BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
Dongo hili anapigwa Kikwete? Lakini kuna umuhimu wa kufahamishwa tangu aanza uVDG wake ameshaleta "wachukuaji" wangapi? wenyewe huwaita wawekezaji
Serikali itathmini safari za viongozi - Kigoda
na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya watu
SERIKALI imetakiwa kufanya tathmini ya faida za safari zinazofanywa na viongozi mbalimbali nje ya nchi kutafuta wawekezaji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali, Dk. Abdallah Kigoda, alisema hayo alipochangia mada kwenye semina ya wabunge kuhusu mwongozo wa kutayarisha mipango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/2009, iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Alisema kamwe Tanzania haiwezi kujikwamua kiuchumi kama haitakuwa na utaratibu wa kutathimini mipango yake pamoja na kuwashirikisha wananchi kumiliki uchumi wao.
Kigoda alisema ni vema ikafanyika tathimini ya wawekezaji waliokuja nchini tangu viongozi walipoanza kufanya safari za kuwasaka nje ya nchi.
Alisema bila kufanya hivyo taifa linaweza likajikuta linatumia fedha nyingi kuliko kile kinachopatikana katika ziara husika jambo ambalo ni hatari kwa ukuaji wa uchumi.
Tuanze kufanya tathimini ya safari zinazofanywa za kuwatafuta wawekezaji, ili kujua wamekuja wangapi na kama hawajaja ni kwa sababu zipi, alisema Kigoda.
Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir (CCM) alisema mipango mingi inayopanga na serikali imekuwa haitekelezeki na kila mwaka inapangwa mingine bila kuangalia mafanikio na hasara ya mipango iliyopita.
Alisema tatizo la wabunge kutokuhoji mafanikio na hasara ya mipango iliyopangwa miaka iliyopita imechangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa hali hiyo, hasa kwa watendaji wa serikali.
Mipango hii inakuwa kama moto wa makuti unawaka kwa kasi kisha unaisha mara moja na sisi wabunge hatuhoji kwa nini mpango fulani umeshindwa, alisema Mudhihir.
Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid (CUF), alisema ni aibu kwa Tanzania kuendelea kutegemea wahisani kusaidia bajeti, huku ina bandari tano ambazo hazitumiki ipasavyo.
Alisema kukosekana mipango thabiti na ufuatiliaji finyu ni miongoni mwa sababu zinazoifanya Tanzania kuendelea kuwa masikini siku hadi siku huku rasilimali za kuikwamua zipo.
Rashid alisema kufurika kwa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam ni aibu kwa nchi kwani kuna uwezekano wa kuboresha bandari nyingine na zikatumika na nchi ikapata mapato zaidi.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 5 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Mnh! Bosi Hamadi (Hamad Rashid),wafikiria serikali ya CCM yaweza kuboresha bandari kama ya Tanga ili watu wa huko nao waneemeke, mawe? Naam, kwa kuwekeza kwenye bandari tu Tanzania yaweza kukuza uchumi wake kiasi cha kuwa nchi iliyoendelea daraja la kwanza maana tumezungukwa na nchi tele ambazo hazina Bandari. Ikiwa Bandari moja tu ya Singapore imewafanya waendelee sisi bandari tano twazuizikalia tu!
na Al Assad, Sungai Pusu, - 31.03.08 @ 10:24 | #4276
JIBU: Viongozi wetu wengu hawaangalii maendeleo ya taifa bali posho zao.
Inaonekena hata madini yetu hatuna mpngo mahususi ya kizazi kijajo, akitokea huyo mwekezaji tunampa, hatuna mipangilio ya wapi tuchimbe leo na wapi miaka hamsini ijayo. Ni lile la chukua chako mapema tu!!
na kalumanzila - 31.03.08 @ 12:38 | #4307
Mudhihir aache unafiki, hivyo anaubavu wa kuhoji mambo hayo iwapo suala la msingi kabisa kwa manufaa ya taifa letu kuhusu madini, alikuwa mmojawapo aliyechangia kumsulubu kijana Kabwe kiasi kile! Leo ajidai kuwa anaweza kuhoji hayo kweli. Ama kweli mwanasiasa usimweke mdhamana.
na osmundo, Dsm Tanzania, - 31.03.08 @ 14:18 | #4326
Mimi namuunga mkono ndg osmundo kwamba mudhihiri ni mnafiki kwani ni sikunyingi hajasikika tokea apate ajali hivyo alitaka asikike kama bado angali yupo,tutamsikia kwani vikao vya bunge havipo mbali kuanza.Pia huyo kigoda alikuwa wapi siku zote asiseme hizo safafi za wakubwa zitathiminiwe ili kujua kama zina mafanikio au la akiwa waziri hakuyasema hayo kwa vile alikuwa akisafiri lakini tangu uwaziri umekwisha ameanza kuchonga aache hizo watanzania wa sasa sio wadanganyika bali waelewa tena zaidi ya yeye na, mangungu
na j.mangungu, Arusha Tanzania, - 31.03.08 @ 14:41 | #4339
Inafurahisha kumuona Mudhihir ameamka kutoka kwenye lindi la usingizi mzito ambapo kwake yeye lililokuwa kuu ilikuwa kulinda chama na si maslahi ya nchi.
Natarajia kusikia akihoji mambo hayo bungeni kwani hiyo ndiyo kazi ya Bunge: Kuisimamia na kuikosoa serikali.
Kigoda naye hakuwa hivi alipokuwa serikalini, ajabu kubwa!
Ila si mbaya. Kizuri ni kuwa wote wawili ama wametambua maana ya kuwa watanzania na wawajibikaji aidha kwa uzalendo au kutambua hawapati gawiwo pakiliwa.
na Danny - 31.03.08 @ 15:22 | #4349