Serikali itambue uwepo wa wanafunzi wasiosikia na kuona

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
SERA ya Taifa ya elimu inabainisha kuwa itatoa elimu kwa watu wote bila kujali upungufu wa wananchi wake hususan wenye ulemavu.

Uhuru wa kila Mtanzania kupata elimu ni haki yake ya msingi haijalishi amezaliwa na upungufu gani mwilini. Kimsingi Serikali inatakiwa impe elimu.


Sitaki kuamini kuwa Serikali inashindwa kutekeleza wajibu,kanuni na sera zake katika kuhakikisha kila mwananchi anapata elimu kwa usawa bila kujali upungufu wake.


Kuna makundi mengi ya walemavu baadhi ni kama walemavu wa kutoona, kutosikia,walemavu wa viungo na hata wasioona na kusikia kwa pamoja.


Kwa walemavu wasioona na kusikia, hawa wako wengi licha ya kuwa viwango vya ulemavu wao vinatofautiana.
Hata hivyo, inasikitisha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki, hakuna hata nchi moja yenye shule ya sekondari kwa ajili ya wanafunzi wenye aina hii ya ulemavu. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Sense International.


Hii inaonyesha walemavu hawa wanaishia darasa la saba na hapo ndio mwisho wao wa kujiendeleza kielimu.Huku ni kuwatenga wananchi hawa ambao ni sehemu ya Taifa hili. Sielewi sababu ya kuwapa mgongo wenzetu hawa.
Aidha, kwa mujibu wa shirika hilo, hakuna chuo chochote kinachotoa mafunzo kwa ajili ya walimu wa walemavu hawa.Kingekuwapo tungesema angalau walemavu hawa nao wanathaminiwa.


Ikumbukwe kuwa ulemavu ni upungufu tu wa kimwili, hivyo haujawa sababu ya mhusika kutengwa na kutotambuliwa na jamii yake.


Naziomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ile ya Afya na Ustawi wa Jamii, kutafuta namna ya kuwasaidia walemavu hawa kwa kuwapa elimu kama ilivyo kwa walemavu wengine.


Siyo jambo zuri hata kidogo kwa nchi yenye umri wa miaka 50 na hivi juzi tumesherehekea kufika hatua hiyo, huku tukishindwa kutambua uwepo wa watu wenye ulemavu wa aina huu ambao wanaonekana wamesahauliwa.


Kwa kila mwanajamii na anayeguswa na suala hili, huu ni wakati wa kuamka na kuwasaidia walemavu hawa.Kwa hali yao, watoto hawa wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwetu kama jamii.

Serikali itambue uwepo wa wanafunzi wasiosikia na kuona
 
Nikweli kabisa mkuu, cha ajabu ni miaka 50 sasa tangu tupate uhuru lakini ndugu zetu mpaka sasa wanateseka. kipindi cha uongozi wa Mwl. Nyerere wazo hili tayari lilikuwa limeisha anza kutekelezwa. ukifika pale musoma kulikuwa na shule ya msingi mwisenge ndugu zetu hawa walikuwa wakipatiwa elimu. latini shule hii imesahaulika na imechoka mpaka majengo. nadhani taifa/serikali lifikirie juu ya ujenzi wa complex schools atleast kila kanda kwa ajili ya kusaidia ndugu zetu hawa, ukweli ni kwamba wanateseka saana!
 
Back
Top Bottom