Serikali iwape SUMA JKT kazi ya kununua na kuuza sukari yote ndani na nje ya nchi

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
SUMA JKT ni shirika la umma ambalo liko chini ya Jeshi la kujenga Taifa.Nashauri lipewe kazi ya kununua sukari yote ya viwanda vya sukari nchini na wawe ndio waagizaji pekee wa sukari yote inayohitajhika nchini na wawe ndio wasambazaji na wauzaji wa jumla nchi nzima wa hiyo sukari.

Faida ya kuwatumia SUMA JKT ni kuwa nchi itakuwa na uwezo wa kuwa na depot za kusambazia sukari nchi nzima na spidi yao ya usambazaji ni ya kijeshi hivyo ni rahisi kuifikisha sukari kila kona ya nchi.Na pia itakuwa rahisi kujua mahitaji halisi ya nchi na uzalishaji halisi ukoje bila kudanganywa iwe na viwanda au wa wafanyabiashara au wataalamu koko wa takwimu na vibaraka wao wachumi koko ambao hutumia elimu zao kuidanganya serikali kwa takwimu pofu na potofu kwa maslahi ya mabepari uchwara.

Kutumia hilo shirika pia kutakuza ajira

yehodaya123@gmail.com
 
Pumba kwa kiwango cha lami

Sehemu zote kwenye biashara au uzalishaji ambako serikali imwekeza pesa zake isimamie yenyewe isiwaachie wazalishaji au wafanyabiashara pekee.

serikali inatoa ruzuku kwenye sukari kama hujui.Pesa zetu za kodi zinatumika kwenye kutoa hiyo ruzuku.Sasa kwa nini wafanyabiashara walipa kodi kwa kushikilia sukari yao ambayo kodi zao za ruzuku zimetumika kwenye hiyo sukari?.

Serikali isimamie yenyewe kupitia SUMA JKT wawe ndio pekee wa kushughulikia hiyo biashara kisitokee kinyago kikasema ohhh sijui biashara huria,biashara huria huwa haina ruzuku ya serikali.Sukari ina ruzuku ya serikali

Magufuli kabidhi Jeshi hiyo biashara.Vinginevyo futa ruzuku ibakie biashara huria.

Pesa zetu za kodi ziko kwenye sukari hatuwezi chezewa na hao maruhuni wafanya biashara
 
Hahhaahahahaha huyu jamaa anajitahidi kutoa thread humu ndani sijui kama huwa anatafakari japo kidogo kabla ya ku click send button. Kuwapa SUMA JKT sio suruhisho la tatizo hilo, hapa inatakiwa kuzuia ugonjwa wenyewe from the root sio dalili za ugonjwa. Ni matumaini yangu mtoa mada ni mmoja wanaoamini kwamba kuna mtu kakutwa na tani 4900 ghalani.
Hawa jamaa kwa sasa wametupatia kweli, wanatupa wananchi cha kushangilia then wanapitia back channels kupiga as usual. Wananchi tuamke jamani huku chini hali ni mbaya mnoo tofauti na watu wanavyodhania.
 
SUMA JKT ni shirika la umma ambalo liko chini ya Jeshi la kujenga Taifa.Nashauri lipewe kazi ya kununua sukari yote ya viwanda vya sukari nchini na wawe ndio waagizaji pekee wa sukari yote inayohitajhika nchini na wawe ndio wasambazaji na wauzaji wa jumla nchi nzima wa hiyo sukari.

Faida ya kuwatumia SUMA JKT ni kuwa nchi itakuwa na uwezo wa kuwa na depot za kusambazia sukari nchi nzima na spidi yao ya usambazaji ni ya kijeshi hivyo ni rahisi kuifikisha sukari kila kona ya nchi.Na pia itakuwa rahisi kujua mahitaji halisi ya nchi na uzalishaji halisi ukoje bila kudanganywa iwe na viwanda au wa wafanyabiashara au wataalamu koko wa takwimu na vibaraka wao wachumi koko ambao hutumia elimu zao kuidanganya serikali kwa takwimu pofu na potofu kwa maslahi ya mabepari uchwara.

Kutumia hilo shirika pia kutakuza ajira

yehodaya123@gmail.com

Kwi kwi kwi kwiiiii eti hivi ndio vichwa vya kumshauri Magu!!!! Hahahahahahahaha
 
Wewe ndio unaongea ujinga kweli, hii ni nchi ya kijeshi? Uchumi una kanuni zake na hao wanajeshi wamefundishwa kuua. Mpaka leo hii nchi yetu ni maskini ni kipi kilichowashinda hao suma JKT kuifanya nchi iwe tajiri? Leo hii wanajeshi wanalalamika kukosa nyumba za kuishi mpaka wengine tunaishi nao huku mtaani kwenye nyumba za kupanga, hao Suma Jkt wako wapi? Kutumia nguvu bila akili ni kama kujichoresha ndugu yangu. Hao wenyewe suma JKT hata uniform tu zimechakaa sembuse kusimamia sukari ambalo ni jambo la kiuchumi? Nenda kaangalie hayo magari yao na vitendea kazi vyao vilivyo vichovu, ushindwe kusimamia cha kwako ukaweze vya wenzio waliojinyima mpaka kufikia hapo walipo? Wangalau ningekuelewa kama ungesema yaanzishwe mashamba makubwa ya miwa na kujengwa viwanda vya sukari ambapo hao suma Jkt ndio watakuwa wazalishaji, washindane na soko na sio kuleta vitisho vya kijeshi kwenye mali za watu.
 
Jifunze kupitia RTC ndio uje upya. Hii haina mashiko.
 
Kuwapa SUMA JKT sio suruhisho la tatizo hilo, hapa inatakiwa kuzuia ugonjwa wenyewe from the root sio dalili za ugonjwa. .

SUMA JKT waweza pewa hata mashamba ya miwa wazalishe wenyewe wana Capacity kubwa katika swala la kilimo.Waweza pewa JKT na Magereza kazi ya kuzalisha miwa na kuuzia viwanda na kuinunua sukari yote na kuisambaza.Kama uzalishaji wa miwa unasumbua kazi hiyo ikabidhiwe magereza na JKT hakuna haja ya kuleta mwekezaji wa mashamba makubwa ya miwa wapewe.Wataajiri wasomi kibao toka VYUO KAMA SOKOINE NK
 
Huyu mtoa mada kaleta utumbo wa mbwa jamvini,ni mpaka serikali itakaporudi katika misingi ya kuonhoza nchi,haiwezekani nchi iongozwe na mtu mmoja na mawaziri wanabaki hawana hata instrument,lazima nchi ikushinde,huwezi kuwa kila mahali wakati wote,suala la vibali vya kuagiza sukari alilihamishia ofisini kwake na akasema atakuwa anasaini yeye mwenyewe,sasa uhaba wa sukari umetokea,ofisi ya Mkuu inataka kutuambia inafeli?kama ofisi ya Mkuu inafeli nyingine je?hao suma so lwafungue mashamba ya miwa na kiwanda?
 
Wewe ndio unaongea ujinga kweli, hii ni nchi ya kijeshi? Uchumi una kanuni zake na hao wanajeshi wamefundishwa kuua.

Jeshi la sasa lina wasomi ambao wengine hata uraiani huwezi kuwapata.Jeshi letu lina kila aina ya wasomi.Ukienda madaktari wapo,ukitafuta mainjinia wapo,wahasibu,wapo,wachumi wapo tena wengi tu.Kazi ya jeshi pamoja na kazi zingine ni kuwa na wapiganaji wachumi ambao kazi yao ni kupigana na kuulia mbali wahujumu uchumi kwa kutumia elimu ya uchumi waliyopata.Vita si bunduki tu mhuni aweza tumia hata sukari kujaribu kuiangusha serikali au kutaka serikali ichukiwe na wananchi.Jeshi linao wapiganaji wa kila eneo.

Hao wahujumu uchumi kama wanadhani wanaweza kuwatumia wachumi koko maruhuni wa mitaani kuua uchumi wa Tanzania wanaota.WATAONDOKA WAO NA WATAPOTEZA BIASHARA ZAO TANZANIA ZITAKUFA KIFO CHA MENDE.
Kama wanatangaza vita ya kiuchumi na serikali wajiandae kufa kiuchumi wao na watajuta kwa nini wamewekeza Tanzania.Kama ni biashara wafanye lakini uhuni wowote ule kupambana na serrikali hautavumiliwa wala kukubalika.
 
