Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Mkuu,kama wewe unaweza kuvaa barakoa kila mahali na kukaa ndani kaa.,kama unasubiri kuambiwa ujilinde ndio ujilinde karagabaho.Tusilazimishane kujilinda,kila mtu ashinde mechi zake.
Acha upuuzi.

Katika mapambano haya ni lazima serikali itoe uongozi. Kuna nafasi ya mtu mmoja mmoja na nafasi ya Serikali.

Kwa mfano, kuvaa barakoa hakukusaidii wewe uliyevaa bali kunakuzuia wewe usiwaambukize watu wengine. Sasa hata wewe ntu mmoja ukivaa barakoa halafu wenzako hawajavaa, itakusaidia nini? Lakini serikali ina uwezo wa kutoa maelekezo kuwa kila mmoja avae barakoa. Seerikali inaweza kufanya hivyo, lakini wewe kama mtu binafsi, huwezi.

Serikali ina uwezo wa kutoa maelekezo kuwa kila mahali, ndani ya mabasi, makanisani, mikutanoni, kwenye sherehe, ni marufuku kujazana, wewe mtu binafsi unaweza kutoa maelekezo hayo? Lakini Serikali inaweza kupiga marufuku sherehe mbalimbali. Wewe mtu binafsi unaweza?

Kwa hiyo watetezi wa ukimya wa Serikali, kwa ujumla ni wajinga, wanatetea upumbavu. Kama kila kitu kinaweza kufanya na mtu mmoja mmoja, umuhimu wa Serikali ni upi?
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,406
2,000
mkuu Kwanza punguza woga kikubwa unafahamu taratibu za kujikinga ni vyema ukazi zingatia
Na una uhakika kila Mtanzania, vijijini na mijini, watoto kwa watu wazima, wazee kwa vijana, wanazifahamu? Acha kuwa self-centred kiasi hicho.
 

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,513
2,000
Nyuzi zingine za kipumbavu Tu!!

Elimu ipi inayohusu kujikinga na Corona wewe huna???

Njia ipi unadhani serikali ikifanya tofauti na zinazifanyika duniani huko inaweza kuzuia hayo usemayo?

Mtu kutwa kulalama tu halafu hata huugui bhana!!
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
3,084
2,000
Wengi wa wale wenye access ya vitu vingi vizuri kwenye maisha tunayoishi ikiwa ni pamoja na wasomi na wafanyabiasha wakubwa ndio wengi wao wanapata shida ya upumuaji na homa ya mapafu

Sijui hivi vitu vinahusianaje😇
Mungu tunusuru watu wako 🙏
Imbeni tu mapambio simnataka mbaki nyie ili mfaidi keki ya taifa.
 

koro-boy

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
560
500
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?...
Mhuu kwani watu wanakufa sana? au watu wa Kilimanjaro na Arusha tu tunaona Coaster nyingi zikielekea huko. Do you matter at all? Chukaua hatua acha kulalamika.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,919
2,000
Corona ipo duniani na Tanzania siyo kisiwa.

Nchi kuwa na Corona siyo aibu, maana kirusi hakijui mipaka ya kisiasa...
Mpigie huyu 0783132277 au 0715132277 anaitwa Sele ni mshauri mkuu wa CCM idara ya mitaani club Bar vijiweni kila kona zote zenye mikusanyiko ikiwemo super market, mpigieni mwambieni kwa kuwa alisema magufuli humsikiliza sana nina imani mkimpigia wengi atafikisha salam ikulu kwa haraka zaidi.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,919
2,000
Hali ni mbaya sana watu wanakufa kimya kimya wanaogopa kusema ni corona kwa hofu ya kutengwa na jamii
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,919
2,000
Awareness kama tunayo inatosha ss kujikinga wenyewe. Serikali haijakataza raia kujikinga na covid...
Serikali wapige marufuku salam za kushikana mikono wasisitize ndoo kukaa kila ofisini zikiwa na sabuni maji tiririka
 

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
1,382
2,000
Nakumbuka mwaka juzi 2019 mwishoni watu tuliumwa sana na hadi leo hatujajua ni nini kilikuwa chanzo, ila kama hali hiyo ingetokea mwaka jana hadi mwaka huu basi tungerahisisha tu kuwa ni corona.
Na ndiyo maana kupima lilikuwa ni janbo muhimu sana.

Rais Magufuli anataka kuendesha nchi kimbumbumbu. Hataki kupima, hataki takwimu! Mtu wa namna hiyo, hivi anatakiwa kuwekwa kundi gani?

Katika Dunia ya kisasa, kila jambo, liwe jema au baya, cha kwanza ni takwimu. Magufuli hataki takwimu. Hivi kweli huyu ni kiongozi anayehitajika kwenye karne hii?
 

wilmar

Senior Member
Nov 27, 2018
190
250
Hapana, mi nadhani tahadhari ya mtoa mada ina mashiko. Bila kuwaambia watu wote kama ilivyokua mwaka jana, usitegemee watu wa kawaida kuchukua tahadhari, na hilo ni jambo la hatari. Hivyo kuwapa elimu wananchi wote ni jambo bora na jema kuliko kila mmoja kujilinda kivyake, kwani ikitokea hii strain ikasambaa hadi kwa wananchi wengi wewe huoni ni hatari?!
mkuu serikali ilisha Jenga imani kwa wananchi na ilifanikiwa kwa ilo shida na wasiwasi ni Kama watakili kuwa upo watajenga ofu kwa kiasi kikubwa Jambo ambalo litasababisha mahambukizi yasambae kwa Kasi mkuu serikali inaona na inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na janga ili la Corona tuendelee kujifukiza na kufanya mazoezi na kufuata tahadhali nyingine zinazoelekezwa na wataharamu wa afya.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom