Marisi schweini
Senior Member
- Dec 3, 2018
- 130
- 374
Wasalaam wanajukwaa...!! Kulingana na hali ya uchumi wa wananchi walio wengi hasa vijijini ambako wanaishi asilimia zaidi ya 75 kuwa mbaya ambapo walio wengi wanaishi chini ya msitari wa umasikini hivo kushindwa kuhimili hata mahitaji msingi ya binadamu achilia mbali mahitaji mengineyo muhimu kama afya n.k,
Wasichana wengi walio katika umri wa kupevuka wamekuwa wakishindwa kuhimili gharama za kununua vitaulo hivi na kujikuta wakitumia vipande vya khanga n.k ambavyo sio salama kwa afya zao. Wengine wamejikuta wakikosa kujiamini na kuathirika kisaikolojia huku wengine wakishindwa kuhudhuria shule siku ambazo wako kwenye hedhi kutokana na kukosa vitaulo vya kuwasitiri.
Wengine wamejikuta wakidanganyika na kuingia kwenye tabia povu ili kuweza kupata pesa za kustahimili kununua pedo kutokana na hali duni ya kipato cha familia
Naomba serikali iangalie uwezekano wa kupeleka vitaulo hivi shule za sekondari ambapo kila msichana ataweza kupata hitaji hili la msingi. Serikali inaweza kuamua kutafuta vyanzo cha kufund na napendekeza mojawapo iwe makato ya asilimia kadhaa ya mshahara wa wabunge na mawaziri pamoja na kuongeza kodi kwenye vipodozi. Naomba kuwakilisha
Cc: Paschal mayalla ; zitto; Faiza fox;