Serikali italinda Amani kwa Nguvu Zote - Dk Shein | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali italinda Amani kwa Nguvu Zote - Dk Shein

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, May 31, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Bara na Visiwani,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]


  Na Juma Mohammed, MAELEZO

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema kwamba Serikali italinda amani kwa nguvu zote na kuonya kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua watakaochochea na kufanya vurugu.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu Zanzibar, Dk. Shein alisema “Tutailinda amani kwa nguvu zote, atakayethubutu kuchezea tutamshughulikia kwa mujibu wa sheria”

  Rais Shein alisema amesikitishwa sana na vitendo vilivyotokea wiki iliyopita na kuelezea vurugu hizo zimeharibu sifa njema ya Zanzibar ambayo kwa miaka mingi ianjulikana kwa uvumilivu wa kidini kiasi cha hata Serikali ya kikoloni mwaka 1953 kuamua kufanya shindano la uchoraji wa stamp ya uvumilivu wa kidini.

  “Kwa masikitiko makubwa nataka kusema kuwa vitendo vilivyotokea vya kuvunja amani ni vya aibu, vimetusononesha sana na haya wananchi lazima wajue kuwa amani yetu ni muhimu kuliko jambo lolote lile” Alisema Rais Dk. Shein.

  Alisema ameshangazwa na vitendo vya uchomaji makanisa moto vilivyofanywa wiki iliyopita akihoji kwamba kulikuwa na uhusiano gani baina ya Muungano na makanisa “Mie nilikuwa nashangaa sana hivi kuna uhusiano gani kuzungumzia Muungano na kuchoma makanisa,kupora mali za watu” Alisema Dk. Shein.

  Rais Dk. Shein alisema matatizo ya Muungano yanashughulikiwa chini ya utaratibu uliokubaliwa na Serikali mbili, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kuna kamati ya kushughulikia kero za Muungano na hadi sas kuna mambo 12 yanafanyiwa kazi ikiwemo suala la mafuta na gesi asilia.

  “Taratibu za kutatua kero za Muungano zinaendelea, kuna mambo 12 yamewasilishwa katika kamati na yanafanyiwa kazi, miongoni mwa hilo ni suala la mafuta na gesi asilia, sisi tumeshaamua, SMT bado haijaamua ,lakini sisi tumeamua kuyaondoa katika Muungano, lakini nasema ndugu wawili hawagombani…tutakubaliana” Alisema Rais Dk. Shein.

  Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao na akielezea kuw ahiyo ni fursa muhimu kwa Wazanzibari kueleza wanataka katiba iweje na kuwatoa wasiwasi kuwa hakuna atakayetishwa na wasiogope,lakini akasisitiza ni lazima wasubiri Tume ndipo watoe maoni yao maana wakieleza sasa hakuna anayawasikiliza.

  “Wanaotoa maoni yao kuhusu Muungano kwa hivi sasa wanapoteza muda wao, ni sawa na kusema na ukuta tu kwani hakuna anayewasilikiza, hakuna anayechukuwa maoni yao maana Tume haijaanza kazi,wasubiri itakapoanza wakatoe maoni yao” Alisema Rais Dk. Shein.

  Rais Dk Shein alitoa ufafanuzi huo akijibu swali la waandishi waliohoji kuwepo kwa kamati ya kutatua kero za Muungano na mjadala wa katiba mpya kwamba Serikali ingesubiri matokeo ya Tume ya Katiba kuhusu Muungano maana inawezekana mambo yakabadilika.

  “Sheria ya Tume ipo wazi, lazima wafuate sheria na taratibu hatazuiwa mtu kutoa maelezo yake,lakini kero za Muungano zinaendelea kushughulikiwa kuwepo kwa Tume ya Katiba hakuzuii kamati iliyo chini ya Waziri Mkuu na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kushughulikia kero za Muungano.

  Katika hatua nyengine, Rais Dk. Shein ameipongeza Polisi kwa busara na hatua walizochukua kushughulikia vurugu zilizotokea wiki iliyopita Visiwani Zanzibar ” Nilipopigiwa simu nikauliza kuna alijeumizwa,vifo nikaambiwa hakuna nikasema Alhamdulillah salama” Alisema Dk Shein.

