UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,987
2,000
Wataalam wa afya ndiyo wanaua watu!Corona inapenda sana upelekwe hospitali ili ukalale kwa mgongo ikumalize.Rafiki namba moja wa Corona ni kulala kwa Mgongo.Adui namba moja wa Corona ni mazoezi ya mapafu,hili hutofundishwa popote pale.Ambacho utafundishwa kwa wingi sana ni ujinga wa kula malimao na kujifukizia!
Acha kudanganya watu, mtu hawezi kuvuta pumzi unamwambia akafanye maziezi? Wakati oxygen haifiki hata kichwani ?Mtu hana fahamu unamlisha malimao. Acha kudanganya watu wewe. Wewe unayejiona mzima usisubiri uambiwe ufanye sijui maziezi,kula malimao anza kujenga mwili kama ya kuumwa.Ukiumwa wewe hata hayo malimao hakuna atakaekupa.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
31,904
2,000
Acha kudanganya watu ,mtu hawezi kuvuta pumzi unamwambia akafanye maziezi?wakati oxygen haifiki hata kichwani ?Mtu hana fahamu unamlisha malimao .Acha kudanganya watu wewe.Wewe unayejiona mzima usisubiri uambiwe ufanye sijui maziezi,kula malimao anza kujenga mwili kama ya kuumwa.Ukiumwa wewe hata hayo malimao hakuna atakaekupa
Kwa nini usubiri hadi hatua ya kushindwa kuvuta pumzi ndiyo uanze kuchukua hatua? Yaani unachukua hatua ukiwa katika stage ya kufa?Na ni wapi nimesema kuwa watu wachukue hatua wakiwa katika stage ya kufa?
 

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,987
2,000
Kwa nini usubiri hadi hatua ya kushindwa kuvuta pumzi ndiyo uanze kuchukua hatua?Yaani unachukua hatua ukiwa katika stage ya kufa?Na ni wapi nimesema kuwa watu wachukue hatua wakiwa katika stage ya kufa?
Ndio elimu watu wanatakiwa kupewa, wasisubiri hapo. So unakuta mpakq.mbunge anafia hotelini kizembe eti anajifukiza shame of.my country hii ingekuwa prevented kabisa kama wangempa right health information
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,092
2,000
Kaandika ujumbe huu hapa chini kupitia twitter:

Ndugu zangu tuchukue tahadhali sana, watu wanakufa sana, hii sio kawaida. Leo hii tu nimepokea taarifa za watu watano ninaowafahamu, Mwenyezi Mungu awapumzishe mahali pema.

Heche.PNG
 

Mbeshe

Senior Member
Jan 26, 2021
181
250
Kaandika ujumbe huu hapa chini kupitia twitter:

Ndugu zangu tuchukue tahadhali sana, watu wanakufa sana, hii sio kawaida. Leo hii tu nimepokea taarifa za watu watano ninaowafahamu, Mwenyezi Mungu awapumzishe mahali pema.
Sijaelewa tahadhari ya nini.
 

MC44

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
1,750
2,000
Kaandika ujumbe huu hapa chini kupitia twitter:

Ndugu zangu tuchukue tahadhali sana, watu wanakufa sana, hii sio kawaida. Leo hii tu nimepokea taarifa za watu watano ninaowafahamu, Mwenyezi Mungu awapumzishe mahali pema.
Bado una wenge hebu andika tena
 

mnengene

JF-Expert Member
Nov 21, 2011
2,315
2,000
Korona ipo jamani
Mimi mwenyewe nimeshuhudia vifo Zaid ya 3 vya mke na mume vimefuatana mfululizo sababu za vifo vyote inasema wamefariki ghafla
 

SAIDWE

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
377
500
Bibi yangu aliniambia ujinga hauna kidonge. Korona ipo na inaua chukueni tahadhari achaneni na wanasihasa matapeli
 

Kite Munganga

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,741
2,000
Nahisi kuna ka movement cha wafanyabiashara na mabeberu wanaotaka kuirudisha covid 19 kwa kasi ili wapige hela.

SIO KWA TANZANIA YA LEO, WATAKWAMA

Mkuu tayari wajanja wapo wengi wameiga kwa mzee wa Loliondo ...Sasa hivi wamekuja na kitu inaitwa NIMRCAF ambavyo wengine wanadai inatibu na wengine wanasema ni makorokoro ya lishe dawa.
 

