Serikali itunge Sheria ili mahojiano kati ya trafiki na dereva yafanyike huku abiria wakisikia Kila kitu. Kama inataka kufuta rushwa Kwa trafiki

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,495
2,043
Ndugu wanabodi huwa nakerwa sana na hii tabia ya askari wa usalama barabarani kuchukuana na kondakta au dereva wa gari na kuenda kumalizana nyuma ya gari.

Utamaduni huu unafuga rushwa na kupelekea zoezi la ukaguzi wa magari kufanywa kisanii tu.
Naiomba serikali ipitishe Sheria mahojiano kati ya dereva na traffic yasifanyike Kwa kificho.
 
Trafiki wote wapewe spika za megafone wazitumie kuhojiana na madereva🤣
 
Ndugu wanabodi huwa nakerwa sana na hii tabia ya askari wa usalama barabarani kuchukuana na kondakta au dereva wa gari na kuenda kumalizana nyuma ya gari.

Utamaduni huu unafuga rushwa na kupelekea zoezi la ukaguzi wa magari kufanywa kisanii tu.
Naiomba serikali ipitishe Sheria mahojiano kati ya dereva na traffic yasifanyike Kwa kificho.
acha umbea
 
Niliwahi leta humu Syndicate ya rushwa ya Trafiki Barabarani, Wakina Mod wakafuta faster post yangu.

Kwa kifupi Rushwa ya Trafiki ni Syndicate mkuu kuna watu wengi sana wako kwenye pyroo ya Trafiki.

Ndani ya jeshi la Polici kuanzia IGP hakuna anaue weza kukemea hili make ni mnufaikaji mkubwa, Wizara ya mambo ya ndani kuna wayu ni wanufaikaji wakubwa.

Mkoan hadi Offisi ya mkuu wa mkoa kuna wanufaikaji, Wilayani hao wakina Mkuu w wilaya ni wanufaikaji, Takukuru wilayani ni wanafaikaji.
 
Ndugu wanabodi huwa nakerwa sana na hii tabia ya askari wa usalama barabarani kuchukuana na kondakta au dereva wa gari na kuenda kumalizana nyuma ya gari.

Utamaduni huu unafuga rushwa na kupelekea zoezi la ukaguzi wa magari kufanywa kisanii tu.
Naiomba serikali ipitishe Sheria mahojiano kati ya dereva na traffic yasifanyike Kwa kificho.
Hivi,unamjua binadamu vizuri?Atatafuta mbinu nyingine.
 
Kwa Tanzania bado sana kuondoa au hata kupunguza hiyo rushwa ya barabarani. Hapo Kenya wameenda mbali zaidi kuondoa hii rushwa ya barabarani kwa kuweka sheria ngumu ya kuwa hakuna trafiki atakayeruhusiwa kusimamisha gari barabarani kama hana "reflactor jacket" maalum. Reflactor Jacket hiyo inayotolewa na serikali ya Kenya kwa askari wake wa barabarani ina kamera na kinasa sauti kwa hiyo kwa mazungumzo kati ya dereva na askari wa barabarani yanachukuliwa video na sauti kwa wakati mmoja.
 
tutawaua njaa ma-trafic wetu na kazi wataiona chungu; tuwaache maana maisha yatakuwa magumu kwao - 1.2m kwa mwezi una familia ya watu 6 home utakimbia mji. :D
 
Kwa nini Trafic wanaogopa kuishauri serikali mabasi yasafiri usiku. ? Makusanyo yatashuka?

Ndugu wanabodi huwa nakerwa sana na hii tabia ya askari wa usalama barabarani kuchukuana na kondakta au dereva wa gari na kuenda kumalizana nyuma ya gari.

Utamaduni huu unafuga rushwa na kupelekea zoezi la ukaguzi wa magari kufanywa kisanii tu.
Naiomba serikali ipitishe Sheria mahojiano kati ya dereva na traffic yasifanyike Kwa kificho.
 
Ndugu wanabodi huwa nakerwa sana na hii tabia ya askari wa usalama barabarani kuchukuana na kondakta au dereva wa gari na kuenda kumalizana nyuma ya gari.

Utamaduni huu unafuga rushwa na kupelekea zoezi la ukaguzi wa magari kufanywa kisanii tu.
Naiomba serikali ipitishe Sheria mahojiano kati ya dereva na traffic yasifanyike Kwa kificho.
Hakuna kitu hapo ..maana rushwa inawekwa kwenye makaratasi anayo kagua trafiki.ni kimya kimya tu .dereva anajiandaa na rushwa kabla hata ya safari
 
Unataka wakose afutatu za kubrashia?

Gari za masafa marefu(Dar -Mwanza, Mbeya, Kagera, Mara, Tunduma n.k) kila siku lazima zipoteze sio chini ya 30k kwa kuwalipa matrafiki.

Hili nimeliona mara kadhaa baada kukaa kwenye kigodoro nikipanda gari hizo. Konda kila akiona anakaribia kijiwe cha hao jamaa, anakunja elfu 5 kwenye kikaratasi, akifika anashuka fasta anasalimiana naye chini mbele ya gari, sekunde 5 tu gari inasepa.

Kuna trafiki pale Mtumbatu kuelekea Gairo walikuwa wanawake 3, bila aibu ya kike wakachukua buku 5 wakiwa wamekaza sura kabisa.

Rushwa haiwezi kuisha nchi hii hata kama sheria ngumu na kali kiasi gani zitungwe hii ni kutokana na wasimamizi wa sheria ndio vinara wa Rushwa
 
Back
Top Bottom