SUMA JKT ni shirika la umma ambalo liko chini ya Jeshi la kujenga Taifa.Nashauri lipewe kazi ya kununua sukari yote ya viwanda vya sukari nchini na wawe ndio waagizaji pekee wa sukari yote inayohitajhika nchini na wawe ndio wasambazaji na wauzaji wa jumla nchi nzima wa hiyo sukari.

Faida ya kuwatumia SUMA JKT ni kuwa nchi itakuwa na uwezo wa kuwa na depot za kusambazia sukari nchi nzima na spidi yao ya usambazaji ni ya kijeshi hivyo ni rahisi kuifikisha sukari kila kona ya nchi.Na pia itakuwa rahisi kujua mahitaji halisi ya nchi na uzalishaji halisi ukoje bila kudanganywa iwe na viwanda au wa wafanyabiashara au wataalamu koko wa takwimu na vibaraka wao wachumi koko ambao hutumia elimu zao kuidanganya serikali kwa takwimu pofu na potofu kwa maslahi ya mabepari uchwara.

Kutumia hilo shirika pia kutakuza ajira

yehodaya123@gmail.com
Wazo ni zuri lakini hofu yangu,
mara nyingi inakua ni ngumu sana kufuatilia kunapotokea uozo majeshini,jeshini ni sehemu tofauti kidogo,yani panapo kua na uozo hatujui na panapo kua hakuna uozo hatujui,kila siku unasikia habar za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya ukaguzi,ulishawah sikia habar ya hasabu za jeshi?
 
SUMA JKT waweza pewa hata mashamba ya miwa wazalishe wenyewe wana Capacity kubwa katika swala la kilimo.Waweza pewa JKT na Magereza kazi ya kuzalisha miwa na kuuzia viwanda na kuinunua sukari yote na kuisambaza.Kama uzalishaji wa miwa unasumbua kazi hiyo ikabidhiwe magereza na JKT hakuna haja ya kuleta mwekezaji wa mashamba makubwa ya miwa wapewe.Wataajiri wasomi kibao toka VYUO KAMA SOKOINE NK

Kada kama wewe ni mmoja wa Think Tank ya Mkulu basi naomba tender your letter of resignation faster. Sababu kuna kitu ambacho hamjakiona ila mmekiona mnaogopa kumwambia Mkulu.. Hizi issues za UJAMAA zishapitwa na wakati huu ni muda wa kuachia soko ndo liamue ni nini kinatakiwa kufanyika. Ni lazima tuwe na strategy za long run and short run. Sasa hiyo unayoizungumzia ya kuanzisha kilimo cha miwa hao SuMaJkt ni suala la muda mrefu. Swali la msingi Je wananchi waendelee kuumia bei huku wakisubiria miwa ya jkt iwe tayari kwa uzalishaji?
 
Hizi issues za UJAMAA zishapitwa na wakati huu ni muda wa kuachia soko ndo liamue ni nini kinatakiwa kufanyika. Ni lazima tuwe na strategy za long run and short run

Kama umesoma utakuwa ulikariri ulichosoma.

Ulaya kuna soko huria? nani kakudanganya.Bei za vitu vyetu kama pamba,kahawa,korosho nk tukiwauzia wao ndio wanapanga bei wanunue bei gani sio sisi wazalishaji lakini vitu vyao wakituuzia wao ndio wanapanga watuuzie bei gani!!!

Umejaa ukoloni mamboleo kichwani kwako.Hilo soko huria ni porojo za wazungu kuwarubuni msiojua mnachosoma kama wewe.
 
Jeshi la sasa lina wasomi ambao wengine hata uraiani huwezi kuwapata.Jeshi letu lina kila aina ya wasomi.Ukienda madaktari wapo,ukitafuta mainjinia wapo,wahasibu,wapo,wachumi wapo tena wengi tu.Kazi ya jeshi pamoja na kazi zingine ni kuwa na wapiganaji wachumi ambao kazi yao ni kupigana na kuulia mbali wahujumu uchumi kwa kutumia elimu ya uchumi waliyopata.Vita si bunduki tu mhuni aweza tumia hata sukari kujaribu kuiangusha serikali au kutaka serikali ichukiwe na wananchi.Jeshi linao wapiganaji wa kila eneo.

