Serikali iwakemee watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji kujihusisha na utapeli kwa vijana walioomba nafasi za kuhesabu watu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,701
36,119
Habari!

Yaani bila aibu Mtanzania, mtendaji wa kata, mtaa na wilaya anaomba rushwa kwa vijana walioomba nafasi za kuhesabu watu.

Hii ni aibu na ukatili mkubwa.

Kijana ambaye hana ajira unathubutu vipi kumwomba rushwa ili apate ajira?

Naamini sio wote wanaofanya huu uhuni ila nimefanya utafiti na kujiridhisha kwa baadhi ya watendaji hapa Dar es salaam hili zoezi la sensa wameligeuza dili.

Je, Watanzania ni lini tutaamua kuwa waaminifu kwa kila jambo?

Serikali angalau wakemee kwenye media huu urasimu, na mabinti wengine wanaombwa tendo la ndoa.

Hii ni aibu.

Niko tayari kutoa ushirikiano endapo mtu au taasisi itahitaji ushirikiano katika hili.
 
Hiyo tu? Kuna zoezi la anwani za makazi, kila mtendaji amejitafutia watu wa kuandika namba kwenye nyumba na mabango ya barabara za mitaa iliyoko kwenye kata zao, cha ajabu wanaomba nao wapewe hela na hao waandika namba na mabango, tena wanajipangia fedha wapewe kama takrima. Mbaya zaidi wanapunguza fedha za makubuliano kwa kila nyumba huku wanataka pia wapewe takrima. Hawaridhiki na mishahara yao.
 
Back
Top Bottom