kuelewa kwa nini polisi au vyombo vyovyote vya usalama havijamkamata wala kumhoji ofisa wa Ikulu, Ramadhan Ighondu, aliyetajwa kuhusika na tukio la Dk. Ulimboka,” alisema.


  Aliongeza kuwa alichokisema akiwa mahututi hakitofautiani na alichokisema baada ya kupona, lakini akahoji kwa nini polisi hawakuwahi kumhoji Ighondu badala yake serikali ilikimbilia kulifungia gazeti la MwanaHalisi lililoripoti taarifa hiyo.


  “Huu ni mkakati wa makusudi wa kutopeleleza kitu kinachojulikana, kwani wenye jukumu hili wanawajua watesaji au wanajua sakata lote nyuma ya hili suala ndiyo maana hawapelelezi,” alisema.


  Ofisa mwingine alidai kuwa matukio hayo likiwemo la Kibanda na mengine yanatoa tafsiri kuwa serikali haiwajibiki.

  Alisema watu waache kusingizia kuwa nchi imeharibika, bali inaharibiwa na serikali kwa kutowajibika.
  Alisema upelelezi matukio ya Ulimboka, Mwangosi na Kibanda unazidi kusuasua huku vyombo hivyo vikiwa vimeibua suala jipya la video ya Wilfred Lwakatare na kuhamisha mjadala wa wananchi.

  “Tukio la Mwangosi picha zinaonyesha wazi alivyouawa, lakini pamoja na wale waliomuua kuonekana, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na ninyi waandishi mmeacha kuandika, hivyo hivyo suala la Kibanda limenyamaziwa sasa, mnajihusisha na Lwakatare,” alisema ofisa huyo.


  Usiku wa kuamkia Juni 27, 2012, watu wasiojulikana walimteka kisha kumpiga na kumjeruhi vibaya Dk. Ulimboka.

  Pamoja na polisi kudai kuunda kamati ya uchunguzi, baadaye walitupiana mpira wakidai hakuna kamati kama hiyo huku Ulimboka mwenyewe kutowahi kuhojiwa hadi leo.

  Kibanda naye alitekwa na kuteswa Machi 6, mwaka huu, lakini hadi leo hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo wakati video ya Lwakatare iliyoonekana mtandaoni Machi 11, polisi wamekwishachunguza na kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani.


  Akizungumzia uharaka huo wa kumkamata kiongozi huyo wa CHADEMA, ofisa maarufu mstaafu wa idara ya usalama wa taifa alidai kuwa suala hilo linapoteza heshima ya serikali kwani sasa inaonekana kulinda wauaji wanaoua wanaharakati au watetezi wengine.

  ‘Serikali iwataje watesaji wa Kibanda, Ulimboka’
   
 2. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 3,134
  Likes Received: 1,608
  Trophy Points: 280
  Nimeanza kuhisi mauaji ya watu na utesaji wakiusishwa TISS na POLISI yana mkono wa JK.
   
 3. T

  Tabby JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2013
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 10,157
  Likes Received: 6,093
  Trophy Points: 280
  Kinachonipa shida ni serikali kukaa kimya wakati mara kwa mara kumekuwa na taarifa za awali zinatolewa juu ya kuwepo kwa mipango dharimu kwa wa TZ ama makundi ya wa tZ mbali mbali. Taarifa hizi zimekuwa zikithibitishwa na matukio halisi tena baada ya muda si mrefu sana. Leo tumesikia tena taarifa kuwa maisha ya Zito yako hatarini.

  Likimpata Zitto si ajabu tena ikatengenezwa cnema nyingine ya Rwakatare ili kudivert attention na kudhoofisha Chadema. The Govt is not serious.

  Serikali yoyte makini haidharau taarifa ila hainamini kila taarifa. Ilipaswa kushughulika na hzi taarifa kabla hayajawa.

  Serikali ya Tanzania inafanya nini katika kulinda haki za kuishi na usalama wa wananchi wake? Tumeshuhudia wimbi kubwa la harifu za aina mbali mbali lakini serikali imekaa kimya na wala hakuna dalili zozote za kuzuia hizo harifu zisitokee ama kufuatilia na kuchukua hatua thabiti ambazo zingeweza kupelekea ukomo ama upungufu wa mambo haya.

