Korona ipo jamani
Mimi mwenyewe nimeshuhudia vifo Zaid ya 3 vya mke na mume vimefuatana mfululizo sababu za vifo vyote inasema wamefariki ghafla
 
Bibi yangu aliniambia ujinga hauna kidonge. Korona ipo na inaua chukueni tahadhari achaneni na wanasihasa matapeli
 
Nahisi kuna ka movement cha wafanyabiashara na mabeberu wanaotaka kuirudisha covid 19 kwa kasi ili wapige hela.

SIO KWA TANZANIA YA LEO, WATAKWAMA

Mkuu tayari wajanja wapo wengi wameiga kwa mzee wa Loliondo ...Sasa hivi wamekuja na kitu inaitwa NIMRCAF ambavyo wengine wanadai inatibu na wengine wanasema ni makorokoro ya lishe dawa.
 
Nini kimebaki?

Kwani kuambia watu ukweli utapungukiwa na nini?

Jamani watu wanakuputika jamani

Hii sio mzaha jamani

Eeeh mungu nini hiki

Unajua nilikua nachukulia normal lakini hii new ni hatari sio mambo ya week 2 tena hii ni fasta tu

Tunapoteza tu watu jamani

Proffesa mamiro kaniuma!!!!among of the best women ambao ni wapambanaji nimeumia mnooo

Tunakwenda wapi sasa?

Tupo gizani ama?

Sielewi hadi lini sasa?

Nawafikiria wazee wangu bibi zangu na babu zangu nachokaaah

Uzidi kumpumzika kwa amani professor delphina mamiro
Video yako ya youtube imeniuma mnoo tumempoteza msomi na mtaalam

Kimebaki nini sasa?
 
Kila nikiingia social network,matangazo ya MTU kupoteza ndugu na jamaa ni mengi sana, hali hii si kawaida its total extreme
 
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?

Mtu mwenye busara, kukubali kwamba tulikosea na hali ni mbaya kuliko tulivyofikiria ni jambo la kawaida. Na pia kuna uwezekano kwamba ni kweli huko nyuma tatizo la Covid-19 Tanzania lilikuwa dogo sana, lakini sasa hali zimebadilika, na huenda hata tumeingilia na strain mpya za Covid-19 ambazo huko nyuma hazikuwepo.

Inashangaza sana kwamba hadi sasa taasisi zimeamua kuchukua maamuzi za kutoa matamko yao bila kuwapo tamko rasmi la serikali. Hili ni jambo lisilokubalika hata kidogo, lazima serikali ichukue nafasi ya kwanza katika kuwaongoza watanzania katika janga hili, sio kuachia watu mmoja mmoja, familia au taasisi huku serikali inakaa kimya.

Tunasubiri nini hasa, kwamba tumpoteze raisi, au makamu wa raisi, au spika au mawaziri kadhaa kwa Covid-19 ndio tukiri kwamba tuna tatizo la Corona nchini? Hawa wananchi, wataalamu wetu, wazee wetu, watoto wetu, waume zetu, wake zetu, marafiki zetu nk wanaokufa kila siku wao si muhimu kwa serikali kuona kuna uharaka mno wa kuweka mkakati maalumu?

Labda ni vema kwa wenye utaalamu wa sheria kuanza kufikiria kuwafikisha viongozi wetu Mahakama ya Kimataifa ICC kwa kosa la kuwanyima kimakusudi wananchi haki ya kuendelea kuishi kwa kuacha waambukizwe na kufa kwa Covid-19, ikiwa ni pamoja na kuzuia chanjo. Organization zinazopigania haki za binadamu mnapaswa kuanza kufikiria hili.

Serikali inatakiwa sio tu kutoa maelekezo ya kujilinda kama kuzuia mikusanyiko na kuvaa barakoa, bali pia kuwa na mkakati wa matibabu unaoelweka kwa wanaougua Covid-19. Imefikia mahali ambapo wengi wa wanaogua wanapelekwa hospitali kwa ajili ya kufia huko, kwa kuwa serikali haina mkakati maalumu wa kushughulikia wagonjwa wa Covid-19.

Na pia serikali sasa inabidi ijikite kwenye kupima na kutoa takwimu za wenye virusi, wanaoumwa na wanaokufa kwa Covid-19. Tutakaa kimya hadi lini?

Serikai inapaswa kukumbuka kile wahenga walisema - mficha maradhi mauti humuumbua!
 
Mkuu, kama wewe unaweza kuvaa barakoa kila mahali na kukaa ndani kaa., kama unasubiri kuambiwa ujilinde ndio ujilinde karagabaho. Tusilazimishane kujilinda, kila mtu ashinde mechi zake.
 
'
JamiiForums329407765.jpg


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?...
Mkuu Kwanza punguza woga kikubwa unafahamu taratibu za kujikinga ni vyema ukazi zingatia
 
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?...
Tanzania hatuna corona...ipo chache sana...walioenda nje ndio wameileta...'' Alisikika kiongozi mmoja.
 
Back
Top Bottom