Serikali itusaidie kuona mijadala ndani ya Bunge-Live

Mamboleo

Member
Oct 15, 2008
69
38
Pamoja na nia nzuri ya serikali kubana matumizi na Bunge pia kuamua kurusha Habari za bunge bila kuchukuliwa na vituo binafsi vya televishen moja kwa moja,mie kama raia wa Tanzania ninaisihi sana serikali yenu na Bunge letu tukufu kuruhusu vitu binafsi kurusha matangao “live” ya vipindi vya bunge.

Sis kama wananchi tunahitaji kuona namna serikali yetu inavyoelezea mipango yake ya maendeleo na na hiyo kupata nafasi ya kujua ni namna gani ya kusaidiana nayo katika mipango hiyo.

Ikiwa mijadala haitaonyesha,nina uhakika kuna vyombo vya Habari na watu watakaopotosha mambo mengi yanayohusu mipango mema na mizuri ya serikali ya Mh.John Pombe Magufuli.

Bado sina uhakika ni kwa nini watu wengi wanahisi kuwa wapinzani wanapata sifa kwa kuonekana michango juu ya mijadala yao bungeni.Sifa zinapatikana kwa serikali kuwa na viongozi shupavu na imara wanaoeleza mipango na mikakati ya serikali vizuri na kwa ufasaha hivyo kuzib mianya ya wapotoshaji.

Naiomba serikali yetu ituonyeshe mijadala ya ndani ya bunge Tanzania moja kwa moja(Live)
 
Wazungu wanasema 'information is power' na hiyo power wanayosema ni 'knowledge' na 'knowledge = education'.
Angalia kila kitu Tanzania kiko ovyo sababu ya lack of knowledge, hii ni kuanzia utendaji mbovu makazini, michezo hata ufisadi unaofanyika ni wa kijinga mno! Sasa nchi itatokaje kwenye giza la ujinga bila kupata taarifa!!!???
Kwa maana hiyo wanaosimamia mpango huu nao ni victims wa 'lack of knowledge' na wanataka Watanzania wote nao waendelee kuwa mazuzu kama wao! Sidhani kama serikali inaweza kusaidia lolote katika hili maana ndio hiyo hiyo inazuia habari, ni zamu ya Watanzania wachache wenye kuelewa sasa kuwaonyesha wajinga wengi na wenye nguvu kuwa binadamu sio kondoo!
 
Back
Top Bottom