Serikali iwalipe house allowance walimu wanaoishi nyumba za kupanga kama ilivyo kada nyingine kama jeshi.

Optic nerve

Member
Mar 18, 2019
19
20
Walimu wa Tanzania ni kada inayodharauliwa sana,walimu wanaamini kuwa mchawi wa mwalimu ni mwalimu,ikimaanisha kuwa mwalimu akiwa kiongozi,huwa anawakandamiza walimu kimaslahi hata kuwa dharau huku akiwanyima maslahi walimu japo yapo kisheria.Mifano inaanzia chini kabisa,wakuu wa shule,afisa elimu kata,maafisa elimu wilayan na mikoan,hawa ni wachaw wa walimu katika harakati za walimu kuinuka kiuchumi.Ukotoka huko uangalia viongoz wengi wa kisiasa waliopitia au kuwahi kuwa walimu ni wachawi wa akubwa wa walimu,agalia naibu wazir tamisemi huyu mkurya,amesitisha makusudi kabisa uhamisho kwenye kada ya ualimu ambao upo kisheria na kikanuni.Wazir mkuu ni mwalimu,mkuu wa nchi na mke wake ni walimu hata kututetea maslahi ya walimu hawako tayari.Serikali inatambua walimu ni kada ya kimaskin inayodharauliwa na wanalipwa kidogo,walimu wengi hawana uwezo na wengi wao wamepanga nyumba,serikali imejitoa katika kulipa house allowance kama kada zingine ili kumrahisishia ugumu wa maisha huyu mwalimu ili watufundishie vzr watoto wetu.
 
Hilo haliwezekani! na sababu zao siku zote ni zile nyepesi nyepesi tu mfano watakuambia kada ya ualimu ina watumishi wengi hivyo wakiamua kuwalipa hizo allowance basi nchi itafilisika tofauti na kada nyingine ambapo watumishi wake ni wachache.

Nini cha kufanya; siku zote walimu wanatakiwa wafanye kazi under minimum stress! Fanya kazi muda kiduchu kadiri iwezekanavyo na muda mwingi unaobakia ni wa kuutumia kwenye mambo binafsi ya kujiingizia kipato. Mtoto wako jitahidi asome shule nzuri ili asije naye akaangukia kwenye ualimu ambao siku zote unatumika kama daraja dhidi ya kada nyingine.
 
Walimu wa Tanzania ni kada inayodharauliwa sana,walimu wanaamini kuwa mchawi wa mwalimu ni mwalimu,ikimaanisha kuwa mwalimu akiwa kiongozi,huwa anawakandamiza walimu kimaslahi hata kuwa dharau huku akiwanyima maslahi walimu japo yapo kisheria.Mifano inaanzia chini kabisa,wakuu wa shule,afisa elimu kata,maafisa elimu wilayan na mikoan,hawa ni wachaw wa walimu katika harakati za walimu kuinuka kiuchumi.Ukotoka huko uangalia viongoz wengi wa kisiasa waliopitia au kuwahi kuwa walimu ni wachawi wa akubwa wa walimu,agalia naibu wazir tamisemi huyu mkurya,amesitisha makusudi kabisa uhamisho kwenye kada ya ualimu ambao upo kisheria na kikanuni.Wazir mkuu ni mwalimu,mkuu wa nchi na mke wake ni walimu hata kututetea maslahi ya walimu hawako tayari.Serikali inatambua walimu ni kada ya kimaskin inayodharauliwa na wanalipwa kidogo,walimu wengi hawana uwezo na wengi wao wamepanga nyumba,serikali imejitoa katika kulipa house allowance kama kada zingine ili kumrahisishia ugumu wa maisha huyu mwalimu ili watufundishie vzr watoto wetu.
Askari/wanajeshi wanapanda daladala bule.
Watumishi wengine wanataka nyongeza za mishahara,
Yote hayo mnataka serikali ilipe!!serikali ni nini?serikali inapata mapato yake kwa kukusanya kodi na vyanzo vingine,Mh Raisi analalamika kwamba mashirika ya umma kila mwaka yanapata hasara,sasa hela itatoka wapi?
Kwa ufupi tu,nchi yetu haina mapato ya kujitoshereza kugharamia matumizi yake.
Sitisha chaguzi za kila mwaka,futa bunge,futa vyeo vya wakuu wa mikoa,punguza wafanyakazi wa umma,
Wekeza kwenye elimu,kilimo,
 
Kada zingine zinapata house allowance? Au umechukua mfano wa Askari Tu?

1. Maafisa Kilimo wa Vijiji/Kata
2. Wahudumu wa Afya(Zahanati, vituo vya Afya nk.)
3. Watendaji wa Kata/ Vijiji
4. Maafisa Maendeleo ya Jamii
5. Maafisa Afya wa Vijiji/Kata.

Hata watumishi wote wa Ngazi za Halmashauri hawapati hizo house allowance isipokuwa Wakuu wa Idara nao ni haki yao lakini kutokana na ufinyu wa bajeti wengi hawapewi. Msiwe wabinafsi kujiangalia nyinyi Tu...... Kisa viongozi wakuu wa kitaifa waliwahi kuwa Walimu Basi kila kitu mpendelewe nyinyi? Kama ni suala la maslahi hilo liwe Kwa wote na sio Walimu Tu.
 
  • Thanks
Reactions: Eco

Similar Discussions

Back
Top Bottom