  Ukimya huu wa seriali unatafsiriwa ama ni "kutokujali matatizo ama maisha ya watz;, Udhaifu wa kiweledi na kitechnologia upande wa seriakli kiasi sasa inazidiwa nguvu na maarifa na makundi ya kiharifu; ama serikali kwa makusudi na malengo inayoyajua yenyewe imeamua ama kushiriki moja kwa moja kwenye uharifu ama kutumia makundi ya kiharifu katika kuhujumu haki na maisha ya watazania", ndiyo sababu haijishughulishi kuzuia ama kukomesha tabu hizi.

  Ninachoshindwa kujua ni kiini cha kigugumizi hiki cha serikali kutafuta ukweli wa matukio toka kwa hawa wanaoyajua kabla.

  Kama serikliali imekuwa ikijua haya mapema na kwa makusudi ama udhaifu haina cha kufanya, basi inatoa mwanya kwetu wananchi kutafsiri vile tuonavyo.

  Lakini hatutaendelea kuacha serikali iendeleze mtindo wake wa kutujengea mazingira ya kuchukiana, na kuumizana sisi wenyewe kwa maslahi binafsi ya watawala.

  1. Serikali inatakiwa itoe tamko na kuwaomba msamaha Watz kwa uzembe wake wa makusudi ama wa udhaifu uliopelekea maafa makubwa kisha ichukue hatua za haki na za dhati.

  2. Ichukue hatua madhubuti za kukomesha uharamia wa kihuni huu unaoendelea na kupelekea kuonyesha kwamba TZ ni shamba la mwehu lisilo na mwenyewe.

  3. Kama haina ujasiri ama uwezo wa kuchukua hatua yoyote ya kweli, haki na dhati, ama kwa sababu ya uwezo mdogo, iko busy na propanganda na haina time na mambo ya wananchi, ama woga wa kujikana ama kujipinga, iachie madaraka kabla nchi haijageuka shamba la wanyama pori.
   
 4. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Tukiwa wazalendo wa kweli na hasa wale wanaoshabikia ulaji leo kwani wakisubiri mpaka kesho watajutia muda waliopoteza.
  Pia tuwalaumu viongozi wetu wastaafu ambao wamefunga midomo na wanashindwa kukemea haya.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2013
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,664
  Likes Received: 5,573
  Trophy Points: 280
  Wakuu mnataka serikali yetu dhaifu ijiumbue yenyewe?
   
 6. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #6
  Mar 22, 2013
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 8,685
  Likes Received: 8,405
  Trophy Points: 280
  Mbona hilo jambo liko wazi kwa sasa.

  Na kama Salva Rweyemamu atakuwa na ujasiri wa kulikanusha itabidi tu aulizwe swali moja tu jepesi kama Jeshi la Polisi limeshindwa wajibu wake no. 1 ambao ni kulinda raia wake na mali zao kutokana na matokeo mengi ya kuuawa raia wengi wasio na hatia na matokeo ya kutekwa watu bila wahusika kukamatwa na kama Rais anashikwa na kigugumizi kumfukuza kazi IGP Mwema je huo haujawa tu ni ushahidi tosha kuwa kwa mambo yanayofanyika ya kutekwa kwa raia kwa njia za utatanishi mambo hayo huwa yanafanywa na vyombo vya usalama kwa baraka za mkuu wa nchi mwenyewe??!!
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,052
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Hao watesaji wa Ulimboka mwambieni Ulimboka mwenyewe awataje.

  Ya Kibanda watuhumiwa wapo ndani subiri mwisho usikie kama guilty/innocent.
   
 8. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #8
  Mar 22, 2013
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 999
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MIMI NAONA MAMBO MENGINE YANASUBIRI 2016, KWA MAANA SERKALI ILIYOPO MADARAKANI HAIWEZI KUJITAJA NA KUJICHUKULIA HATUA YENEWE KWA KUTESA NA KUUWA WATU WAKE.

  JAMBO LA MSINGI TUSIYASAHAU MUDA UKIFIKA TUKUMBUSHANE ILI WAKINA Ramadhan Ighondu wafikishwe MAHAKAMANI AU WAPOTEE KAMA BALALI.
   
 9. C

  Chibolo JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2013
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 3,134
  Likes Received: 1,608
  Trophy Points: 280
  kweli kabisa kama na jk anahusika hali ya nchi iko hatarini zaidiya tunavyofikiria.
   
 10. a

  artorius JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2013
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanahalisi:Aliyeteka Ulimboka huyu hapa,
  Ni Ramadhani Ighondu wa usalama wa taifa.Kilichofuata baada ya hapo kila mtu anakijua.
   
Loading...