Serikali itoe ripoti ya Mapato kila Mwezi

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Nimechunguza mijadala mingi.. inaonekana wengi wetu hatuna au hatujui mapato mbali yanayo tokana na serikali.. Laiti serikali ingeweka wazi naamini wadau wengi wengeweza kuchangia maoni yao namna ya kuboresha mapato hayo..

Nashauri serikali badala ya hotuba za rais za kila mwezi basi kuwe na report ya mapato na matumizi ya kila mwezi ili wadau wa sekta mbalimbali waweze kuchangia ktk kuboresha mapato ya taifa..

Tangu magufuli atangaze mapato ya december kumekua na maoni mazuro sana na pia imeonekana ni kitu kinacho tia hamasa wananchi na wadau mbalimbali kutoa maoni..
Kuna mapato mbalimbali ambayo hatujui hata yanachangia kiasi gani.

Uwazi kama huu hata bageti inapo somwa tutakua na uhakika na serikali juu ya mipango yake..

Pengine itafaa kujiuliza kwanini serikali hii haitaki kuweka wazi mapato kwa kila sekta husika?
 
Report za bot ni za wasomi... watu wa kawaida wanahitaji report nyepesi kama aliyo toa magufuli.. haaaa
 
Nadhani hii itasaidia hata kujua pesa hzio zinakwenda wapi/
Kinachohitajika ni taarifa mbili. 1. Taarifa ya mapato kila mwezi kuanzia ngapi za chini hadi taifa 2. Taarifa ya mapato namatumizi kila baada ya miezi mitatu. Taarifa hii italinganishwa italinganishwa na taarifa za mapato za kila mwezi. Lengo ni kuona matumizi hayazidi mapayo
 
Back
Top Bottom