Serikali isiyokidhi matakwa ya wananchi ni haki ya wananchi kuiondoa hata kwa maandamano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali isiyokidhi matakwa ya wananchi ni haki ya wananchi kuiondoa hata kwa maandamano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shayu, May 24, 2011.

 1. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #1
  May 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Pale serikali inaposahau majukumu yake kwa wananchi, wananchi wanajukumu la kuikumbusha serikali kwa njia mbalimbali, njia moja wapo ni njia maandamano.

  Ni haki ya kimsingi ya kila raia kuandamana kuelezea hisia na kuikumbusha serikali majukumu yake, Serikali haina haki yeyote ya kuzuia maandamano ya raia huru walio katika nchi yao wenyewe, jukumu la serikali ni kusikiliza malalamiko ya wananchi na kuyashughulikia, Serikali haiko juu ya wananchi ila wananchi wana mamlaka dhidi ya serikali yao, kwakuwa wao ndio walioichagua iwaongoze, Wana haki ya kimsingi ya kuiwajibisha ikiwa haitimizi matakwa ya raia waliowengi.
  Je swali ni njia mbadala na suluhisho la matatizo yetu?

  Pale serikali inaposahau majukumu yake na kujiingiza katika vitendo vya rushwa na ufisadi, kujiingiza kujilimbikizia mali na kufanya biashara na kushindwa kuangalia matatizo ya kimsingi ya raia, kushindwa kulinda haki za watu, pale ambapo rasilimali za nchi na utajiri unamilikiwa na wachache hasa wakiwa viongozi huku raia wakijua utajiri huo umepatikana mara tu walipoingia kwenye uongozi, raia wanaweza kuhisi wamesalitiwa na serikali yao wenyewe na kuingia barabarani kuandamana kuipinga serikali yao wenyewe, hii imetokea katika nchi za uarabuni, nchi za mashariki ya kati pamoja na Egypt na Libya, Ilitokea pia kwenye mapinduzi ya ufaransa.

  Raia wowote sehemu yeyote duniani wana haki ya kuondoa serikali yeyote ili dhalimu isiyojali wananchi waliowengi na kuiweka serikali nyingine ambayo itatimiza matakwa ya wananchi , italeta matumaini kwa watu na mwelekeo wa taifa.

  Ni haki ya kimsingi ya raia yeyote Yule mzalendo anapoona nchi yake inakosa mwelekeo kupiga hatua moja mbele ya kimapinduzi ikiwa serikali inayowaongoza haisikilizi matakwa ya wananchi na kama wanakwamishwa kimaendeleo na serikali iliyopo madarakani, Watu wenye hamu ya maendeleo wana haki kupiga hatua moja mbele ya ukombozi wa taifa lao wenyewe, Njia mojawapo ya kuelezea hisia hizi ni kupitia maandamano, Kuelezea hisia zao kwa serikali iliyopo madarakani ili kuleta mabadiliko yenye faida kwa watu wote sio kikundi kidogo cha watu na kama serikali isiposikiliza wananchi, wananchi wana haki ya kuiondoa madarakani.
  Je maandamano ni suluhisho la matatizo yetu? Lazima tujiulize matatizo ya taifa hili na chanzo chake ni nini? Kwanini watu wanaandamana?
  Je ni kweli serikali imeshindwa kutatua matatizo ya watu wake mpaka wanafikia hatua ya kuandamana?
  Maandamano ni moja ya dalili za raia kukosa imani na serikali juu ya uwezo wake kutatua matatizo ambayo yanawakabili raia,
  Raia wanapokosa njia nyingine mbadala ambayo matatizo yao yanaweza kusikilizwa njia pekee ni kwa wao ni kuandamana kuelezea hisia zao na hasira zao kwa serikali inayowatawala.

