Serikali iwalinde vijana wabunifu kwa kuondoa tozo ya BRELA na COSOTA. Tunaibiwa na kudhulumiwa sana

MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
4,925
8,910
Habari wadau wa JF !

Hakuna mtu asiyejua kwamba, kwa dunia ya leo "Ubunifu" ndio kila kitu.

- Lakini kutokana ukosefu wa mitaji kianzio na fedha za usajiri, vijana wabunifu wamekuwa wakiibiwa mawazo yao ndani ya usiku mmoja tena waliyoyahangaikia mpaka kukondeana miaka mingi wanapokuwa wanaenda kupitch na kutafuta wafadhili.

- Naamini wabunifu mnajua ni namna gani kazi ya kufikiria ilivyo ngumu na kama unadhani ni rahisi hebu jaribu kufikiria " Just a simple, short, catchy, sound and attractive company or brand name" uione shughuli yake.

- Kwa muktadha huu nilikuwa naiomba serikali ijaribu kuwatupia macho wabunifu hawa ili waweze kujikwamua kutokana na jasho lao kama mmoja wa wabunifu SYLVESTER STALYONE alivyofanikiwa.

Cc Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda na Biashara
 
Chochote kilicho na thamani kwako lazima kiwe na bei(price).
Kikiwa bure hutakithamini.
Band name kwa mfano ukiigharamia huwezi kuitelekeza.
 
Chochote kilicho na thamani kwako lazima kiwe na bei(price).
Kikiwa bure hutakithamini.
Band name kwa mfano ukiigharamia huwezi kuitelekeza.
Usemacho ni sahihi lakini kama ni "User Fee" haikupaswa kuwa kubwa mpaka mtu anashindwa kulipia. Ukubwa wa hizo ndio unaochochea ongezeko la biashara zisizo rasmi. Usajiri tu unakaribia pesa ya mtaji
 
Usemacho ni sahihi lakini kama ni "User Fee" haikupaswa kuwa kubwa mpaka mtu anashindwa kulipia. Ukubwa wa hizo ndio unaochochea ongezeko la biashara zisizo rasmi. Usajiri tu unakaribia pesa ya mtaji

Usajili wa COSOTA kwa mfano, Ipi ni gharama ya kutisha pale?
 
Back
Top Bottom