ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Katika sekeseke la makontena 349 ni makontena takribani 200 tu ndiyo watanzania tumeambiwa wamiliki wake na mengine yaliyosalia mamlaka husika zinapata kigugumizi gani kutuambia nani mmiliki wake pamoja na serikali kutoa siku saba wahusika kujitokeza na kuyalipia.
Taarifa zilizo zagaa ni kwamba makontena hayo yamelipiwa kinyemela huku wahusika bila kufahamishwa ni nani anayamiliki makontena hayo.
Tunaamini kwamba serikali yetu ni sikivu , ya uwazi na ukweli tunaomba tuambiwe hayo makontena ni ya nani , wahusika watajwe kama walivyo tajwa wale wa mwanzo , wahusika wabainishwe bila kujali vyeo au wadhifa waliokuwa navyo, hii itailetea heshima serikali ya awamu ya tano