  Alisema kwamba licha ya Polisi kuchokozwa na vijana waliokuwa wakichoma moto matairi ya magari barabarani, kuweka mawe na magogo kuziba njia,lakini Polisi ambao walikuwa na silaha hawakutumia silaha hizo,zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi.

  ”Jeshi la Polisi halibebi lawama,linastahili sifa na kupongezwa…Polisi wana busara sana wanafanya kazi vizuri hawa ndugu zetu wa Polisi kwa kweli lazima tuwapongeze” Alisisitiza Rais Dk. Shein wakati akijibu swali kwamba Polisi wanastahili kulaumiwa, Rais alisisitiza kuwa Polisi walitimiza wajibu wao kwa uzalendo mkubwa wa kuepusha madhara kwa jamii.

  ”Mimi nilikuwa natoka mazikoni, nilipita barabara ya amani,mwanakwerekwe, nimejionea namna vijana walivyoweka mawe,magogo, kuchoma matairi,lakini Polisi hawakutumia nguvu zaidi ya kuwatawanya kwa kutumia mabonu ya machozi, tuwapongezeni Polisi wetu wamejitahidi sana” Aliongeza.

  Rais Dk Shein alisema kwa wale wote waliokamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, haki itatendeka kwa kila mtu na kwamba hakuna atayakeonewa wala kudhulumiwa. Pia alisema Serikali inafanya tathimini kuweza kuelewa athari za matukio yaliyotokea. Pia alitumia fursa hiyo kuwapa pole wale wote waliopatwa na matatizo ya vurugu zilizotokea.
   
 2. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,939
  Likes Received: 1,476
  Trophy Points: 280
  Huyu mheshimiwa anaonekana kuongea kwa hekima sana,sasa sijui kama wanaoelezwa wataelewa!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Dr kajitahidi sana anafaa kuongoza waZanzibar milele.
   
 4. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ngoja nikapande boti. Imani yangu ndogo sana kuhusu haya mambo. Maneno ya busara sana. Kuna kitu ndani ya muungano hii movie ni ndefu sana.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katika taarifa yao ya habari usiku huu Chanel10 wameiminya habari ya mkutano wa Dr Shein kuhusu ghasia huko znz. Mtangazaji aliitaja lakini clip haikutokea na akaomba radhi kwa hitilafu ktk mitambo hivyo clip ingekuja baadaye na hapo hapo akaleta habari za JK na mkutano wa AfDB.

  Hata hivyo mtangazaji alimaliza habari za kitaifa bila kuileta clip hiyo ya Dr Shein. Kuna nini hapa?
   
 6. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Yes! Tunahitaji kauli njema kama hizi. Hongera Dk. Shein!
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mods, nisaidie kuondoa hii thread kwani hatimaye mwishoni kabisa Ch10 waliileta habari hiyo.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Pumba tu Ngoja tuendelee kuwa tawala hao wazenji chezea bara wao
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KERO ZA MUUNGANO NA PALE WALIKOKWAMIA CUF NA CCM KULE VISIWANI, CHADEMA WANALO JIBU TENA MARIDHARA KWA TAIFA ZIMA BARA NA VISIWANI - SERIKALI ZA MAJIBU ZINAZOKUTANIA TU KWENYE SERIKALI YA SHIRIKISHO

  THINK-TANK ya CHADEMA ifanyeni Homework yenu vyakutosha juu ya sekeseke za Tanzania Visiwani. Japo yanayoendelea huko ni UCHURO lakini si kweli kwamba yote ni uchuro mtupu.

  Yapo Madai ya kweli kabisa walioainisha hawa wenzetu wa kikundi cha uamsho ambayo CHADEMA lazima tukayatafakari na kuyatafutia majibu ya kuridhisha.