Hao wahujumu uchumi kama wanadhani wanaweza kuwatumia wachumi koko maruhuni wa mitaani kuua uchumi wa Tanzania wanaota.WATAONDOKA WAO NA WATAPOTEZA BIASHARA ZAO TANZANIA ZITAKUFA KIFO CHA MENDE.
Kama wanatangaza vita ya kiuchumi na serikali wajiandae kufa kiuchumi wao na watajuta kwa nini wamewekeza Tanzania.Kama ni biashara wafanye lakini uhuni wowote ule kupambana na serrikali hautavumiliwa wala kukubalika.

Unaweza ukawa na hoja, ila jazba hata hoja haionekani. Jeshi letu linazalisha nini? Unapoongelea jeshi lazima uone linazalisha nini kwenye uchumi wetu. Kimsingi jeshi letu wao zaidi ya kufundishana mambo ya kijeshi halina uzalishaji mali wowote mkubwa ambapo nchi inaweza kujivunia. Kwa maneno marahisi kwakuwa hakuna vita, jeshi linatumia kuliko linavyozalisha. Nilitarajia wakati huu wa amani jeshi letu litumike kuzalisha mali, kwa mfano hizi milioni hamsini kila kijiji, jeshi lingeweza kukabidhiwa usimamizi wa miradi ya maendeleo kwenye vijiji hivyo na litoe wataalamu wake kwenda kushirikiana na wananchi kuzalisha mali. Sasa kama jeshi litasubiri kunyang'anya sukari kilo 10 au 20 huoni tija yake itakuwa ndogo? Pia jeshi wakati huu wa amani lingeweza kutumika kujenga nyumba za bei rahisi kwa kushirikiana na NHC. Tungeondoa makazi duni na watu wangeishi kwenye makazi bora. Lakini leo nenda jeshini hata vitunguu vya kupika jikoni wananunua uraiani wakati Tz ina mapori kibao!!! Jeshi kutumika kwenda kupora sukari za watu wenye mitaji yao ni kulidhalilisha, naomba Magu asithubutu kuchukua mawazo ya watu wa aina yako.
 
Utumbo mtupu
Tujiulize ufanisi na uendelevu wa miradi ya SUMA
Power tillers
Matrekta ya India
Ujenzi wa nyumba za serikali
Madawati nk..
kila kitu ni ZERO
Yaani mtu anadhani karne hii mashirika ya serikali yafanye biashara!
 
Kazi ya serikali mahali popote duniani ni kuwawezesha wananchi wake kuendesha uchumi na yenyewe kupata kodi na siyo kufanya biashara kupitia taasisi zake. Tulitoka huko tukashindwa vibaya sana. Hebu nieleze tokea serikali imewapa SUMA JKT miradi kadhaa ya biashara imekusanya kodi kiasi gani kutoka kwao? Hizo biashara wangekuwa wanafanya watu binafsi wanefuatwa na TRA hadi vyumbani kwao.
 
Wewe ndio unaongea ujinga kweli, hii ni nchi ya kijeshi? Uchumi una kanuni zake na hao wanajeshi wamefundishwa kuua. Mpaka leo hii nchi yetu ni maskini ni kipi kilichowashinda hao suma JKT kuifanya nchi iwe tajiri? Leo hii wanajeshi wanalalamika kukosa nyumba za kuishi mpaka wengine tunaishi nao huku mtaani kwenye nyumba za kupanga, hao Suma Jkt wako wapi? Kutumia nguvu bila akili ni kama kujichoresha ndugu yangu. Hao wenyewe suma JKT hata uniform tu zimechakaa sembuse kusimamia sukari ambalo ni jambo la kiuchumi? Nenda kaangalie hayo magari yao na vitendea kazi vyao vilivyo vichovu, ushindwe kusimamia cha kwako ukaweze vya wenzio waliojinyima mpaka kufikia hapo walipo? Wangalau ningekuelewa kama ungesema yaanzishwe mashamba makubwa ya miwa na kujengwa viwanda vya sukari ambapo hao suma Jkt ndio watakuwa wazalishaji, washindane na soko na sio kuleta vitisho vya kijeshi kwenye mali za watu.

Unajua hadi nakuogopa, suma Jkt waendelee kuchukua miradi ya ujenzi tu maana hata magari yao hayana namba za kijeshi, kwahiyo bado yatakuwa ni yale yale ya kupigiana promo tu kupitia jf. Rais anajua nini kifanyike, sisi tutulie kusubiri ataamua nini kutunusuru!!!
 
Back
Top Bottom