Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema) Phillemon Ndesamburo amesema kwamba wanywaji pombe ni watu wazuri kwa serikali kwa kuwa ndio wachangiaji wakuu wa uchumi.
Akichangia bajeti hiyo, Mbunge wa Moshi (Chadema), Phillemon Ndesamburo alisema tangu azaliwe bajeti
zote zinaongeza kodi kwenye pombe na sigara bila kuangalia maeneo mengine ya kutoza kodi.
''Watu wamesifia sana TRA, wanafanya kazi nzuri wanaingiza fedha nzuri. Mimi nasema hapana, ningesema wangetufungulia njia mbadala, njia nyingine nyingi, ningesema wamefanya kazi nzuri,'' alisema Ndesamburo na kuongeza:
''Wanywaji pombe nadhani ni watu wazuri kwa serikali ndio wachangiaji wakuu wa uchumi, siyo hiyo tu tunawafanya wananchi wanakuwa mabega kwa kurudi kwenye piwa (gongo) na hii inakuwa gharama nyingine kwa hospitali kuwahudumia.''
Ndesamburo alisema, hakuna chanzo kipya kilichobuniwa na TRA kupanua wigo wa kodi, lakini wamekuwa wakiendelea kumkamua Mtanzania ambaye amechoka.
Kuhusu kilimo, Ndesamburo alisema sio kila mtu ni mkulima na kutahadharisha kwmba, serikali isifanye makosa kama ilivyofanya kwa wafanyabiashara kuwaita wote Wamachinga.