  Kweli ni chukizo ajabu Wabara kufukuzwa kama mmbwa koko Visiwani, Wakristo na Ukristo kuwindwa kama swala porini lakini a Good Thinker ni sharti aende mbele zaidi ya hapo na kujiuliza kwamba tumefikaje hpo kwanza. Tathmini yangu juu ya madai ya Wazanzibari kupitia mihadhara ya Wana-Uamsho ni pamoja n haya:

  1. Wenzetu ni kundi kubwa la watu waliofikiwa pomoni na matatizo lakini WAMEKOSA PAKUWASIKILIZA BILA UNAFIKI;

  2. Adui mkubwa ya WaZanzibari iliowafikisha hadi hapo pa kuona aheri wakatae jumla hata na hako Ka-Muungano ni UMASIKINI WA KUPINDUKIA katikati yao;

  3. Kwa matokeo ya Serikali ya sasa ya Umoja wa Kitaifa kati ya Makada wa CUF na CCM, WaZanzibari wengi wanajihisi KUSALITIWA MAANA HAWAJAONA CHOCHOTE KILICHOBADILIKA KATIKA MEZA YAO wala mlo kuongezeka kitu kwao isipokua tu baadhi ya viongozi wachache tu na maswahiba wao kujineemesha katika vyama vya CUF and CCM.

  Ujanja ujanja huo uliochezwa na ile 'Kamati ya Makamba / Maalim Seif' kwa WaZanzibari, kwa mujibu wa tathmini yangu binafsi, ndio kiini cha EXPLOSION OF VIOLENCE in the Isles.

  The two parties seem to be hidding their heads on the sand about the GENUINE STRUCTURALLY BIASED SOCIO-ECONOMIC PLIGHTS of the Islanders down there, which may in some days culminate into 'SOMETHING WORST' than what we witnessed a few day ago, AN IMMEDIATE AND RATHER SOFTER 'COMMON-ENEMY' to pelt-off their time-long angers so subconciously occurred to be CHRISTIANS AND ANY OTHER THING THAT STANDS FOR CHRISTIaNITY in the island.

  In a sense, my independent analysis gives me that Christians and Mainlanders in the Island were merely VICTIMS OF CIRCUMSTANCES of a most suffocating public that do not even know who exactly to lament to yet silence is never any warmer a seat home for them with the daily increasing poverty-biting on their back-curved empty bellies. The cite cases of:

  i. Roads in pathetic conditions as Mainlanders are currently going for a a-five-lane double road;

  ii. Zaini and other numerous industries being magnetically pulled to Dar vacating their neighbourhoods as we cry foul in Dar for factories errected in residential places ;

  iii. A miserably Inome inequality and poverty to the extent that an individual fundraiser exercise for a mere Tsh 300,000/- for hospitalisation would demand an effort of visiting over 60 Mosques but without any success;

  iv. Double-taxation of both Island and mainland TRAs becomes a most deterring factor for both home nd foreign investments to them

  v. And a host of other socio-economic factors all add up to Zanzibaris TOTAL AND POINTEDLY UNREASONED REJECTION of the presence of the Union Government.

  NB: Kutokana na baadhi tu ya haya maoni toka Unguja na Pemba, mimi kama mwanachama wa CHADEMA, napendekeza hivi sasa kwa uongozi wangu Taifa ichukue hatua mara moja kwa kuunda KIKOSI-KAZI CHA MALALAMIKO JUU YA MUUNGANO - ikapate kufanya kazi ndani ya siku 21 kuongea na wananchi (si kikundi cha Uamsho) mashinani kuwatafuta maoni nini malalamiko yo Juu ya Muungano (WaTanganyika kwa WaZanzibari kupitia random sampling) na tiba gani wanaiona kwa ajili ya KUBORESHA NA WALA SI KUVUNJA MUUNGANO.

  Mara baada ya ripoti hiyo kuwekwa pamoja, CHADEMA ishirikishe wadau mbalimbali juu ya mambo walioypata kutoka kwa wananchi mashinani, kuwaomba nao wadau hao maoni zaidi KISHA RIPOTI ITAKAYOKUA IMEBORESHWA NA WADAU kwenye maoni yale ya mashinani sasa ipate kupelekwa KAMATI KUU YA CHAMA CHETU kuijadili kiundani zaidi na zaidi kisha kutoa jibu la kisera kichama juu ya nini kifanyike kKUNAWIRISHA 'MUUNGANO' kwa faida ya taifa zima na wala si WaZanzibari peke yao.

