CHAMVIGA
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 7,687
- 2,238
Dodoma.Sakata la Watanzania walioficha Sh314 bilioni katika mabenki nchini Uswisi linatarajiwa kutikisa Mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea Mjini Dodoma, endapo Serikali itashindwa kuwasilisha kwa mara nyingine ripoti ya uchunguzi.
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), jana alikwenda mbali zaidi na kusema kama Serikali itaendelea kulipiga danadana suala hilo na kushindwa kutoa ripoti hiyo, basi safari hii bungeni hapatatosha.
Ripoti hiyo ya uchunguzi, inatokana na hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) aliyoiwasilisha bungeni mwaka jana na Bunge kuagiza Serikali kufanya uchunguzi.
Kutokana na agizo la Bunge, Serikali iliunda kikosi kazi kilichohusisha Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa, Takukuru na wataalamu wa fedha kuchunguza sakata hilo linaloelezwa kuwa Nyeti.
Ripoti ya kikosi kazi hicho ilikuwa iwasilishwe Bunge la Aprili mwaka huu, lakini Serikali ikaomba muda zaidi lakini haikuweza kuiwasilisha Bunge la Oktoba, na sasa kuna wasiwasi isiwasilishwe pia.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jana, Mpina alisema hata kikao cha kupeana taarifa (breafing) cha Wabunge wote kilichofanyika juzi Ukumbi wa Spika, suala hilo halikuguswa kabisa.
Hili ni jambo nyeti sana, sasa kwenye vikao vya kupeana taarifa halipo nataka niwe mkweli kwamba, kama Serikali haitaleta ripoti hii katika Bunge hili hapatatosha, alisema Mpina.
Mbunge huyo alisema Serikali isipowasilisha ripoti hiyo, wao kama Wabunge watachukua hatua kwa kutumia kanuni za Bunge akisisitiza kuwasilishwa kwa ripoti hiyo ni matakwa ya Bunge.
Tunataka kujua kikosi kazi hiki cha Serikali kimeona nini au kimegundua nini. Watanzania wanataka kujua nini hatima ya fedha zao zilizotoroshwa kwenda Uswisi. alisema Mpina.
Mpina alisema Serikali haiwezi kukwepa kuwasilisha ripoti hiyo akisema ahadi yao iko kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) na wabunge hawataki kusikia tena danadana za Serikali.
Kwa mujibu wa Mpina, yeye ni miongoni mwa Wabunge waliohojiwa baada ya kutamka bungeni kuwa zaidi ya Sh11.9 trilioni zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 na mwaka 2008.
Nilipolisema hili jambo niliikabidhi Serikali kupitia Bunge taarifa za tafiti mbalimbali ili ifuatilie hizo fedha na kuzirejesha na baadaye Zitto akaja na hoja ya Bilioni 314, alisema.