Serikali itusaidie kukomesha huu udalali kwenye tiketi za mabasi

Mrs Bishanga

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,002
2,272
Tarehe 24/12/2020 nilienda ubungo kukata tiketi ya kuelekea mafinga. Baada ya kupita ofisi karibia zote za Mabasi yanayofanya safari za huko niliambiwa tiketi zimejaa hadi za tarehe 27/12/2020.

Basi huku na huku akaja kijana mmoja akaniambia kama nina 40,000 anipe siti kwenye Njombe Express nisafiri tarehe 25 ila ni ya mwisho kabisa. Basi nikakubali. Tarehe 25 nimefika kwenye basi saa 11.00 alfajiri nikaona bado wanapiga debe kwenye mabasi ya Galaxy, Njombe Express, Luwinzo nk.

Abiria wengi tu wakakatiwa siti za mbele kabisa kwenye mabasi haya tuloambiwa yamejaa tena kwa bei kubwa. Hivi hii ni haki? Huyu askari anayehusika anakuwa wapi?

Leo nimefanya mawasiliano natafuta tiketi ya kutoka Ubungo kwenda Upareni ofisi za mabasi ya huko wanadai siti hakuna kuanzia leo hadi tarehe 1/1/2021. Narudishwa kuongea na maajenti ambao nao wanadalalia tiketi.

Safari ya 20,000 wanataka ilipiwe hadi 40,000 je hii ni sawa? Utashangaa siku ya safari pale Ubungo asubuhi tiketi zitakuwa nyingi sana tu. Kutengeneza uhaba (scarcity) ili bei zipandishwe ni uhujumu uchumi pia. Tunaomba seikali ishughulikie hili. Ina maana mamlaka hazijui huu uhuni?
 
Ticket uliipata ofisini? Ulioneshwa passenger manifest?(Chati)
Kama jibu ni ndiyo anza na muhusika aliyekukatia ticket Kama ulinunua uchochotoni hilo ni kipengele kingine
 
Tarehe 24/12/2020 nilienda ubungo kukata tiketi ya kuelekea mafinga. Baada ya kupita ofisi karibia zote za Mabasi yanayofanya safari za huko niliambiwa tiketi zimejaa hadi za tarehe 27/12/2020.

Basi huku na huku akaja kijana mmoja akaniambia kama nina 40,000 anipe siti kwenye Njombe Express nisafiri tarehe 25 ila ni ya mwisho kabisa. Basi nikakubali. Tarehe 25 nimefika kwenye basi saa 11.00 alfajiri nikaona bado wanapiga debe kwenye mabasi ya Galaxy, Njombe Express, Luwinzo nk.

Abiria wengi tu wakakatiwa siti za mbele kabisa kwenye mabasi haya tuloambiwa yamejaa tena kwa bei kubwa. Hivi hii ni haki? Huyu askari anayehusika anakuwa wapi?

Leo nimefanya mawasiliano natafuta tiketi ya kutoka Ubungo kwenda Upareni ofisi za mabasi ya huko wanadai siti hakuna kuanzia leo hadi tarehe 1/1/2021. Narudishwa kuongea na maajenti ambao nao wanadalalia tiketi.

Safari ya 20,000 wanataka ilipiwe hadi 40,000 je hii ni sawa? Utashangaa siku ya safari pale Ubungo asubuhi tiketi zitakuwa nyingi sana tu. Kutengeneza uhaba (scarcity) ili bei zipandishwe ni uhujumu uchumi pia. Tunaomba seikali ishughulikie hili. Ina maana mamlaka hazijui huu uhuni?
Usikute ofisi ulizoingia hazihusiani kabisa na hayo mabasi
 
Wale wanafanya wizi, mara nyingi tu nimeshawahi kuambiwa gari imejaa. Kesho yake ukifika pale saa 11 asubuhi unakuta wanakatisha tiketi mlangoni, gari ileile waliyosema imejaa. Ukikatia pale asubuhi unatozwa pesa kubwa.
 
Back
Top Bottom