  Kwa vyovyote vile maandamano mara nyingi hutokea hasa kwa serikali ambazo hazijali raia wake, serikali za kifisadi, zilizosahau majukumu yake kwa raia na kunyonya mali za umma, wakiishi maisha ya kifahari na kuacha raia wengi maskini wa kutupwa, wakati tabaka la viongozi wao wakiwa matajiri na kujinufaisha na mali ya umma, hii hupelekea wananchi kuhisi wanasalitiwa na kuandamana kutaka kufanya mapinduzi, ni haki yao kama serikali imewasaliti, kuandamana na kuelezea hisia zao, kwamba tumewatuma mtuongoze, mmetubadilikia, Kwamba tulihitaji maendeleo kwa wote lakini ndugu zetu viongozi mnakuwa matajiri haraka haraka wakati sisi tuliowatuma ni maskini wa kutupwa na huduma za kijamii kila siku zinaendelea kuwa duni, Elimu inaendelea kudorora, huduma za afya, umeme mgawo kila siku, maji na uzembe mwingi unaosababisha vifo vya watu, Raia wanapoona serikali imekosa umakini katika kuwaongoza mara nyingi huchukua hatua ya kuandamana ili kuelezea hisia zao kwa serikali inayowaongoza.
  Hali inapokuwa mbaya zaidi hupelekea machafuko kutokea hasa pale hali ya maisha inapokuwa ngumu kutokana na mfumuko wa bei na ukosefu wa ajira unaotokana na serikali ambayo haiwajibiki ipasavyo kwa raia wake bali inajali starehe na anasa na kushindwa kuongoza nchi kwa umakini na kumiliki raia wake wenyewe, hivyo raia kupoteza matumaini kwa nchi yao wenyewe na kwa viongozi wao, ikifikia hali hii raia hawasikii chochote wanaingia barabarani kuandamana hata mtutu wa bunduki hauwezi kuwazuia, Serikali inapokosa umakini ina hatarisha amani ya taifa nzima, serikali inaposhindwa kusimamia haki, kuhakikisha kuna ustawi katika jamii, inaposhindwa kuondoa rushwa na ufisadi wananchi wanakuwa hawana jinsi yeyote isipokuwa kuandamana na kuelezea hisia zao.

  Kwahiyo maandamano ni njia ya kuelezea hisia za wananchi kwa serikali yao, kama serikali ikiwa sikivu inaweza kufanya mabadiliko ili kukidhi matakwa ya raia hivyo hapa maandamano yanaweza kuwa ni suluhisho kwa matatizo yao kwakuwa serikali imewasikiliza baada ya jitahada za kawaida kushindikana na wao kufanya maandamano ili kushinikiza serikali kufanya yale ambayo wanafikiri ni haki yao kama raia kufanyiwa. Kawaida serikali makini haiwezi kusubiri mpaka maandamano ili kuweza kusikiliza matakwa ya wananchi, serikali makini siku zote macho yao na masikio yao yako katika kuhudumia wananchi bila kusukumwa ila serikali za kibwanyenye na kifisadi lazima zisukumwe kwa maandamano.

  Lakini pia maandamano yanaweza kutokea tu, kutokana na hasira ya raia kwa serikali yao kama serikali yao imepotoka na kuwa ya kifisadi isiyoangalia maisha ya raia wake na kujiingiza katika maisha ya kifahari na anasa huku siku baada ya siku maisha ya watu waliowengi kuwa ya dhiki kupindukia, raia wanaweza kuingia barabarani tu, na mapanga na marungu kama wamechoshwa na ujinga wa serikali yao. Ni muhimu kwa serikali kuwa makini katika kuhudumia raia wake waliowengi, ni muhimu kwa serikali kulinda na kuheshimu haki za watu, Ni muhimu kwa serikali kulinda kusitokea matabaka makubwa katika nchi yetu kati ya walionacho na wasionacho.

  katika nchi yetu tunashuhudia watu waliopewa uongozi wa nchi, wafanya kazi wa taasisi taasisi mbalimbali wakiwa matajiri wakubwa, tunajiuliza, tofauti kubwa hizi za kima tabaka zinatokana na juhudi za watu katika kufanya kazi kweli au watu waliopewa majukumu ya kutumikia watu wa nchi hii kuwa wasaliti na kuwaibia raia ili kujinufaisha wao binafsi?

  Raia walio wengi wakiona na wakiamini wamesalitiwa lazima wataingia mabarabarani kuandamana kupinga hali yao ya ufukara na utajiri wa kupindukia wa viongozi wao. Kwakuwa wao kwa pamoja kama wananchi kama raia wa nchi hii walijivua mamlaka na dhamana zao na kuwapa viongozi wawaongoze ili kulinda haki na kuleta ustawi kwa watu wote, Viongozi kwa kufanya jambo lolote lililo kinyume cha ustawi wa jamii ni usaliti unaopelekea watu kuandamana.
  Kama raia wanakandamizwa na serikali yao, wananyimwa uhuru wao wa kujiamulia mambo yao wenyewe, kama raia wakichoshwa na ahadi za mara kwa mara za serikali yao zisizotekelezeka, raia wanaweza pia kuwa na hofu na umakini wa serikali yao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili hivyo kukosa imani na serikali yao na mapenzi kwa taifa lao.

