Serikali iunde sera madhubuti kusaidia wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kujikimu wakati huu wa kupambana na Covid-19

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
23,463
70,191
Wakati nchi mbali mbali duniani zikotoa subsidies kwa wananchi wake na makampuni ili kuweza kujikimu kipindi hiki kigumu cha mapambano dhidi ya covid-19 hali imekuwa tofauti Tanzania ambapo serikali inataka kuchangisha tena na kutapeli wananchi na wadau wengine.
2351528_2C77CA7D-132F-459B-BBE2-7AE00F75E22F.jpeg
2351526_BD123602-CBBB-4505-BDD4-AADB773B909D.jpeg


Tuangalie nchi za wenzetu wanachofanya. Mfano Canada wametoa subsidy ya asilimia 75 ya mishahara kwa small and medium enterprises ili wafanyakazi katika sekta hizo waweze kujikimu huku biashara zikiendelea ku survive. Pia wamerahisisha kwa kutoa interest free loans (mikopo isiyo na riba).

Trudeau promises 75% wage subsidy for businesses hit by coronavirus pandemic

Wakati huo huo IMF wanaprovide emergency financing kwa nchi mbali mbali ili kuweza ku uphold well being ya raia wake. Soma hapa

Fiscal Policies to Protect People During the Coronavirus Outbreak

Serikali yetu inafikiria nini kukopa humo kwaajili ya well being ya raia wake? Je wanapenda kukopa kwaajili ya kujenga mabarabara na reli tu na kununua wapinzani?

Katika kipindi kama hiki ndio wakati serikali ilitakiwa angalau isaidie makampuni binafsi na wafanyakazi kwa kutoa subsidies. Mfano baadhi ya kampuni za utalii zimepunguza wafanyakazi kwa muda na nyingine ambazo hazijapunguza basi wafanyakazi wamekubali na waajiri kulipwa nusu mshahara.

Ajabu sasa serikali bado hapo kwenye nusu mshahara bado watakata PAYE na makokoro kibao mwisho wa siku wafanyakazi watashindwa kujikimu na familia zao.

Policy makers wetu mmelala usingizi? Kwanini hatujasikia matamko mpaka sasa kwa maslahi mapana ya wananchi? Viongozi wa nchi za wenzetu wako frontline kupambana na covid-19 mpaka kufikia hatua ya wao wenyewe kuambukizwa (refer: Boris Johnson n.k)

Lakini viongozi wetu wamekimbia miji wanajificha sehemu zenye less population kwa kuogopa. Nini maana ya kupewa dhamana ya kuongoza nchi kama utakimbia wakati wa majanga?
 
Back
Top Bottom