Serikali isipotoa ripoti ya mabilioni ya uswisi, bungeni patachimbika~wabunge.

CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,687
2,238
Dodoma.Sakata la Watanzania walioficha Sh314 bilioni katika mabenki nchini Uswisi linatarajiwa kutikisa Mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea Mjini Dodoma, endapo Serikali itashindwa kuwasilisha kwa mara nyingine ripoti ya uchunguzi.
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), jana alikwenda mbali zaidi na kusema kama Serikali itaendelea kulipiga danadana suala hilo na kushindwa kutoa ripoti hiyo, basi safari hii bungeni hapatatosha.
Ripoti hiyo ya uchunguzi, inatokana na hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) aliyoiwasilisha bungeni mwaka jana na Bunge kuagiza Serikali kufanya uchunguzi.
Kutokana na agizo la Bunge, Serikali iliunda kikosi kazi kilichohusisha Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa, Takukuru na wataalamu wa fedha kuchunguza sakata hilo linaloelezwa kuwa “Nyeti”.
Ripoti ya kikosi kazi hicho ilikuwa iwasilishwe Bunge la Aprili mwaka huu, lakini Serikali ikaomba muda zaidi lakini haikuweza kuiwasilisha Bunge la Oktoba, na sasa kuna wasiwasi isiwasilishwe pia.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili jana, Mpina alisema hata kikao cha kupeana taarifa (breafing) cha Wabunge wote kilichofanyika juzi Ukumbi wa Spika, suala hilo halikuguswa kabisa.
“Hili ni jambo nyeti sana, sasa kwenye vikao vya kupeana taarifa halipo…nataka niwe mkweli kwamba, kama Serikali haitaleta ripoti hii katika Bunge hili hapatatosha,” alisema Mpina.
Mbunge huyo alisema Serikali isipowasilisha ripoti hiyo, wao kama Wabunge watachukua hatua kwa kutumia kanuni za Bunge akisisitiza kuwasilishwa kwa ripoti hiyo ni matakwa ya Bunge.
“Tunataka kujua kikosi kazi hiki cha Serikali kimeona nini au kimegundua nini. Watanzania wanataka kujua nini hatima ya fedha zao zilizotoroshwa kwenda Uswisi.” alisema Mpina.
Mpina alisema Serikali haiwezi kukwepa kuwasilisha ripoti hiyo akisema ahadi yao iko kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge (hansard) na wabunge hawataki kusikia tena danadana za Serikali.
Kwa mujibu wa Mpina, yeye ni miongoni mwa Wabunge waliohojiwa baada ya kutamka bungeni kuwa zaidi ya Sh11.9 trilioni zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 na mwaka 2008.
“Nilipolisema hili jambo niliikabidhi Serikali kupitia Bunge taarifa za tafiti mbalimbali ili ifuatilie hizo fedha na kuzirejesha na baadaye Zitto akaja na hoja ya Bilioni 314,” alisema.
 
Ni vigunu sana kutoa majina ya waliohifadhi mabilioni hayo kwani na viongozi waandamizi wa serikali wamo pamoja na watu wengine maarufu! Kwa nini hadi sasa imekuwa vigumu kuwataja wamiliki wa KAGODA, MREREMETA, DEEP GREEN FINANCE nk. hadharani?
 
Usimsahau na Mbowe pia yumo.
 
!
!
"Hili ni jambo nyeti sana, sasa kwenye vikao vya kupeana taarifa halipo…nataka niwe mkweli kwamba, kama Serikali haitaleta ripoti hii katika Bunge hili hapatatosha,"
!
!
huyu nae, eti hapatatosha, tangu lini?
 
kama hamjamsikia Nape aka Vuvuzela wa CCM akiliongelea basi ujue kapigwa Speed Gavana. Hili jambo haliwezekani kabisa!! ni sawa na Sajenti kumfungulia mashitaka Meja.

I mean Bunge halina meno ya kuwadhibiti hawa watu, maana ni VIGOGO na ukijaribu kuwagusa tu - basi tunaazima maturubai na viti mapema.
 
Ni vigunu sana kutoa majina ya waliohifadhi mabilioni hayo kwani na viongozi waandamizi wa serikali wamo pamoja na watu wengine maarufu! Kwa nini hadi sasa imekuwa vigumu kuwataja wamiliki wa KAGODA, MREREMETA, DEEP GREEN FINANCE nk. hadharani?

ukikamata mafisadi nchi itayumba ~~pinda
 
kama hamjamsikia Nape aka Vuvuzela wa CCM akiliongelea basi ujue kapigwa Speed Gavana. Hili jambo haliwezekani kabisa!! ni sawa na Sajenti kumfungulia mashitaka Meja.

I mean Bunge halina meno ya kuwadhibiti hawa watu, maana ni VIGOGO na ukijaribu kuwagusa tu - basi tunaazima maturubai na viti mapema.

No evidence no right to speak.
 
Wanao sema bunge liendelee hata kama ripoti ya mamilioni ya uswiss haijatolewa waseme ndioooooo!!! Ndiooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!!!!
wanao pinga waseme sio. Sioo waliosema ndio wameshinda BUNGE LINAENDELEA
 
Hivi Zitto siku atakapokanyaga bungeni atakaa kiti kipi?. Isijekuwa anaona aibu kuingia bungeni coz atakaa nyuma.
 
Huyo mbunge ni mpuuzi. Hiyo hela ni ya ccm na zitarudi kabla ya uchaguzi wa 2015.
 
Haya mambo yanakera sana.Issues zinazohusu Watanzania mnazifanya kuwa za kisiasa.Mko wa hovyo sana.Yaani mmepoteza mwelekeo kabisa.Tunapashwa kujikita kqenye kutetea wananchi sio vyama.
Usimsahau na Mbowe pia yumo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom