"Serikali itafanya kila linalowezekana kuwatafuta samaki wote walioingia sokoni mpaka wapatiakane" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Serikali itafanya kila linalowezekana kuwatafuta samaki wote walioingia sokoni mpaka wapatiakane"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Penguine, Jul 28, 2011.

 1. P

  Penguine JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Jamani baadhi ya hawa Mawaziri wetu wanataka kutupeleka wapi na kauli zao Bungeni? Jana nilimsikia Naibu Waziri- Kilimo na Chakula akiliarifu Bunge juu ya hatua za Serikali kufuatia Sakata la Samaki wanaosadikika kuletwa hapa nchini kutokea Japani wakihofiwa kuingiwa na mionzi ya nyuklia ambayo ni hatari kwa afya za viumbe hai.

  Naibu waziri anasema Serikali imechukua hatua ikiwa ni pamoja na kuzuia mauzo zaidi ya samaki hao na kufanya kila linalowezekana kuhahikisha samaki walioingia sokoni (yaani walionunuliwa na wauzaji mbalimbali na walionunuliwa na walaji pia kwa maana hiyo) wanapatikana!

  Jamani hivi utawapataje samaki walioliwa kama siyo utani mjengoni? cha ajabu zaidi wapo waheshimiwa humohumo Bungeni waliokuwa wakiipigia makofi kauli hii isiyotekelezeka na yenye kukosa umakini.

  Ushauri: Dear Serikali jaribu kuwa makini na kauli zako kwa umma hata kama wabunge waliowengi mjengoni wameamua kukukubalia udanganyifu wako.
   
 2. TabletFellow

  TabletFellow JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa kama wameshaliwa watawakamua watu matumbo?? au kwenda kukusanya vinyesi na kuunganisha??

  kauli za wanasiasa hazina tofauti na maneno ya kwenye khanga
   
Loading...