ely B
Member
- Jul 27, 2016
- 14
- 4
Kwanza naipongeza serikali kwa hatua ilizochukua kuhusu kupunguza gharama za maombi kwa vyuo vyake kwa waombaji wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka 2017/18.
Ombi langu kwa serikali ni kuiomba itoe tamko kwa umma na kwa vyuo husika kurudisha pesa kwa waombaji walio omba kabla ya gharama kupungua.
Nasema hivi kwa kile ninachokiona kwa baadhi ya vyuo kutoa taarifa ya kuwa wale walio lipa kabla ya gharama kupungua wakipata nafasi kwenye vyuo hivyo hiyo hela itawekwa kwenye ada na baadhi ya vyuo mpaka sasa havijatoa matangazo yoyote ili hali vimebadilisha gharama ya maombi.
Pia suala la kusema kuwa hiyo hela itarudishwa pale tu utakapokuwa umeonyesha kumbukumbu ya malipo na kwa kuzingatia mfumo wa ulipaji ulitumia njia ya mitandao ya simu kwa vyuo karibia vyote.Je, kwa ambaye ameshaifuta message aliyotumiwa kama namba ya kumbukumbu atasaidiwaje?
Na pia kwa walio bahatika kusoma vyuo vikuu suala la chuo kurudisha hela kwa mwanafunzi huwa ni suala ambalo chuo linakiona kama gumu yaani wanakupatia milolongo mirefu adi unakata tamaa.
Mwisho wa kuwasilisha.