Serikali iwapeleke A Level shule za vipaji maalumu wanafunzi waliopata division one kali kutoka shule za kata kwanza baadae za private

Cobra70

Senior Member
Jan 2, 2020
167
363
Namaanisha mwanafunzi mwenye division one kutoka shule ya kata ni hazina ya taifa kama ataendelezwa kikamilifu.

Hii ni kwa sababu anaweza kutumia mazingira magumu kama changamoto na changamoto hiyo anaitatua kikamilifu na kwa usahihi sana hivyo IQ yake ni kubwa mno tofauti na wa mazingira mazuri.

Wa mazingira mazuri ukimuweka magumu anaharibu kama si kukimbia. Watu hawa si wa kutegemea sana.
 
Elimu ya Tanzania haiko kumsaidia masikini.

Mtoto anapata division 1 shule ya kata ambayo haina walimu wala vifaa vya kutosha kujifunzia, alafu mwingine anapata division 1 feza boys, cha ajabu huyu wa fedha boys ambae analipa ada 9m anapendelewa kupelekwa shule nzuri ya serikali na yule wa shule ya kata anabakia shule za kata, unajiuliza hizi ni akili au mavi?

Huyu wa feza atapelekwa shule zinazoitwa za vipaji maalumu(siku hizi karibu wanafunzi elfu 20 wanapata 1.7, sijui ndio tanzania imekuaa vipaji vingi), alafu yule wa shule ya kata anabakia shule ya kata, unajiuliza kati ya huyu wa fedha na huyu wa kata kama vi kipaji nani ana kipaji? Cha ajabu anaonekana wa feza ndie mwenye kipaji.

Mfumo wa elimu wa nji hii hauwezi kutufikisha mahala. Unakuta jambo dogo tu linatushinda tunaita vijana wadogo kabisa kutoka ulaya kuja kutusaidia huku tumejaza division 1.7 na division 1.3 za kutosha nchi hii za vipaji.
 
Nakubali mkuu, binafsi nawa-appriciate sana madogo waliotoka shule za kata.. Kama hv majuzi baada ya kutoka results niliamgalia matokeo ya shule moja ya kata (Kata niliyopangiwa field kipindi fulani.) Kuna dogo wa pekee kapiga 1.12 yaan nimependa Huyo dogo, unaamini kabisa kuna madogo sana vipaji.. Wenzie in divsn 3 na 4 ambao ni wachache na zero kama zote
 
Wengi wao wanarudi huko huko st. Mtoto wa Feza umepeleka Milambo Sec. anapata zero yake mapema kabla ya mtihani wa form six.
 
Back
Top Bottom