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,766
2,000
Nini kimebaki?

Kwani kuambia watu ukweli utapungukiwa na nini?

Jamani watu wanakuputika jamani

Hii sio mzaha jamani

Eeeh mungu nini hiki

Unajua nilikua nachukulia normal lakini hii new ni hatari sio mambo ya week 2 tena hii ni fasta tu

Tunapoteza tu watu jamani

Proffesa mamiro kaniuma!!!!among of the best women ambao ni wapambanaji nimeumia mnooo

Tunakwenda wapi sasa?

Tupo gizani ama?

Sielewi hadi lini sasa?

Nawafikiria wazee wangu bibi zangu na babu zangu nachokaaah

Uzidi kumpumzika kwa amani professor delphina mamiro
Video yako ya youtube imeniuma mnoo tumempoteza msomi na mtaalam
Kimebaki nini sasa?
 

kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,238
2,000
Kila nikiingia social network,matangazo ya MTU kupoteza ndugu na jamaa ni mengi sana, hali hii si kawaida its total extreme
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,406
2,000
Hivi kwa nini hadi sasa serikali bado inafumbia macho ukweli kwamba Tanzania imefikia hali mbaya sana ya maambukizi, kuugua na vifo vinavyotokana na Covid-19? Ni kwa kuwa raisi na voingozi wengine wanaona aibu kukubali ukweli kwa kuwa huko nyuma walitoa kauli zilizoonyesha kwamba Tanzania hatuna Covid-19?

Mtu mwenye busara, kukubali kwamba tulikosea na hali ni mbaya kuliko tulivyofikiria ni jambo la kawaida. Na pia kuna uwezekano kwamba ni kweli huko nyuma tatizo la Covid-19 Tanzania lilikuwa dogo sana, lakini sasa hali zimebadilika, na huenda hata tumeingilia na strain mpya za Covid-19 ambazo huko nyuma hazikuwepo.

Inashangaza sana kwamba hadi sasa taasisi zimeamua kuchukua maamuzi za kutoa matamko yao bila kuwapo tamko rasmi la serikali. Hili ni jambo lisilokubalika hata kidogo, lazima serikali ichukue nafasi ya kwanza katika kuwaongoza watanzania katika janga hili, sio kuachia watu mmoja mmoja, familia au taasisi huku serikali inakaa kimya.

Tunasubiri nini hasa, kwamba tumpoteze raisi, au makamu wa raisi, au spika au mawaziri kadhaa kwa Covid-19 ndio tukiri kwamba tuna tatizo la Corona nchini? Hawa wananchi, wataalamu wetu, wazee wetu, watoto wetu, waume zetu, wake zetu, marafiki zetu nk wanaokufa kila siku wao si muhimu kwa serikali kuona kuna uharaka mno wa kuweka mkakati maalumu?

Labda ni vema kwa wenye utaalamu wa sheria kuanza kufikiria kuwafikisha viongozi wetu Mahakama ya Kimataifa ICC kwa kosa la kuwanyima kimakusudi wananchi haki ya kuendelea kuishi kwa kuacha waambukizwe na kufa kwa Covid-19, ikiwa ni pamoja na kuzuia chanjo. Organization zinazopigania haki za binadamu mnapaswa kuanza kufikiria hili.

Serikali inatakiwa sio tu kutoa maelekezo ya kujilinda kama kuzuia mikusanyiko na kuvaa barakoa, bali pia kuwa na mkakati wa matibabu unaoelweka kwa wanaougua Covid-19. Imefikia mahali ambapo wengi wa wanaogua wanapelekwa hospitali kwa ajili ya kufia huko, kwa kuwa serikali haina mkakati maalumu wa kushughulikia wagonjwa wa Covid-19.

Na pia serikali sasa inabidi ijikite kwenye kupima na kutoa takwimu za wenye virusi, wanaoumwa na wanaokufa kwa Covid-19. Tutakaa kimya hadi lini?

Serikai inapaswa kukumbuka kile wahenga walisema - mficha maradhi mauti humuumbua!
 

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
945
1,000
Mkuu, kama wewe unaweza kuvaa barakoa kila mahali na kukaa ndani kaa., kama unasubiri kuambiwa ujilinde ndio ujilinde karagabaho. Tusilazimishane kujilinda, kila mtu ashinde mechi zake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom