Serikali itazame TANROADS kwa manyanyaso haya barabarani

majutobeach

JF-Expert Member
Aug 10, 2016
212
164
Sisi madereva wa magari makubwa hususani malori tunanyanyasika sana barabarani imefikia hatua hata ya kuichukia serikali yetu inayoongozwa na mtukufu Rais Dkt. John Pombe Magufuli tunaimani sana na Rais wetu huyu kwa utendaji kazi wake wenye kuleta maendeleo nchini na mtetezi wa wanyonge lakini kuna baadhi ya watendaji kazi wake wanamuangusha.

Nirudi kwenye mada; MADEREVA wa maroli tunanyanyaswa sana na hawa watu wa TANROADS kwenye swala la parking kwa mfano mimi nimetoka safari aidha nimetoka Congo nakuja Dar es Salaam ninakaa Kibamba huku njiani kutokana na kujibana kwangu matumizi nikaninua mkaa aidha nyanya au hata mahindi japo debe mbili tu na lazimishwa nisisimame kwenye parking yeyote mpaka nikasimame Mbezi Mwisho au Temboni kwenye parking ya malori kisha nitafute usafiri wa kukodi nibebe mzigo wangu nirudi nao Kibamba ambao huo usafiri nitakaochukua kutoka Temboni mpaka Kibamba ughalama kubwa si chini ya elfu ishilini.

Tunaiomba serikali yetu tukufu ituangalie sisi madereva wa malori tunapata tabu sana watu wa TANROADS wanatunyanyasa sana wakikuta unashusha mzigo japo kwa dakika tano tu faini yake wanataka laki tatu chondechonde Mh Rais tunakuomba uliangalie swala hili hawa watu wana tusumbua sana sana sisi madereva wa malori pamoja na kufanyakazi ngumu tunashangaa serikali yetu kupitia watendaji wake wanavyo tusumbua humu barabarani wezetu huko tukoka safiri hususani CONGO, RWANDA, UGANDA, ZAMBIA NK huwa wanaheshimu sana Madereva wa magari haya, unahitaji kupumzika kuna parking tena zipo barabarani unapumzika hata masaa mawili unaondoka.

Unataka kushusha mzigo unashusha na kuondoka hupuguziwi lakini hii nchi kila kiongozi yeye ni hakimu wa kuhukumu mfano jana nimetoka kampara nafika temboni kwenye parking nimeshusha maindi yangu linatokea lijitu linanida ushuru shilingi elfu moja ya uchafu nikaliuliza haya mahindi ni uchafu halikunijibu nikamwambia ok kama unahitaji pesa ya huu uchafu nilioshusha hapa nipatie lisiti halina linadai ushuru huku limelewa chakali naiomba sana Serikali itazame hawa watu wa TANROADS imefikia hatua mpaka matapeli wamejiingiza humo wanajifanya wao ni watu wa TANROADS.
 
Back
Top Bottom