  Katika hatua hii ndio muda mwafaka sasa CHADEMA kuteremsha Sera yake juu ya Muungano na kusaidia wananchi pale ambapo CCM na CUF wao walishindwa na kuamua kuitana kishikaji kwenda kula mabua pamoja kwenye jukwaa linaloitwa SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA Zanzibar isiokua na tija yoyote kwa wananchi wa kawaaida.

  Remember, it is always during a time of IMMENSE NATIONAL CRISIS AND CONFUSION like this ndipo COOL-MINDS hutambulika hata bila kujinadi huko mitaani kwa vyeo uchwara, kujichukulia japo ka-sekunde kufikiri kwa faida ya taifa hata kama wengine wasiopenda badadiliko waamua kumbandika jina eti mhaini.

  Do something now CHADEMA; we can be a party to offer permanent solutions to age-long challenges where everybody seems to be shivering their spinal-cords off as they water their pant for mere inability to FIND OUT THE RIGHT THING TO DO without escalating any further blood-letting scenes in our neighbourhood!!

  Wenu UWEZO TUNAO.

   
 10. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wazanzibar wanamuangusha ana huyu Presdaa jamaa ana hekima sana sasa watawaliwa hawataki hekima
   
 11. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 60
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema Asiyeutaka Muungano Akae Pembeni. Amesema serikali itafanya tathmini ya hasara zilizotokea na Hatua za kuchukua.
   
 12. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Mumefurahishwa nae kwa sababu kasema in short muungano usikuswe na watu wasubiri kutowa maoni katika katiba?.

  Huyu pumba yote kwenye katiba mpya wazanzibar wanayo katika katiba yao ,watanganyika ndio wakuhitaji kuwa na tanganyika yao na kurudi kwa katiba yao.

  Wazanzibar hawahitaji katiba wanahitaji kujuwa hatma ya muungano huu uite wa tanzania na zanzibar au?
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Dr. kawajibu wale waliotaka waznz wauwawe na polisi ili eti waone polisi inafanya kazi.

  Ila la kutawala milele naona una lako jambo
   
 14. Z

  ZIGZAG Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  uyu prisident sio msemaj wa mapolisi sio amir jeshi.
   
 15. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ngoja nikaperuse kidogo mzalendo.net...nahisi nitayaona 'mapovu' hata kwenye screen!
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Katoa bonge la speech binafsi nimemkubali nimtu mwenye uwelewa mkubwa na mstaarabu kwa kweli
   
 17. blea

  blea JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Dr kaongea kwa busara na hekima sasa je hawa jamaa wanamwelewa kweli? Tatizo hapa si KATIBA bali ni kero za muungano na umaskini uliopindukia unaolikumba taifa ndio maana hata wakiambiwa wafanye kitu cha kijinga kama walichokifanya watafanya kwani wameshachoka na hali ngumu bila kutafakari imetokana na nini wao wanajipa jibu jepesi kuwa ni wabara makanisa sijui muungano. zinahitajika busara kuwakabili watu waliochoka na jambo ambalo wao wanaamini ni jepesi kulitatua kumbe sio
   
 18. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama misingi ya amani imevunjika, ni amani gani inayolindwa hapa. Amani ni matokeo na si bidhaa unayosema uaweza kuilinda. Kwani vurugu zilipokuwa zinaanza siku zote who showed concern. Watakapoanza kuchoma ofisi za serikali ndipo wataamka maana kwasasa uchomaji wa nyumba za ibada inaonekana hakuna anayejali. Hivi kwa yote yaliyotokea siku zote hizo leo eti ndio raisi anakuja kutoa matamko ya kusema atalinda amani.
   
 19. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ktk taarifa ya habari ya Itv ya saa 2 usiku nimesikitishwa sana na docta sheini kuseama kwamba serikali ilikuwa ina waona tangu mwanzo kikundi cha uamsho!. Swali je kama walikuwa wanaona mienendo yao tangu mwanzo iweje wasikipige marufuku hicho kikundi?. Na je kwa nini serikali iseme kuwa walikuwa wahuni! je hicho kikundi ni cha wahuni? Kama ni wahuni iweje mhuni akapema kibali cha kuhubiri dini ya kislam? Na je kwa nini hawatajawa hao wahuni waliochoma makanisa?

