Serikali itazame upya Sera za kuendesha uchumi na watu sahihi wa kuendesha uchumi

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,842
Kwenye hii story ya vijana wa JKT kikubwa kabisa ni story ya ukosefu wa ajira.

Kama sikosei kuna takwimu zilitoka kuonesha uchumi wetu ulikuwa unakuwa Kwa asilimia 2.5 Tu Kwa miaka miwili iliyopita.

Tofauti na propaganda za kuwa unakuwa Kwa asilimia 7 kila mwaka.

Na ili uchumi uzalishe ajira za kutosha lazima ukue Kwa asilimia kuanzia 15.

Kwahiyo tatizo letu kubwa hapa Tz sasa ni uchumi mbovu unaoendeshwa vibaya na maagizo ya kisiasa ndo maana unaona vijana wanaandamana. Kwenda kuomba kuajiriwa jeshini kwa nguvu.

Nchi hii kuajiriwa serikalini ni 'kuukata'.

Zamani enzi za Mzee Ruksa watu walikuwa hawataki kuajiriwa serikalini, wengine hadi wanaacha kazi wanaenda sekta binafsi.

Serikali itazame upya Sera za kuendesha uchumi na watu sahihi wa kuendesha uchumi, vinginenevyo hili bomu la ajira litalipuka mda si mrefu.
 
Uko sahihi mkuu. Suala la ukosefu wa ajira kwa vijana ni changamoto kubwa sana. Hata hivyo haitoshi tu kila mtu kusema 'ni bomu libalosubiria kulipuka' kisha akaishia hapo.

Siku nikitulia nitaleta ushauri wa kisera juu ya namna ya kulitatua tatizo hili angalau kwa 50℅ kwa kutumia timing, kucheza na mifumo ya elimu kwenye angle degree flani hivi na kutumia fund kwa kiwango kile kile ambacho kinatumika kwa sassa au kwa nyongeza kidogo sana.

Nitaomba mjadala huo ukija kila mtu aweke input zake ili tuweze kuwasaidia wafanya maamuzi na sote kwa pamoja tutatue tatizo hili.

Ni muhimu kuwasadia vijana wenzetu, wanapata shida sana ndugu zangu, na taifa linapata hasara kubwa kundi la vijana linapokuwa halizalishi wa la kuweza kujitegemea
 
Tunapowalaumu tu watunga sera au wafanya maamuzi kwenye suala hili la ukosefu wa ajira, inakuwa si sawa sana. Issue hii ni complicated &paradoxical, hivyo inahitaji kutuliza vichwa kweli kweli kufikiri kuliko kurushiana maneno.

Suala hili ni mfano wa korona ambayo licha ya kuwa tuna uhakika ni tatizo ambalo kweli lipo lakini wengi hawajui dawa ni nini na kuwa kiongozi pekeee hakukufanyi ujue dawa.

Kwa hiyo ni muhimu kila mtu aka play party yake.

Uzuri ni kwamba kwa utafiti ambao nimeufanya mwaka 2019- 2020, inaoneka kwamba kwa miaka ya hivi karibuni, maamuzi mengi ya viongozi wa nchi mbalimbali duniani huathiriwa kwa kiasi flani na mijadala mbalimbali inayofanyika mitandaoni. Uzuri zaidi ni kwamba ipo dalili kwamba serikali hii ya awamu ya sita itakuwa inashaurika vyema zaidi kuliko hapo kabla.

Hivyo tutumie mitandao hii wisely, na nawahakikishia kuna kitu kizuri kitatokea inshaallah.
 
Suala la ajira ni wakat wa serikali kuangalia mfumo wa kielemu mahitaji yetu kwa sasa ni tofauti na kipindi tunapata uhuru Tanzania kipindi cha uhuru tulikuwa tunaitaji wasomi ila sasa sidhani kama mahitaji ya wasomi ni makubwa sana.

Wasomi wapo wengi sana ni wakati sasa wa kudeal na kuwekeza kwenye fani ambazo huitaji kuajiriwa unaweza kufanya mwenyewe mfano ufundi tuboreshe Veta na vyuo vya ufundi ikibidi hata tutoe na mikopo kuwa shawishi watu kwenda kusomea ufundi huyu fundi ni vyepesi kukulipa mkopo kwa maana akimaliza tu anaweza kujiajiri na kuanza kutengeneza pesa kuliko huyu uhasibu, Doctor, Engineer ambae mpk apate ajira ambazo hazipo.

Kipindi tunaitaji wasomi tuliwekeza nguvu kubwa mpaka kila mtanzania akaamini degree ndo kila kitu hii ikapelekea kupatikana mpk Degree za Chupi na watu kuanza kufoji vyeti imefikia hatua tofauti ya msomi na darasa la saba kuwa ni cheti tu.

Hatuwezi kuendelea kwa kutengeneza taifa la white collar jobs sasa ni wakati wa kutengeneza blue collar jobs pia kudhibiti idadi ya wanaoenda vyuo waende wale wenye sifa kweli kweli mfano hata kwa mwaka tukizalisha wasomi laki 2 mwenye weledi inatosha kuliko kuzalisha wasomi laki 8 ambao hawana tija zaidi ya mavyeti tu

Waende vyuo wachache wengi waende Veta na vyuo vya ufundi na wapate mikopo kabisa kama hawa wanaoenda vyuo
 
Aidha, nawahakikishieni, atakayefanya kitu kusaidia kutatua tatizo hili la ukosefu wa ajira nchini, atakuwa amefanya jambo kubwa sana la kiubinadamu na kutoa mchango usiomithilika kwenye taifa hili. Vile vile atakuwa na sehemu maalum huko peponi ( jocking).

Kwa hiyo kama kuna eneo la kushindania kwa sasa, ni kuja na ufumbuzi kwenye mambo mawili. Moja ni hili na la pili ni dawa na chanjo ya kuaminika ya korona. Kadhalika mashindano ya kutafuta ufumbuzi wa mambo haya yana faida bila hasara tofauti na mashindano ya aina nyingine kama ya kugombea madaraka na.k
 
Zamani enzi za Mzee Ruksa watu walikuwa hawataki kuajiriwa serikalini.
Wengine hadi wanaacha kazi.. wanaenda sekta binafsi.

Serikali itazame upya Sera za kuendesha uchumi na watu sahihi wa kuendesha uchumi.. vinginenevyo hili bomu la ajira litalipuka mda si mrefu
Kwa hiyo unamshauri mama Samia achapishe pesa nyingi kama alivyoshauriwa vibaya mzee Mwinyi? Unataka kujaza mission town kila mahali kwa fedha ambazo hazikuzalisha bali zilichapishwa, inflation ikiongezeka utafurahi?
 
Marehemu meko alimuachia madiluu maelekezo ya kutudanganya kuwa wametengeneza ajira milion12! Haya majitu bora yangekufa yote mawili
Ataanza mama yako halafu utafuata wewe!

Kama MUNGU ni mjomba wako subiri utaona!

Mb*a wewe!
 
Tunahitaji watu wenye akili na ubunifu kuongoza wizara ya elimu; kwa sababu ufumbuzi wa tatizo la ajira litategemea kama elimu wanayopata vijana inaendana na matakwa ya waajiri!
 
Tatizo kubwa zaidi ni kupika uongo.

Serikali inatunga sheria kabisa ili kuulinda uongo inaousambaza kwa watu wake.

Ile sheria ya takwimu na kitengo chenyewe cha takwimu ni upumbavu.

Huyu mama anayo mengi sana ya kurekebisha, na sioni kamwe kwamba anao ujasiri au uwezo wa kurekebisha mengi yaliyovurugwa.

Na kama atajaribu kurekebisha nina wasiwasi mkubwa sana naye, inawezekana Kikwete akawa ni bora zaidi baada ya yeye kurekebisha.

Hii miaka minne tunaweza kujikuta tunatoka kwenye 'extreme' moja mbovu sana, na kwenda mbio zaidi kuelekea kwenye 'extreme' ya upande mwingine ambao pia hauna manufaa sana kwa taifa letu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
punguza ukubwa wa bunge pesa zianzishe veta nchi nzima.

futa post za kiserikali zisizo na lazima,mfano madc,pesa peleka kwenye kutrain vijana waone kujiajiri ndiyo kitu cha fahari zaid.

weka sera rafiki ili kuwawezesha vijana kusafiri ughaibuni kirahisi kusaka fursa.
wakitoka veta,wape passport,waende nje huko iwe sudani kusini au uchina.

cha msingi weka sheria kali yasije yakatokea kama ya wanaijeria.

wakifika huko wakishaajiriwa wale wanaotuma pesa nyingi nyumbani serikali iwatambue.

serikali iboreshe michezo ili vijana wajiajiri huko.
katika hili azam kupitia michezo ya ngumi apongezwe.
 
Sky Eclat

nadhani ifike kipindi serikali itekeleze lile agizo lake la kuwa one stop investment block.

taasisi zote zinazohusika na uwekezaji zikae katika jengo moja.

ilo likifanikiwa serikali iboreshe mitandao wake,si vyema ofisi za umma zikakosa mtandao.

na mwisho serikali iboreshe masilahi ya watumishi wake.
 
Tuliambiwa idadi ya viwanda ambayo awamu ya tano imezalisha ni 2,400. Kama hili lingekuwa sahihi tatizo la ajira kwa vijana lingepungua.

Hata tukijenga viwanda millioni kumi lakini kama wahitimu wetu hawana skill sets zinazohitajiwa na viwanda hivyo, watazidi kuranda randa barabarani tu!

Zaidi ya hapo lazima wahitimu wetu wafundishwe kuwa waaminifu wawapo kazini kwani wawekezaji wengi wanalalamika kuwa wafanya kazi watanzania sio waaminifu ndio maana wanaajiri kutoka nchi nyingine!
 
Back
Top Bottom