  Maandamano ni kiashiria cha matatizo ambayo jamii inayo na inafikiria serikali haijachukua njia madhubuti ya kukabiliana nayo, Raia hawawezi kutoka barabarani kuandamana bila sababu za msingi bila madai ya msingi, maandamano ni njia ya kuelezea hisia za wananchi kwa serikali yao, wananchi hawawezi kukaa tu wanapoona mambo hayaendi sawa kama serikali yao haiwajibiki kwao lazima wataandamana.
  Maandamano huikumbusha serikali majukumu yake, kama njia ya kuleta mapinduzi yatakayoleta mabadiliko katika taifa,Wananchi wanaweza kuingia mabarabarani kudai katiba mpya kama katiba iliyopo ina mapungufu yanayowapa kikundi cha watu wachache mamlaka makubwa dhidi ya waliowengi, kama katiba ni ya kibaguzi na inawanyima wananchi haki zao za kimsingi na uhuru wao, na kama harakati za kawaida za kudai marekebisho ya kikatiba ili kujenga jamii bora zaidi, iliyo huru na inayotenda haki imeshindikana, wananchi wanawajibu huo wa kuingia barabarani na kuandamana kudai haki zao za kimsingi na uhuru wa kama raia, ni haki yao ya kuzaliwa kudai uhuru na maisha bora zaidi kama serikali inayowatawala haiwajibiki ipasavyo.

  Kwa kawaida maandamano yanaambatana na madai kama madai ya waandamanaji yatafikia malengo basi matatizo ambayo yanawakabili wananchi yanaweza kutatuliwa, lakini mara zote maandamano huwa njia ya mwisho kabisa baada ya njia nyingine kushindikana, tumeona sehemu nyingi duniani maandamano yakipelekea kubadilishwa kwa katiba, kuleta mapinduzi katika nchi na kubadilishwa sheria kandamizi ambazo ziko kinyume na haki za binadamu, sheria za kibaguzi katika marekani dhidi ya watu weusi na katika afrika kusini, Unapoonewa lazima unyayue sauti yako juu ama sivyo anayekuonea hato kupa uhuru wako hato kurejeshea heshima yako, haki yako na utu wako, ni lazima watu wanaoonewa sehemu yoyote ile wapige hatua moja mbele na kunyanyua sauti zao kupinga maonevu na unyanyaswaji unaofanywa na serikali za kifisadi popote pale duniani, kwa maandamano na mabango na hutuba za kukemea wizi, udhalimu na ukandamizaji unaofanywa na serikali zisizojali maslahi ya umma. Pasipo kufanya hivi taifa lolote lile halitopiga hatua mbele katika democrasia na uwajibikaji wa serikali kwa raia wake.

  Mwisho serikali na jeshi la polisi halina haki ya kuzuia maandamano ya raia wanaodai madai ya kimsingi kutoka kwa serikali yao, wanapodai mabadiliko kwenye nchi yao wenyewe, kutumia jeshi la polisi kuzuia sauti za umma zisinyanyuke dhidi ya udhalimu wa serikali yao wenyewe ni udikteta na uonevu mkubwa, wananchi wana haki ya kuiondoa na kuiweka serikali yeyote ile wanayoitaka, kwa kuwa mamlaka ya serikali yetu kikatiba ni lazima yatokane na umma hata kama uchaguzi haujafika wananchi wakichoshwa na upumbavu na ujinga wa serikali unaopelekea usalama wa nchi na raia kuwa hatarini, unapopelekea hali ya kiuchumi na maisha kuwa magumu wana haki ya kimsingi kuiondoa serikali hiyo na kuiweka serikali itakayowajibika kwao na kuleta , umoja na maendeleo kwa watu wote.
   
 2. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #2
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Tafakari kuhusu maandamano na wajibu wa kiongozi kwa raia.
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, hii ungeongea na Said Kubenea, akupe ukurasa mzima katika Mwanahalisi
   
 4. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #4
  Sep 24, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  naona umeweka picha ya mwanaharakati hapo juu ni mmoja wa my favourate.
   
 5. Shayu

  Shayu Platinum Member

  #5
  Dec 1, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 180
  Nairudia hii ni muhimu kwa somo la uraia na haki za kila mmoja dhidi ya serikali yake.
   
Loading...