  Naanza kuamini wahusika wakuu ni wa uchomaji wanaweza kuwa ni SERIKALI YA ZANZIBAR.
  Wakishirikiana na kikundi cha UAMSHO.

  Kama serikali ya zanzibar haitawataki kwa uhaini hawa wanaoitwa wahuni sisi wa KRISTO
  hatutakuwa na imani na smz.


  Bangoo Rimoy
  box
  ARUSHA
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]JK,Shein in crisis meeting
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 30 May 2012 22:44
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  By Mkinga Mkinga
  The Citizen Reporter
  Zanzibar.

  The President of Zanzibar, Dr Mohamed Ali Shein, yesterday travelled to Dar es Salaam for a crucial meeting with President Jakaya Kikwete in the wake of the weekend disturbances in the Isles that have largely been blamed on socio-religious zealots. The meeting called by President Kikwete comes only a day after some people questioned the silence of top national leaders in the face of a crisis they widely described as "very serious".

  In the trip to Dar es Salaam, Dr Shein was accompanied by the CCM deputy secretary general (Zanzibar) Mr Vuai Ali Vuai.Minister of State in the Second Vice President's Office Mohammed Aboud confirmed that Dr Shein travelled to Dar es Salaam for a crucial meeting called by the Union President.

  Mr Aboud told a clergymen's meeting here yesterday that the Zanzibar President had left Zanzibar for a meeting in Dar.Meanwhile, Christian religious leaders meeting here yesterday issued a statement, in which they accuse the Shein administration of not taking appropriate action that would have prevented "recurrent attacks on church buildings and church properties".

  Reading the statement on behalf of his colleagues, the head of the Anglican Church in Tanzania (ACT), Bishop Valentino Mokiwa, said Christians were nearing the upper limit of their tolerance over the government's lack of action against people who have been attacking churches.

  He noted that since 2001, some 25 churches have been torched in Zanzibar but no single culprit has been punished for the crime.

  And when contacted to clarify whether President Kikwete has called for a meeting with his Zanzibar counterpart, director of communication in the President's Office, Mr Salva Rweyemamu could only say there was no need of doubting the minister's (Aboud's) statement.

  "Why should you doubt the statement delivered by a government minister? I urge you to rely on Mr Aboud's statement… you should quote him as the right source," Mr Rweyemamu said.

  Mr Kikwete, who was in Arusha on Tuesday evening returned to Dar es Salaam and was yesterday engaged in various official activities including the meeting with Zanzibar leaders.

  Reacting to concerns that Dr Shein's silence on the weekend chaos was disturbing, Mr Aboud said the Isles' head of government was closely monitoring the situation and he would ultimately issue a statement.
  "You never know; maybe after he's done with his Dar es Salaam trip, he will deliver a statement on the position of his administration but for the time being we, his aides, are doing our best to restore peace here… it is improper for the President to rush into issuing statements whenever anything happens," he said.

  Because of the Dar es Salaam trip, the bishops, who had wanted to have an audience with Dr Shein, failed to do so; neither could they see his second-in command, Ambassador Seif Idd, who was said to be abroad.In their statement, the bishops blamed the Zanzibar government for not doing enough to protect Christians in the Isles.
  Their statement was drafted during a daylong meeting at Kariakoo, where the clerics discussed the destiny of Christianity in Zanzibar following the recent attacks that targeted churches.

  The bishops' delegation, led by the head of Anglican Church in Tanzania, Dr Valentino Mokiwa, was received by the Minister of State in the Second Vice President's Office, to whom they delivered their message.

  Said Dr Mokiwa: "We've come to give to Dr Shein our position on the chaos…at least 25 churches have been burnt since 2001 but nothing has been done by the government and nobody has been taken to court over the incidents."
  Dr Mokiwa told Mr Aboud that had they met Mr Kikwete or Dr Shein, they would have delivered the same strongly worded message because their patience had been overstretched.

  "We've been tolerant for a long time… and now we are saying: enough is enough," said Dr Mokiwa.
  He said Christians in Zanzibar live as second-class citizens in their own country, adding that they are tired of that situation and if the government has failed to protect them, it should say so, so that they could look into how they would protect themselves.

  Additional reporting by Florence Mugarula
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...