Serikali ituambie ni hatua gani zinazochukuliwa ili tuache kuwategemea mabeberu!

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,087
2,000
Wanajamvi,

Kwanza, kama serikali ya ccm inaona kwamba ni yenyewe peke yake inayoweza kusimamia rasilimali zetu kwa usahihi, basi wanajidanganya! Na hilo naweza kulipinga kwasababu historia na hali halisi za wananchi havi akisi hilo.

Kwa mfano hata Maghufuli alipoingia madarakani, alikuwa analalamikia mikataba ambayo wao wenyewe waliisaini. Siyo upinzani kwa maana ya chadema wala cuf ama chama kingine chochote tofauti na ccm.

Sehemu Lissu alipopishana na Maghufuli.

Walipopishana, ni pale ambapo kwa maoni yangu, serikali imechaguwa njia ya kutokusema ukweli, kutumia hadaa na ukosefu wa hekima na busara.

Kwasababu haya mambo ni ya siasa, TL aliona jinsi Maghufuli anavyotaka kuwapiga bao wao kama wapinzani. Kwa kujidai kuwa wao ni wazalendo wenye kusimamia nchi na rasilimali zake dhidi ya mabeberu. Na wakati si kweli. Wao ccm ndiyo walioingia hiyo mikataba! Wapinzani wana haki ya kulikosoa hilo! Kwasababu ccm ni kama wametengeneza tatizo wao halafu wanataka kutuaminisha kwamba wao siyo waanzilishi bali watatuzi wa matatizo yetu. Hapa ndipo pahala ambapo demokrasia ilitakiwa ifanye kazi kama ni kweli ipo. Siyo kweli kwamba wananchi wanakubaliana na hali hiyo iliyopo kwa zaidi ya miaka hamsini sasa!

Lissu alipoona wanataka kupigwa bao, ndipo akaweka wazi kuwa wao ndiyo wamesaini mikataba, na hawana ujanja zaidi ya kuiheshimu, ili tusiweze kuingizwa kwenye janga kubwa zaidi la kulipishwa faini kama ilivyotokea ndege kukamatwa kwa sababu hiyo. Ambapo kuna kesi ilifunguliwa na tukashindwa!

Tatizo lilikuja kwasababu Magufuli na watu wake, waliamini kuwa Lissu ndiye aliyewashtua wadeni wetu kuhusu ndege inayotoka Canada ambayo tuliagiza. Kwahiyo kuanzia hapo ndo akaanza kuitwa msaliti ambaye hastahili hata kuendelea kuvuta pumzi!

Kwahiyo ccm hapo ikawa imeshamtengeneza adui anayeshirikiana na mabeberu dhidi ya Taifa na rasilimali zake!!

Ila ukitizama kwa jicho la tatu, siyo kweli! Halafu hapo inanikumbushia zile story zinazohusiana na wahalifu ama makundi ya uhalifu nk. Kuna kitu wanachokiita “snitching”, yani kutoa taarifa polisi ili wakamatwe, hao dawa yao huwa ni kuuwawa. Kitendo alichofanyiwa TL ni kama hivyo tu. Pale wanapodai alitoa taarifa za uhalifu! Maana kama mahakama iliamuwa, serikali ikaenda kinyume, huo ni uhalifu, na TL kama mpinzani, ni haki yake na wapinzani kusema hapa serikali mmeshindwa kazi, wanatoa hoja zao. Ndivyo demokrasia ilivyo. Serikali siyo genge la uhalifu! Wala haitakiwi kuwa kama genge la uhalifu!

Kwahiyo kwenye hili, kabla sijauliza swali langu la msingi, kuhusiana na hatua serikali inazozichukuwa ili tuache kuwategemea mabeberu, ningependa kuipa serikali ushauri.

Kama serikali na ccm kwa ujumla, wanaamini kabisa kuwa ni wao tu ndiyo wazalendo, kwamba ni wao tu wanaoweza kuingia mikataba mizuri ya rasilimali zetu, kwamba ni wao pekee wanaoweza kuzisimamia kwa dhamira moja na kwa dhati kabisa rasilimali zetu(mimi siamini), basi wafute kabisa vyama vingi kabla hatujaingia kwenye machafuko! Huu ni ushauri ambao ni muhimu kuzingatiwa.

Sasa, nirudi kwenye swali, Je kuna wanaofahamu hizo hatua? Tafadhali wasije kusema kuwadhibiti wapinzani, kuwanyansa, kuwateka ama kuwauwa, ndiyo mojawapo ya hizo hatua, Maana kama ni hivyo, pointi yangu ya kufuta vyama vingi inakuwa na nguvu zaidi.

Je ni kuongeza kodi zaidi kwasababu hao mabeberu wanakuwa wamepunguza kuchangia? Hilo nalo litakuwa “smooth”, endapo tutakuwa chini ya mfumo wa chama kimoja, kwasababu wananchi kama ni kweli wana haki ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi huru na wa haki, hawawezi kukubaliana na hali hiyo, wakiona wanakamuliwa hadi damu, Wanaweza kusikiliza sera mbadala na kutoa nafasi kwa chama kingine. Kwahiyo tena kama ni kweli mnataka kupambana na mabeberu, hatua ya kwanza ni kufuta upinzani.

Lakini binafsi siamini kama upinzani ukifutwa ndiyo maendeleo! Kwasababu hata Sasa hivi bado kuna upinzani, lakini ccm ni kama vile wako kwenye “comfort zone” na huku umasikini ndiyo ukizidi!

Je kuna hatua zozote za kiuchumi ambazo serikali inazichukuwa ili kufanikisha hilo la kuachana na utegemezi wa mabeberu?

cc Mzee Mwanakijiji , Rev. Kishoka
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
23,087
2,000
Inaweza isiwe hatua za kisiasa pekee, bali hata za kiuchumi. Kama kuna wenye maoni zaidi ya kelele za usaliti na sijui kushirikiana na mabeberu, ni bora mkaweka maoni yenu ili tuache kuwategemea mabeberu. Lakini endapo hizo hatua hazipo, basi kwa maoni yangu, ccm ndo wasaliti wa Taifa letu. Pamoja na wale wote wanaosapoti matendo yao kama hayaendani na kusaidia na kulikwamua Taifa letu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom