Mkuu,kama wewe unaweza kuvaa barakoa kila mahali na kukaa ndani kaa.,kama unasubiri kuambiwa ujilinde ndio ujilinde karagabaho.Tusilazimishane kujilinda,kila mtu ashinde mechi zake.
Nadhani kuna haja ya kuwaambia Magufuli, Majaliwa, Gwajima na Ndugai kwamba tutawashitaki ICC kwa kusababisha kimakusudi vifo vya Watanzania wakati wakiwa na uwezo wa kuvizuia.

Wanachofanya viongozi wetu ni kuwanyima wananchi haki ya kuendelea kuishi huku wakiwa na uwezo wa kuzuia vifo vyao. Hii ni pamoja na kuzuia kuja nchini kwa chanjo za Covid-19. Lazima wakikishwe ICC.
 
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?....
Mbona wewe hujafa sasa
 
mkuu Kwanza punguza woga kikubwa unafahamu taratibu za kujikinga ni vyema ukazi zingatia
Hapana, mi nadhani tahadhari ya mtoa mada ina mashiko. Bila kuwaambia watu wote kama ilivyokua mwaka jana, usitegemee watu wa kawaida kuchukua tahadhari, na hilo ni jambo la hatari. Hivyo kuwapa elimu wananchi wote ni jambo bora na jema kuliko kila mmoja kujilinda kivyake, kwani ikitokea hii strain ikasambaa hadi kwa wananchi wengi wewe huoni ni hatari?!
 
Kwa serikali inayoweza kummiminia mwananchi wake 31bullets, kwa lengo la kuchukua roho yake. Sidhani kama kuiangalia Covid_19 ikiteketeza mamia ya raia ni jambo la kushangaza. Cha msingi ni kwamba suala la kumuongezea KAYAFA muda haliathiriki kwa njia yoyote ile.
 
Mie ni msomi na mwenye uelewevu wa mambo, lakini bado ninaweza kuathiriwa na kutokuwapo kwa mkakati wa serikali. Lakini pia najua kuna Watanzania wengi tu ambao wanakufa kwa kukosa maarifa katika kupewa uongozi na kutokuwapo mkakati wa serikali katika upambana na Covid-19. Kwa hiyo ni shauri yao?
Umenena vyema na kiungwana sana. Sasa naunga mkono hoja yako
 
Wengi wa wale wenye access ya vitu vingi vizuri kwenye maisha tunayoishi ikiwa ni pamoja na wasomi na wafanyabiasha wakubwa ndio wengi wao wanapata shida ya upumuaji na homa ya mapafu

Sijui hivi vitu vinahusianaje😇
Mungu tunusuru watu wako 🙏
 
Mkuu,kama wewe unaweza kuvaa barakoa kila mahali na kukaa ndani kaa.,kama unasubiri kuambiwa ujilinde ndio ujilinde karagabaho.Tusilazimishane kujilinda,kila mtu ashinde mechi zake.
Acha upuuzi.

Katika mapambano haya ni lazima serikali itoe uongozi. Kuna nafasi ya mtu mmoja mmoja na nafasi ya Serikali.

Kwa mfano, kuvaa barakoa hakukusaidii wewe uliyevaa bali kunakuzuia wewe usiwaambukize watu wengine. Sasa hata wewe ntu mmoja ukivaa barakoa halafu wenzako hawajavaa, itakusaidia nini? Lakini serikali ina uwezo wa kutoa maelekezo kuwa kila mmoja avae barakoa. Seerikali inaweza kufanya hivyo, lakini wewe kama mtu binafsi, huwezi.

Serikali ina uwezo wa kutoa maelekezo kuwa kila mahali, ndani ya mabasi, makanisani, mikutanoni, kwenye sherehe, ni marufuku kujazana, wewe mtu binafsi unaweza kutoa maelekezo hayo? Lakini Serikali inaweza kupiga marufuku sherehe mbalimbali. Wewe mtu binafsi unaweza?

Kwa hiyo watetezi wa ukimya wa Serikali, kwa ujumla ni wajinga, wanatetea upumbavu. Kama kila kitu kinaweza kufanya na mtu mmoja mmoja, umuhimu wa Serikali ni upi?
 
mkuu Kwanza punguza woga kikubwa unafahamu taratibu za kujikinga ni vyema ukazi zingatia
Na una uhakika kila Mtanzania, vijijini na mijini, watoto kwa watu wazima, wazee kwa vijana, wanazifahamu? Acha kuwa self-centred kiasi hicho.
 
Nyuzi zingine za kipumbavu Tu!!

Elimu ipi inayohusu kujikinga na Corona wewe huna???

Njia ipi unadhani serikali ikifanya tofauti na zinazifanyika duniani huko inaweza kuzuia hayo usemayo?

Mtu kutwa kulalama tu halafu hata huugui bhana!!
 
Wengi wa wale wenye access ya vitu vingi vizuri kwenye maisha tunayoishi ikiwa ni pamoja na wasomi na wafanyabiasha wakubwa ndio wengi wao wanapata shida ya upumuaji na homa ya mapafu

Sijui hivi vitu vinahusianaje😇
Mungu tunusuru watu wako 🙏
Imbeni tu mapambio simnataka mbaki nyie ili mfaidi keki ya taifa.
 
Back
Top Bottom